WATUMISHI WA OFISI YA WAZIRI MKUU WAJENGEWA UWEZO KUKABILI MAAFA

Mkuu wa Huduma kwa Serikali kwa nchi za Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika kutoka Shirika la “Africa Risk Capacity” Bi. Lucy ...



Mkuu wa Huduma kwa Serikali kwa nchi za Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika kutoka Shirika la “Africa Risk Capacity” Bi. Lucy Nyirenda akifafanua jambo wakati wa Warsha ya Kugharamia Maafa na Matumizi ya Bima za Majanga iliyofanyika Mjini Dodoma kwa lengo la kutoa elimu kwa Watumishi wa Serikali juu ya masuala ya maafa.


Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Issa Nchasi akifungua Warsha ya siku moja kwa niaba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) iliyofanyika Oktoba 24, 2017 Dodoma Warsha hiyo iliandaliwa na Taasisi ya Africa Risk Capacity (ARC) iliyopo chini ya Umoja wa Afrika.

NA MWANDISHI WETU
WATUMISHI wa Ofisi ya Waziri Mkuu wameshiriki Warsha ya kujengewa uwezo kuhusu kugharamia maafa na matumizi ya Bima za majanga ili kutumia fursa zilizopo za kukabili maafa pindi yanapotokea kwa kushirikisha wadau mbalimbali  ikiwemo Taasisi zilizopo chini ya Umoja wa Afrika .
Akizungumza wakati wa Warsha hiyo iliyofanyika Oktoba 24, 2017 Mjini Dodoma kwa niaba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera na Bunge, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Bw. Issa Nchasi alisema kuwa warsha hiyo inalenga kutoa uelewa kuhusu utaratibu utaotumiwa na African Risk Capacity (ARC) ambayo ni Taasisi chini ya Umoja wa Afrika.
“Serikali imekuwa ikifanya kazi ya kuboresha mazingira ili kujenga uwezo wa kukabili madhara yatokanayo na maafa nchini” Alisisitiza Nchasi
Akifafanua amesema kuwa, warsha hiyo itasaidia watumishi wa Idara ya Uratibu wa Maafa kuwa na uwezo katika Menejimenti ya Maafa hali itayorahisisha Kujikinga, kukabili na kurejesha hali.
Washa hiyo ya siku moja imelenga kuwajengea uelewa Watumishi wa Ofisi hiyo kuhusu utaratibu unaotumiwa na Taasisi ya Africa Risk Capacity katika kuhudumia na kugharamia maafa na Bima za majanga.
Kuwawezesha Serikali kutambua maeneo ya ushirikianao katika huduma na kugharimia maafa na Bima za majanga.
Kwa upande wake Mkuu wa Huduma kwa Serikali kwa nchi za Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika kutoka Shirika la “Africa Risk Capacity” bi. Lucy Nyirenda amesema kuwa mpango huo uko chini ya nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) na takribani nchi 9 zimeshajiunga katika mfumo wa Bima za majanga.
“Takribani nchi 32 zimeshajengwewa uwezo kuhusu umuhimu wa kuwa na bima ya majanga ili kuimarusha uwezo wa kuyakabili pale yanapotokea kwa kushirikiana na wadau.” Alisisitiza Lucy
Akifafanua Lucy amesema kuwa, ni vyema nchi za Afrika zikaungana ili kuweza kuzuia majanga katika Bara la Afrika kwa kushirikishana mbinu mbalimbali zikiwemo fursa zinazoweza kusaidia kukabiliana na majanga hayo .
Warsha hiyo ya siku moja iliyoandaliwa na Taasisi ya Africa Risk Capacity (ARC ) iliyopo chini ya Umoja wa Afrika kwa kushirikiana na Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu imewashirikisha  Watumishi kutoka  Wizara za kisekta na Idara zinazojitegemea Takribani 42.



Meneja Kanda ya Kati Mamlaka ya BIMA Tanzania Bi. Stella Rutaguza akichangia hoja kuhusu umuhimu wa Bima za Majanga wakati wa Warsha ya siku moja juu ya Kugharamia Maafa na Matumizi ya Bima za Majanga iliyoandaliwa na Taasisi ya Africa Risk Capacity kushirikiana na Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu.



Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Issa Nchasi (wanne kulia) akiwa katika pichga ya pamoja na washiriki wa Warsha  hiyo mapema leo mjini Dodoma. (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU - DODOMA )

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WATUMISHI WA OFISI YA WAZIRI MKUU WAJENGEWA UWEZO KUKABILI MAAFA
WATUMISHI WA OFISI YA WAZIRI MKUU WAJENGEWA UWEZO KUKABILI MAAFA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgT3t7xz6Kq0F_iTlhQoqMcuKNxoMJ9qF-IWFcuH3WHH3tK9QEAmBlHUk-CadXMkAgc0PaBv2HMDAKsP4WxFhyphenhyphenGJN4TokYTA5zpejPIAjOsnWOhmi3p6SrsoKo6jRGTn-40Hqd2VUhg-HKl/s640/3.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgT3t7xz6Kq0F_iTlhQoqMcuKNxoMJ9qF-IWFcuH3WHH3tK9QEAmBlHUk-CadXMkAgc0PaBv2HMDAKsP4WxFhyphenhyphenGJN4TokYTA5zpejPIAjOsnWOhmi3p6SrsoKo6jRGTn-40Hqd2VUhg-HKl/s72-c/3.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/10/watumishi-wa-ofisi-ya-waziri-mkuu.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/10/watumishi-wa-ofisi-ya-waziri-mkuu.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy