AIRTEL YAJA NA PROGRAMU MPYA YA U900 KUBORESHA HUDUMA ZA INTANETI

Meneja Uhusiano wa AIRTEL Tanzania Jackson Mmbando akizungumza na waandishi wa habari leo katika uzinduzi wa programu mpya ya  Airtel U900 ambao lengo lake kuu ni kuimarisha ubora wa mtandao na kutoa huduma bora kwa wateja wake mahali popote nchini. Mradi Tayari ushazinduliwa na kuwasha mitambo kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza na Arusha. Kushoto ni Meneja Ubora wa huduma za Mtandao Emmanuel Luanda
HomeJamii

AIRTEL YAJA NA PROGRAMU MPYA YA U900 KUBORESHA HUDUMA ZA INTANETI

• Teknolojia ya U900 kuwapatia watumiaji wa Airtel Intaneti yenye kasi  popote •Airtel yawekeza kwenye teknolojia mpya ya int...

WEEKLY BULLETIN, ISSUE NO.165
SERIKALI YAIPONGEZA BoT KWA KUELIMISHA WAANDISHI WA HABARI
TANZIA; MSIBA WA INNOCENT WAPALILA, KAKA WA MARIACONSOLATA NA HONEST WAPALILA




• Teknolojia ya U900 kuwapatia watumiaji wa Airtel Intaneti yenye kasi  popote
•Airtel yawekeza kwenye teknolojia mpya ya intaneti kutoa mtandao bora hata ukiwa ndani ya jengo.
 Airtel Tanzania Plc kampuni ya  mawasiliano iliyojikita katika huduma zenye ubunifu wa teknolojia zaidi nchini, leo katika muendelezo wake wa kutimiza dhamira yake ya kuwa mtandao bora zaidi imetangaza na kuzindua rasmi programu yake ya maboresho ya huduma za mtandao wake kupitia teknolojia ya iliyopewa jina la ‘Mradi wa U900’  ukiwa na lengo la kuimarisha ubora wa mtandao na kutoa huduma bora kwa wateja wake mahali popote nchini.
Mradi wa U900 ni uwekezaji mkubwa unaolenga kuhakikisha uhakika wa upatikanaji wa huduma ya 3G, ujazo wa data kamili pamoja na kuongeza kasi ya intaneti kwa kutumia teknolojia hii ya mawimbi ya mawasiliano ya masafa ya  900 Mhz. Teknolojia hii itaongeza upatikanaji wa mtandano wa 3G kwa Asilimia 50 zaidi pamoja kuongeza ubora wa upatikani wa intaneti bila kujali maeneo mteja alipo, Popote utapata Intaneti bora. 
Akiongea leo jijini Dar es Salaam wakati wa kutangaza huduma hiyo, Meneja Ubora wa huduma za Mtandao Airtel, Emanuel Luanda alisema kuwa Airtel imewekeza kwenye kuimarisha huduma ya mtandao kutokana na ongezeko la matumizi ya simu za smartphone na pia kutokana na uhitaji wa huduma mpya za ziada. Kutokana na uboreshaji wa mtandao wetu, wateja wote nchini watakuwa wakitapa huduma yenye kasi na hivyo kuwa na uhakika na huduma bora kutoka Airtel wakiwa popote. 
Bw, Luanda alidokeza “ripoti ya hivi karibuni ya TCRA inayotoa mchanganuo wa matumizi ya huduma za Intaneti (Data)  inaweka wazi kuweko kwa ongezeko la watumiaji wa huduma za intaneti kutokea 34% kwa mwaka 2015 na kupaa hadi 40% kwa mwaka 2016.  Hali hiyo ndio inatoa msukumo hata kwetu Airtel kuendelea kuwekeza zaidi katika teknolojia mpya  ili kuwapatia wateja wetu huduma bora zaidi”.
“Tayari tushafanya maboresho kwenye miji ya Dar es Salaam, Arusha na Mwanza huku maboresho mengine yakiendelea kufanyika Dodoma, Morogoro na miji mingene yenye uhataji mkubwa wa huduma zetu hapa Tanzania.” Alieleza Luanda

