OSHA YAAGIZWA KUWEKA MIKAKATI MAHUSUSI YA KIUTENDAJI
HomeJamii

OSHA YAAGIZWA KUWEKA MIKAKATI MAHUSUSI YA KIUTENDAJI

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Eric Shitindi, akiwahutubia watumishi wa Wakala wa U...

RC PAUL MAKONDA AKIHUTUBIA WAKAZI WA KEKO MCHANA HUU
MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA ATUNUKU SHAHADA NA STASHAHADA KATIKA MAHAFALI YA CHUO CHA TAKWIMU MASHARIKI MWA AFRIKA
RC MAKONDA AENDELEA NA ZIARA YAKE YA KUIJENGA DAR MPYA KWA KUTATUA KERO ZA WANANCHI







Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Eric Shitindi, akiwahutubia watumishi wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) katika kikao chao cha baraza la wafanyakazi mjini Tanga kilichofanyika leo Ijumaa Novemba 24,2017.
****
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Eric Shitindi, ameuagiza Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) kuweka mikakati mahususi ya kiutendaji itakayosaidia kuboresha mazingira ya biashara na kukuza ajira nchini. 

Mtendaji Mkuu huyo wa Wizara ametoa agizo hilo alipokuwa akiwahutubia watumishi wa OSHA katika kikao chao cha Baraza la Wafanyakazi kilichofanyika katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga.

Shitindi alifafanua kwamba mikakati hiyo inapaswa kujikita katika kuimarisha mifumo ya kiutendaji itakayolenga katika kuboresha huduma zitolewazo kwa wateja na taasisi hiyo ya umma ili kuwaondolea usumbufu watu mbali mbali wanaofanya shughuli mbali mbali za kiuchumi hapa nchini.

“Wakati mwingine tunashindwa kujipanga vizuri katika utekelezaji wa kazi zetu na hivyo kuwasababishia usumbufu mkubwa wateja. Kwa mfano unakuta mkaguzi mmoja wa Usalama na Afya mahali pa kazi anapita katika eneo fulani la kazi asubuhi na mwingine anakuja katika eneo hilo hilo mchana wakati watu hawa wangeweza kufika katika eneo la kazi kwa pamoja na kukamilisha kazi zao za kaguzi kwa wakati mmoja,” alisema Shitindi.

Aidha Katibu Mkuu huyo aliwaasa watumishi hao kufanya kazi zao za kila siku kwa kuzingatia kanuni za maadili ya utumishi wa umma ikiwemo kujiepusha na vitendo vya kutoa na kupokea rushwa.

“Maadili ya utumishi wa umma yanajumuisha mambo mengi ikiwemo mavazi stahiki, matumizi ya lugha nzuri wakati wa kuwasiliana na wateja na pia heshima baina ya watumishi na viongozi wao na miongoni mwa watumishi wenyewe,” alisema Shitindi.

Vikao vya baraza la wafanyakazi wa OSHA ambavyo hufanyika kwa mwaka mara mbili vina lengo la kutoa fursa kwa wafanyakazi kujadiliana mambo mbali mbali yanayohusu utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku ili kuleta ufanisi zaidi.


ANGALIA PICHA WAKATI WA KIKAO

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Eric Shitindi, akiwahutubia watumishi wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) katika kikao chao cha baraza la wafanyakazi mjini Tanga.
Watumishi wa OSHA wakifuatilia hotuba ya Mgeni Rasmi, Eric Shitindi, wakati wa kikao chao cha baraza la wafanyakazi kinachofanyika katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga.
Watumishi wa OSHA wakifuatilia hotuba ya Mgeni Rasmi, Eric Shitindi, wakati wa kikao chao cha baraza la wafanyakazi kinachofanyika katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga.


Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Eric Shitindi, akiwa katika picha ya pamoja na menejimenti ya OSHA nje ya ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga. Mtendaji Mkuu huyo wa Wizara alikuwa Mgeni Rasmi katika kikao cha baraza la wafanyakazi wa Wakala huo.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Eric Shitindi, akiwa katika picha ya pamoja wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa OSHA nje ya ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga. 

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: OSHA YAAGIZWA KUWEKA MIKAKATI MAHUSUSI YA KIUTENDAJI
OSHA YAAGIZWA KUWEKA MIKAKATI MAHUSUSI YA KIUTENDAJI
https://4.bp.blogspot.com/-aYRo2uCd4mU/WhhEqeyhhXI/AAAAAAAAUbo/nK9ZC9JNU1gOBli0_zTwoxw7hams_vjmgCLcBGAs/s640/PICHA%2B1%2BA.JPG
https://4.bp.blogspot.com/-aYRo2uCd4mU/WhhEqeyhhXI/AAAAAAAAUbo/nK9ZC9JNU1gOBli0_zTwoxw7hams_vjmgCLcBGAs/s72-c/PICHA%2B1%2BA.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/11/osha-yaagizwa-kuweka-mikakati-mahususi.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/11/osha-yaagizwa-kuweka-mikakati-mahususi.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy