ALIYEKUWA Mbunge Machachari wa Kigoma Kusini, Mhe. David Kafulila, ametangaza leo Novemba 22, 2017 kukihama chama chake cha C...
ALIYEKUWA Mbunge Machachari wa Kigoma Kusini, Mhe. David Kafulila, ametangaza leo Novemba 22, 2017 kukihama chama chake cha CHADEMA na habari zinadokeza kuwa huenda akajiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM), kutokana na sababu alizozieleza za kujitoa kwenye chama hicho kikuu cha upinzani nchini.
Maelezo ya Mhe. David Kafulila ambaye kuna wakati aliitwa Tumbili na aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema, kutokana na msimamo wake mkali dhidi ya rushwa na utawala bora, ameisifu serikali ya awamu ya tano ya Rais John Pombe Magufuli, hususan katika maeneo ambayo Kafulila alikuwa kiyapigania wakati akiwa bungeni. Lakini pia ushahidi mwingine kuwa huenda mwanasiasa huyo akahamia CCM unatokana na kauli ya Rais John Magufuli wakati Fulani aliwahi kumtaja Kafulila kuwa ni shujaa, licha ya kupewa majina ya Tumbili, lakini ameonyesha kuwa na uchungu na nchi yake.
Safari ya David Kafulila ilianzia CHADEMA, kabla ya kujitoa kwenye chama hicho na kujiunga na NCCR-Mageuzi, na baadaye kujitoa NCCR-Mageuzi na kurejea CHADEMA kabla ya uamuzi wake waleo. Hata hivyo Kafulila bado hajataja anajiunga na chama gani licha ya kusema atasalia kuwa mwanasiasa.
COMMENTS