CCM MKOANI MBEYA YAMSHUKURU RAIS MAGUFULI KWA KUMTEUA MHE MWANJELWA KUWA NAIBU WAZIRI WA KILIMO
HomeSiasa

CCM MKOANI MBEYA YAMSHUKURU RAIS MAGUFULI KWA KUMTEUA MHE MWANJELWA KUWA NAIBU WAZIRI WA KILIMO

  Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa akisalimiana na wajumbe wa kamati ya siasa mara baada ya kuwasili kuwasalimu katika Ofi...

NEC YASISITIZA AMANI NA UTULIVU UCHAGUZI MDOGO WA MADIWANI KATIKA KATA 43
DC MJEMA AWAONGOZA VIJANA UVCCM WILAYA YA ILALA KUFANYA USAFI HOSPITALI YA MNAZI MMOJA DAR
SHAKA AONGOZA KIKAO CHA SEKRETARIET YA BARAZA KUU UVCCM TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM

 
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa akisalimiana na wajumbe wa kamati ya siasa mara baada ya kuwasili kuwasalimu katika Ofisi za Chama Cha Mapinduzi Mkoani Mbeya akiwa ziarani Mkoani humo, Jana Novemba 20, 2017. (Picha zote Na Mathias Canal)


Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa akizungumza na viongozi mbalimbali wa CCM Mkoa wa Mbeya mara baada ya kuwasili kuwasalimu katika Ofisi za Chama Cha Mapinduzi Mkoani Mbeya akiwa ziarani Mkoani humo, Jana Novemba 20, 2017.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisalimiana na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mbeya Ndg Wilson Nkambaku mara baada ya kuwasili kuwasalimu katika Ofisi za Chama Cha Mapinduzi Mkoani Mbeya akiwa ziarani Mkoani humo, Jana Novemba 20, 2017.


Na Mathias Canal, Mbeya

Chama Cha Mapinduzi Mkoani Mbeya kimemshukuru na kumpongeza Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa kumteua Mhe Mary Mwanjelwa kuwa Naibu Waziri wa Kilimo kuhudumu katika nafasi hiyo katika serikali ya awamu ya tano.

Pongezi hizo pamoja na shukrani zimetolewa na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mbeya Ndg Wilson Nkambaku kwa niaba ya wajumbe wa kamati ya siasa wakati akitoa taarifa ya chama hicho Ofisini kwake Mara baada ya Naibu Waziri kuzuru katika Ofisi hizo akiwa ziarani Mkoani Mbeya.

Nkambaku alisema kuwa Rais Magufuli amefanya uteuzi muhimu kwani Mhe Mwanjelwa ni mchapakazi na msaada mkubwa kwa chama hicho hivyo uteuzi huo umeonyesha Imani kwa Chama Cha Mapinduzi na Wananchi wa Mkoa mzima wa Mbeya.

Aidha alimsihi Kutenda haki na kufanya kazi kwa bidii huku CCM ikiahidi kutoa ushirikiano mwema Kwa Naibu Waziri wa Kilimo na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoani Mbeya.

Akizungumza na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake kwenye Ukumbi wa Ofisi za CCM Mkoa wa Mbeya Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa aliwasihi makada hao Kutofanya kazi za Chama kwa Mazoea badala yake kufanya kazi kwa weledi ili kuwasaidia wanachama na wasiokuwa wanachama wa CCM katika shughuli za maendeleo.

Naibu Waziri Huyo ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa (MNEC) amejivunia malezi bora na muhimu aliyoyapata ndani ya Chama Cha Mapinduzi huku akiwasihi viongozi kuongeza bidii katika kumsaidia Rais Magufuli kutimiza ndoto ya Tanzania Mpya kwa manufaa ya watanzania katika kuwaletea maendeleo.

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: CCM MKOANI MBEYA YAMSHUKURU RAIS MAGUFULI KWA KUMTEUA MHE MWANJELWA KUWA NAIBU WAZIRI WA KILIMO
CCM MKOANI MBEYA YAMSHUKURU RAIS MAGUFULI KWA KUMTEUA MHE MWANJELWA KUWA NAIBU WAZIRI WA KILIMO
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjeZYAo2F1twiv1KW87fyauLYKmK7Nm4N-Bn4PI5WpT4Rk3tXd8e9xkKmW2U4iIuCv8T8SWy0Fz1gVFcps1Xy_UAiNOYsLG5DnW-bXbRmqgvAS8j5cOyaGisxGdivPa3cqdKE0ojIwuAq5U/s640/IMG_2014.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjeZYAo2F1twiv1KW87fyauLYKmK7Nm4N-Bn4PI5WpT4Rk3tXd8e9xkKmW2U4iIuCv8T8SWy0Fz1gVFcps1Xy_UAiNOYsLG5DnW-bXbRmqgvAS8j5cOyaGisxGdivPa3cqdKE0ojIwuAq5U/s72-c/IMG_2014.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/11/ccm-mkoani-mbeya-yamshukuru-rais.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/11/ccm-mkoani-mbeya-yamshukuru-rais.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy