MATENGENEO MAKUBWA MASHINE NAMBA MOJA YA KUFUA UMEME KIDATU YAFIKIA ZAIDI YA ASILIMIA 95 KUKAMILIKA
HomeMikoani

MATENGENEO MAKUBWA MASHINE NAMBA MOJA YA KUFUA UMEME KIDATU YAFIKIA ZAIDI YA ASILIMIA 95 KUKAMILIKA

  Mafundi wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), wakishirikiana na wakandarasi kutoka kampuni ya Concar kutoka Croatia, wakifanya ma...


 Mafundi wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO),
wakishirikiana na wakandarasi kutoka kampuni ya Concar kutoka Croatia, wakifanya matengenezo makubwa ya mashine namba moja ya kufua umeme, kwenye Kituo cha kufua umeme wa maji Kidatu mkoani Morogoro Desemba 22, 2017. Kituo hicho kina jumla ya mashine 4 (Turbines) za kufua umeme wa Megawati 204.





NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said, Kidatu


MATENGENEZO
makubwa ya mashine namba moja kati ya nne za kufua umeme wa maji kwenye Kituo
cha kufua umeme wa maji Kidatu mkoani Morogoro yamefikia zaidi ya asilimia 95
kukamilika.


Msimamizi
wa matengenezo ya mashine hiyo Mhandisi Rajabu Kindunda amewaambia wahariri wa
vyombo vya habari waliotembelea kituo hicho Desemba 22, 2017.


"Kwa
sasa tumeanza majaribio ya mashine kuzunguka bila kutumia nguvu za maji, mafundi wanazungusha mashine hiyo kwa kutumia mikono ili kuangalia
usahihi wa unyookaji wa shafti,”alisema


Alisema
hatua itakayofuata ni kuunganisha kipande yanapoingilia maji ili kuzungusha
huo mtambo na sehemu ya kuzalishia umeme na Jumapili mafundi hao wanaoshirikiana na mkandarasi kutoka kampuni ya Concar kutoka Croatia wataanza majaribio ya
kuzungusha mtambo wenyewe.


Aidha
Meneja wa Kituo hicho, Mhandisi Anthony Mbushi Amesema Kidatu kuna mitambo minne na kila
mmoja unauwezo wa kuzalisha umeme Megawati 51 na hivyo kufanya jumla ya Megawati 204 za umeme ambao unaingizwa kwenye Gridi ya Taifa.


”Tuliona
tufanye matengenezo makubwa kwani kila baada ya miaka 20 huwa tunafanya zoezi kama hili ili kurejesha mashine kufanya kazi bora kwa kipindi hicho ili kuhakikisha
mtambo unarejea kwenye hali yake ya kawaida.” Alisema.


Naye
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, anayeshughulikia uzalishaji umeme (Power
Generation), Mhandisi Abdallah Ikwasa, alisema, umeme unaozalishwa kutokana na
maji ni wa bei nafuu na kupongeza juhudi za serikali katioka kuhakikisha
wananchi wanatunza mazingira ili kutunza vyanzo vya maji ambayo hutumika
kuzalisha umeme.


“Tunaishukuru
sana serikali kwa hatua inazochukua kama kuboresha upatikanaji wa maji kwa
kutunza vyanzo vya maji (mazingira), hususan bonde la Mto Rufiji, timu
iliyoundwa na Makamu wa Rais ambayo imefanya kazi nzuri nahuenda baada ya muda
matokeo mazuri tutayaona.” Alisema.


Akifafanua
zaidi alisema, juhudi zinazofanywa na serikali kuongeza vyanzo vya kuzalisha
umeme kwa kutumia vyanzo vya maji kama vile Stigler
Gorge
zitasaidia sana nchi yetu na hii inaonyesha serikali ilivyodhamiria
kupunguza gharama za umeme kwa wananchi kwa vitendo.” Alisema.


Kwa
upande wake, Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO Bi. Leila Muhaji, amesema Shirika
limekuwa karibu na wananchi wanaoishi karibu na vyanzo vya maji na vituo vya
umeme ili kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika kutunza mazingira ili
kunusuru vyanzo vya maji.


“Na
ushirikiano wetu na wananchi uko katika maeneo mbalimbali kama vile kutoa
huduma za afya bure kwa wananchi wanaoishi jirani na vituo vyetu vya kufua
umeme, shule za awali lakini pia hata usafiri yumekuwa tukiwapatia usafiri wa
bure wananchi ambapo hutumia magari yetu ya wafanyakazi kwenda maeneo jirani na
vituo.


Geti la kuruhusu maji kuelekea kwenye mashine turbines kwenye bwawa la Kidatu mkoani Morogoro
 Geti la kuruhusu maji kuelekea kwenye mashine za kufua umeme wa maji Kidatu.
  Geti la kuruhusu maji kuelekea kwenye mashine za kufua umeme wa maji Kidatu.
 Mhandisi Abdallah Ikwasa, (kulia), akizungumza kuhusu kituo cha kufua umeme wa maji Kidatu, mkoani Morogoro. Katikati ni Meneja wa Kituo hicho, Mhandisi Anthony Mbushi na kushoto ni Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji.
 Mhandisi Ikwasa, (kulia), akibadilishana mawazo na Afisa Mazingira wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Bw. Yusuf Kamote.
 Geti la kupitishioa maji Kidatu.
 Meneja wa Kituo cha kufua umeme Kidatu mkoani Morogoro, Mhandsi Anthony Mbushi (kushoto), akifafanua masuala ya kiufundi kwenye chumba cha udhibiti umeme kilichoko chini ya ardhi kwenye Kituo cha Kidatu mkoani Morogoro.
 Maafisa wa TANESCO na baadhi ya wahariri wakiangalia mashine iliyoharibika, a,mbayo kwa sasa iko kwenye matengenezo makubwa.
Wasimamizi wa chumba cha kudhibiti mifumo ya umeme wakiwa kazini wakati walipotembelewa na wahariri wa vyombo vya habari Kituo cha Kidatu mkoani Morogoro.
Peter Rauya, (kushoto) na Senorina Maganga  wa chumba cha udhibiti mifumo ya umeme wakiwa kazini.
Wahariri wakipatiwa maelezo na maafisa wa TANESCO kuhusu utendaji kazi wa mashine za kufua umeme (Turbines) kituom cha Kidatu.
Waharorio wakiangalia mashine iliyoharibika ambayo sasa iko kwenye matengenezo makubwa.
Mameneja wa vituo vya kufua umeme kutoka mikoani wakiwa kwenye kituo cha kufua unmeme Kidatu mkoani Morogoro. Mameneja hao kwa sasa wako katika kikao kazi hapo Kidatu.
Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji, (wapili kushoto), akiwa na baadhi ya Mameneja wa vituo vya kufua umeme vilivyoko mikoani ambao kwa sasa wako katika kikao kazi hapo Kidatu.
Mhandisi Ikwasa, akijadiliana na maafisa wake.
Mhandisi Ikwasa, akijadiliana na maafisa wake.
Wasimamizi wa chomba cha udhibiti mifumo ya umeme cha Kidatu mkoani Morogoro; kutoka kushoto ni Peter Rauya, Senorina Maganga na Nicomedy Mhina.
Msimamizi wa matengenezo ya mashine hiyo Mhandisi Rajabu Kindunda (kushoto), akiwa sambamba na wakandarasi kutoka kampuni ya Concar ya Croatia wakati wakiendelea na matengenezo hayo.
Sehemu ya kuingilia "mgodini" chini ya ardhi kwenye mitambo ya kufua umeme wa maji Kidatu mkoani Morogoro.

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MATENGENEO MAKUBWA MASHINE NAMBA MOJA YA KUFUA UMEME KIDATU YAFIKIA ZAIDI YA ASILIMIA 95 KUKAMILIKA
MATENGENEO MAKUBWA MASHINE NAMBA MOJA YA KUFUA UMEME KIDATU YAFIKIA ZAIDI YA ASILIMIA 95 KUKAMILIKA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEivW-ZYQZBwCkXL6p2Pa-wg0tCURvrUyQHiHvAzDm3ht0JncYbCqmzl-CeIi1l1SQPdt4bNV0zXQs9m-uCcOvsAkTkKIehL71orm9yVGsRXGLzW1ZJlO4Ck2k_eiz0GkrCdmwzKFrp8b8e-/s640/5R5A2449.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEivW-ZYQZBwCkXL6p2Pa-wg0tCURvrUyQHiHvAzDm3ht0JncYbCqmzl-CeIi1l1SQPdt4bNV0zXQs9m-uCcOvsAkTkKIehL71orm9yVGsRXGLzW1ZJlO4Ck2k_eiz0GkrCdmwzKFrp8b8e-/s72-c/5R5A2449.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/12/matengeneo-makubwa-mashine-namba-moja.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/12/matengeneo-makubwa-mashine-namba-moja.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy