WANAFUNZI 11,481 WAPATA MIKOPO AWAMU YA PILI 2017-2018
HomeJamii

WANAFUNZI 11,481 WAPATA MIKOPO AWAMU YA PILI 2017-2018

Alhamisi, Oktoba 26, 2017 Waombaji wa Mwaka wa Kwanza Kiasi cha shilingi bilioni  72.2  mpaka sasa kimetolewa kwa ajili ya ...

BALOZI WA CHINA NCHINI AMTEMBELEA SPIKA NDUGAI LEO WILAYANI KONGWA MKOANI DODOMA
SPIKA MSTAAFU ANNE MAKINDA AWAASA MADIWANI WANAWAKE WA JIJI LA DAR KUJITAMBUA KATIKA JAMII
UPDATES; MSIBA WA MBUNGE MSTAAFU WA JIMBO LA MOSHI MJINI PHILEMONI NDESAMBURO.


Alhamisi, Oktoba 26, 2017

Waombaji wa Mwaka wa Kwanza

Kiasi cha shilingi bilioni 72.2 mpaka sasa kimetolewa kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu wapatao 21,677 kati ya wanafunzi30,000 wa mwaka wa kwanza waliopangwa kupatiwa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 108.8 kwa mwaka wa masomo 2017/2018.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Bw. Abdul-Razaq Badru imesema kuwa idadi ya wanafunzi waliobaki wapatao 8,323 watapangiwa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 36.6 katika awamu inayofuata ili kukamilisha idadi iliyopangwa.



Idadi ya wanafunzi 21,677 waliokwishapangiwa mikopo na ambao wamedahiliwa katika vyuo mbalimbali vya elimu ya juu vinavyotambulika; ni asilimia 72.2 ya wanafunzi 30,000 wanaotarajiwa kunufaika na mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu kwa mwaka wa masomo2017/2018.

Orodha ya majina ya wanafunzi hao 21,677 inapatikana kwenye tovuti ya HESLB www.heslb.go.tz  na itatumwa kwenye vyuo husika kwa ajili ya hatua zaidi za kukamilisha malipo ya mikopo.

Wakati huo huo, Bodi imeendelea kutoa mikopo kwa ajili ya wanafunzi wanufaika wanaoendelea na masomo na ambao wamefaulu masomo yao ya mwaka wa masomo 2016/2017.

Jumla wanafunzi 54,936 wanaoendelea na masomo katika vyuo mbalimbali vya elimu ya juu wamepatiwa mikopo mpaka sasa na taarifa zao kuwasilishwa kwenye vyuo husika.

Bodi inatarajia kupanga na kutoa mikopo kwa wanafunzi 123,295 kwa mwaka wa masomo 2017/2018 wakiwemo wa mwaka wa kwanza30,000 na wanaoendelea na masomo wapatao 93,295.



Hitimisho
Bodi ya Mikopo inawasisitizia waombaji wa mikopo kuendelea kuwa na subira wakati ikikamilisha orodha inayofuata ya wanafunzi waliopata mikopo na itaendelea kutoa taarifa kwa vyombo vya habari na tovuti ya Bodi mara kwa mara.

Imetolewa na:
ABDUL-RAZAQ BADRU
MKURUGENZI MTENDAJI
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
ALHAMISI, OKTOBA 26, 2017
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WANAFUNZI 11,481 WAPATA MIKOPO AWAMU YA PILI 2017-2018
WANAFUNZI 11,481 WAPATA MIKOPO AWAMU YA PILI 2017-2018
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiSBvE0VfRMYwEmEhtjITJ55ImW9XELicrErc8ttzlCWulN2mb68o_RBKmHJ30o67PNoKDS7DkLHDzrtFo8oaS6NWVp7Cpeb807NMsl-72I6pM6dSss9eHDT9Ys5GzAM1O91yYCBbIdwv8/s400/CwGWTIEWEAASM7d.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiSBvE0VfRMYwEmEhtjITJ55ImW9XELicrErc8ttzlCWulN2mb68o_RBKmHJ30o67PNoKDS7DkLHDzrtFo8oaS6NWVp7Cpeb807NMsl-72I6pM6dSss9eHDT9Ys5GzAM1O91yYCBbIdwv8/s72-c/CwGWTIEWEAASM7d.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/10/wanafunzi-11481-wapata-mikopo-awamu-ya.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/10/wanafunzi-11481-wapata-mikopo-awamu-ya.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy