MADIWANI WA CCM WALIOSHINDA KATIKA UCHAGUZI JIMBO LA HAI WAKABIDHIWA VYETI
HomeSiasa

MADIWANI WA CCM WALIOSHINDA KATIKA UCHAGUZI JIMBO LA HAI WAKABIDHIWA VYETI

Msimamizi wa Uchaguzi katika Jimbola Hai ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Yohana Sintoo akikabidhi cheti cha uta...

NAIBU KATIBU MKUU CCM BARA MPOGOLO AWAFUNDA VIONGOZI, WANACHAMA JIMBO LA SEGEREA NA UKONGA
KOMREDI KINANA AONGOZA KIKAO CHA MAKATIBU WAKUU WA VYAMA VYA UKOMBOZI WA KUSINI MWA AFRIKA (FRONT LINE STATE PARTIES)
NAIBU KATIBU MKUU CCM BARA, RODRICK MPOGOLO ZIARANI JIMBO LA ILALA, TEMEKE

Msimamizi wa Uchaguzi katika Jimbola Hai ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Yohana Sintoo akikabidhi cheti cha utambuzi kwa Diwani aliyechaguliwa hivi karibuni wa kata ya Weruweru Swalehe Msenges.kulia kwake ni Mkuu wa Idara ya Fedha katika Hamlamahauri  hiyo ,Juma Massatu.
Msimamizi wa Uchaguzi katika Jimbola Hai ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Yohana Sintoo akikabidhi cheti cha utambuzi kwa Diwani aliyechaguliwa hivi karibuni wa kata ya Mnadani  Nassib Mdeme ,kulia kwake ni Mkuu wa Idara ya Fedha katika Hamlamahauri  hiyo ,Juma Massatu.
Msimamizi wa Uchaguzi katika Jimbola Hai ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Yohana Sintoo akikabidhi cheti cha utambuzi kwa Diwani aliyechaguliwa hivi karibuni wa kata ya Machame Magharibi ,Martin Munisi .kulia kwake ni Mkuu wa Idara ya Fedha katika Hamlamahauri  hiyo ,Juma Massatu.
Msimamizi wa Uchaguzi katika Jimbola Hai ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Yohana Sintoo akiwa katika picha ya pamoja na Madiwani waliochaguliwa katika uchaguzi mdogo uliofanyika hivi karibuni .kutoka kushoto ni Diwani wa kata ya Mnadani ,Nasib Mdeme,Diwani wa kata ya Weruweru ,Swaleh Msenges na Diwani wa kata ya Machame Magharibi ,Martin Munisi ,Wengine katika picha ni kulia mwa msimamizi wa uchaguzi ni Msimaizi Msaidizi na Mkuu wa Idara ya Fedha Juma Massatu na kushoto ni Afisa Uchaguzi wilaya ya Hai,Edward Ntakiliho.
Madiwani waliochaguliwa hivi karibuni wakionesha vyeti vyao mara baada ya kukabidhiwa na Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Hai wakiwa na ndugu zao.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini .

MSIMAMIZI wa uchaguzi katika jimbo la Hai, mkoani Kilimanjaro ,
Ndugu Yohana Sintoo amesema kuwa zoezi la uchaguzi katika kata tatu zilizokuwa
hazina uwakilishi limekamilika salama na kuwapata viongozi watakaowawakilisha
wananchi kwenye kata husika.

Ndg Sintoo ameyasema hayo wakati akikabidhi vyeti kwa madiwani
wateule watatu walioshinda  kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika Novemba
26 mwaka huu.

“Ndugu zangu mtakumbuka kuwa mwishoni mwa wiki kulikuwa na
uchaguzi kwenye jimbo letu ambapo wananchi wa kata tatu walikuwa katika zoezi
la upigaji kura kwa lengo la kuwapata viongozi wa ngazi ya udiwani baada ya
madiwani wa kata husika kujiuzulu”

“Wananchi wa kata za Mnadani , Weruweru na Machame Magharibi
walipiga kura ili kuwapata wawakilishi wao  ambapo zoezi hilo limekamilika
bila uvunjifu wa amani kuanzia kipindi cha mikutano ya  kampeni hadi
siku ya zoezi la upigaji kura na leo tunawapatia washindi vyeti vyao”

Amesema, katika uchaguzi huo jumla ya vyama vitano vilishiriki
kwa kusimamisha wagombea wao kuomba ridhaa kwa wananchi ambavyo vilikuwa ni
CCM, CHADEMA, ACT- Wazalendo, CUF na NCCR Mageuzi.

Vyeti hivyo vilikabidhiwa kwa Salehe Msengesi (CCM) ambaye
alishinda nafasi ya udiwani katika kata ya Weruweru, Martini Munis (CCM) wa
kata ya Machame Magharibi na Nasibu Mndeme (CCM) kata ya Mnadani.

Naye diwani mteule wa kata ya Weruweru, Salehe
Msingesi  alisema  ahadi alizozitoa kwenye mikutano yake ya
kampeni atahakikisha kuwa zinatekelezwa kwa uhakika ikiwemo kutatuankero ya
barabara ambazo kwenye hiyo kata hazipitiki msimu mzima wa mwaka kutokana na
uharibifu wake.

Kwa upande wake diwani mteule wa kata ya Mnadani Nasibu Mndeme
Akizungumzia utekelezaji wa ahadi alizotoa  diwani
mteule wa kata ya Machame Magharibi , Martini Munisi alisema ahadi alizotoa
atasimamia ili ziweze kufanikiwa kwa kushirikiana na uongozi wa halmashauri
pamoja na Chama chake ili kuweza kusogeza huduma kwa jamii kwa wakati.

“Natambua kuwa katika kata niliyochaguliwa kuna changamoto
nyingi sana ikiwemo ubovu wa miundombinu ya barabara  , shule zote za
msingi  zilizoko kwenye kata zinahitaji ukarabati wa majengo haswa
shule ya Msingi Kyeri ambayo jiko lake limeanguka na linahitaji ukarabati wa
haraka  ”alisema.








































Katika
uchaguzi mdogo uliofanyika Novemba 26 mwaka huu katika jimbo la Hai, CCM
iliweza kushinda kata zote tatu zilizokuwa zinafanya uchaguzi wa marudio 
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MADIWANI WA CCM WALIOSHINDA KATIKA UCHAGUZI JIMBO LA HAI WAKABIDHIWA VYETI
MADIWANI WA CCM WALIOSHINDA KATIKA UCHAGUZI JIMBO LA HAI WAKABIDHIWA VYETI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiu3xcHAOwyuQIe0pKQdy9obEKEvyLtGAwanZeMA4S9mdJ1q4G09mbR4bHnHRyIZ6Yt6R6aYcr0OBhuTvG-VDfPjS7Ys7PUV34dyZxDKBd9zfkcVi3jHEWNiqSYpnAVfo-QN20Pyk6YbOyE/s640/NAMBA+TATU.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiu3xcHAOwyuQIe0pKQdy9obEKEvyLtGAwanZeMA4S9mdJ1q4G09mbR4bHnHRyIZ6Yt6R6aYcr0OBhuTvG-VDfPjS7Ys7PUV34dyZxDKBd9zfkcVi3jHEWNiqSYpnAVfo-QN20Pyk6YbOyE/s72-c/NAMBA+TATU.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/11/madiwani-wa-ccm-walioshinda-katika.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/11/madiwani-wa-ccm-walioshinda-katika.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy