Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi),Joseph Kakunda(kushoto) akipanda ngazi kukagua mradi wa m...
![]() |
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi),Joseph Kakunda akipanda ngazi kukagua mradi wa maji kijiji cha Eworendeke Kata ya Kimokouwa wilayani Longido. |
![]() |
Mhe Joseph Kakunda na Mkuu wa wilaya ya Longido,Godfrey Chongolo wakijumuika na wananchi kuimba wimbo wa kufurahia mradi wa maji. |
![]() | |
Mhe Joseph Kakunda na Mkuu wa wilaya ya Longido,Godfrey Chongolo wakiagana na wananchi wa Kijiji cha Ranchi. |
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa na Serikali za
Mitaa(Tamisemi),Joseph Kakunda amepongeza ujenzi wa miradi ya maji
inayotekelezwa katika mpango wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya
Tabia Nchi katika wilaya za Longido,Monduli na Ngorongoro.
Mradi huo unaosimamiwa kwa pamoja na
Ofisi ya Rais-Tamisemi,taasisi ya kimataifa ya maendeleo na
mazingira(IIED) na Haki Kazi Catalyst unatarajiwa kuwanufaisha wananchi
walio katika wilaya hizo tatu.
Akiwa katika Kijiji cha Eworendeke
Kata ya Kimokouwa alipongeza hatua iliyofikiwa ya kuwawezesha wananchi
kupata maji safi kwaajili ya matumizi ya nyumbani pamoja na mifugo yao
ikizingatiwa wilaya ya Longido asilimia 95 ya wakazi wake ni wafugaji.
Amesema
mkandarasi amekua mzalendo kwa kujenga miundombinu ya maji tenki pamoja
eneo la kunyweshea mifugo kwa thamani ya Sh 36 milioni na kuonya
wakandarasi wasio na uzalendo wanatekeleza miradi kwa gharama kubwa
lakini inakua haina ufanisi.
Mkuu wa
wilaya ya Longido,Godfrey Chongolo amesema wilaya yake ipo jumla ya
miradi 14 inayofadhiliwa na IIED kwa lengo la kuwawezesha wananchi
kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Naye
Flora Assey ambaye ni mratibu wa mradi huo kutoka Ofisi ya Mkuu wa mkoa
wa Arusha amesema lengo la mradi huo ni kuweka mfumo utakaowezesha
upimaji wa kiutendaji katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya
tabia nchi.
Imeandaliwa na mtandao wa www.rweyemamuinfo.blogspot.com
COMMENTS