Kwa upande wake, Meneja wa Masoko Airtel Tanzania Arnold Madale alisema, “kwa kuwa Airtel tunatambua mahitaji ya wateja wetu, hali ya soko tumekuwa tukifanikiwa kuleta bidhaa zenye ubunifu  na mpangilio wa huduma zinazozingatia mahitaji ya mteja, hii ni hatua kubwa sana hasa kwenye ushindani wa biashara. Tunao  wateja ambao wanatumia mtandao wetu kwa ajili ya intaneti tu, lakini pia kuna wale wanaotumia kwa kupiga na kupokea simu, tunazo bidhaa na huduma ambazo zinakidhi matakwa ya wateja hao kwa muda wote wakiwa mahali popote. Kwa sasa hivi tunaendelea pia kuboresha huduma yetu ya 2G ili kutoa huduma yenye uhakika wa hali ya juu ikiwemo huduma ya Airtel Money ili kuendelea kuwafikia Watanzania wengi waishio pembezoni  huduma za kibenki na huku tukitimiza sera ya serikali ya kushiriki katika uboreshaji wa huduma bora za kifedha vijijini.”
“Tunapotangaza huduma hii muhimu ya kuboresha mtandao wetu, tunayo furaha kutangazia huduma ya Bando la OFA KABAMBE ambayo inapatika kwa urahisi na kumfanya mteja kuwa na Uhuru zaidi wa kutumia Intaneti  yenye kasi kwa muda mrefu zaidi kwa kuwasiliana na ndugu, marafiki  au wadau katika biashara mahali popote. Wateja wetu wataweza kufaidi huduma hii ya bando kwa kupiga *150*60#  na kujipatia 1GB, dakika150 kupiga mitandao yote na kudumu nazo kwa muda wa siku saba, aliongeza Madale.
‘Nia yetu ni kuendelea kukua kupita Maelezo huku tukitengeneza ujuzi wa kuaminiwa na wateja wetu kwa kuwa na gharama nafuu. Mradi wa U900 unadhihirisha kuwa Airtel imeamua kuinua taifa letu kufikia lengo la kuishi kidigitali kwa kuwepo na huduma za kidigitali, aliongeza Madale.



Meneja Ubora wa huduma za Mtandao wa Airtel Tanzania Emmanuel Luanda akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam baada ya kuzindua programu mpya ya Airtel U900 ambao lengo lake kuu ni kuimarisha ubora wa mtandao na kutoa huduma bora kwa wateja wake mahali popote nchini. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Jacksonn Mmbando. Teknolojia hii itaongeza upatikanaji wa mtandano wa 3G kwa Asilimia 50 zaidi pamoja na kuongeza ubora wa upatikaniji wa intaneti bila kujali maeneo mteja alipo.


a

Meneja Chapa na Masoko Airtel Tanzania Anorld Mandale akiongea wakati wa uzinduzi wa programu mpya ya  Airtel U900 ambao lengo lake kuu ni kuimarisha ubora wa mtandao na kutoa huduma bora kwa wateja wake mahali popote nchini. Kampuni hiyo pia huduma ya Bando la OFA KABAMBE ambapo wateja wataweza kufaidi huduma hii kwa kupiga *150*60#  na kujipatia 1GB, dakika150 kwa muda wa siku saba


Meneja Chapa na Masoko Airtel Tanzania Anorld Mandale akishika bango baada ya kuzindua huduma ya Bando la OFA KABAMBE ambapo wateja wataweza kufaidi huduma kwa kupiga *150*60#  na kujipatia 1GB, dakika150 kwa muda wa siku saba. Kulia ni Meneja Ubora wa huduma za Mtandao wa Airtel Tanzania Emmanuel Luanda na Meneja Uhusiano Airtel Tanzania, Jackson Mmbando




Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: AIRTEL YAJA NA PROGRAMU MPYA YA U900 KUBORESHA HUDUMA ZA INTANETI
AIRTEL YAJA NA PROGRAMU MPYA YA U900 KUBORESHA HUDUMA ZA INTANETI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEictJCH-G_n6yc-b2-gSAUMYeC_iwkXMM4j7kGH36ExWNdiO5XsX8dfWTRF5hjZGXE0LsT7UGz1XtTOpc_uT9ZfPq4hfMUMVp6uIpVM6YQcIzHBdVqBAD7dpwHykYZM2rEX12r9FSm3d-U/s640/_MGS3487.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEictJCH-G_n6yc-b2-gSAUMYeC_iwkXMM4j7kGH36ExWNdiO5XsX8dfWTRF5hjZGXE0LsT7UGz1XtTOpc_uT9ZfPq4hfMUMVp6uIpVM6YQcIzHBdVqBAD7dpwHykYZM2rEX12r9FSm3d-U/s72-c/_MGS3487.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/11/airtel-yaja-na-programu-mpya-ya-u900.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/11/airtel-yaja-na-programu-mpya-ya-u900.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy