JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MADINI Telegramu "NISHATI". Barabaraya Kikuyu, Simu: + 255-2...
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MADINI
Telegramu "NISHATI". Barabaraya Kikuyu,
Simu: + 255-26 2322017 S. L. P. 422,
Nukushi :+255 26 2320148 40474DODOMA.
Baruapepe :ps@mem.go.tz
TAARIFA KWA UMMA
Wizara ya Madini inatoa taarifa kwa umma kuwa Mnada wa Madini ya Tanzanite uliokuwa ufanyike katika mji mdogo wa Mererani Wilayani Simanjiro mkoani Manyara kuanzia tarehe 12 hadi 15 Oktoba, 2017, umeahirishwa hadi hapo utakapotangazwa tena.
Sababu za kuahirishwa kwa mnada huo ni kuridhia maombi ya wadau wa mnada ambao waliomba kupata muda zaidi wa maandalizi ili wapate fursa ya kushiriki kwa wingi. Aidha, uongozi wa Wizara na Mkoa wa Manyara watapata muda zaidi wa kuandaa mazingira salama na bora zaidi ya kufanyia mnada huo katika mji wa Mererani.
Hivyo, Wizara ya Madini inawaomba radhi wadau wote wa Sekta hii ndogo ya madini ya vito hususan Tanzanite ambao wameathirika kwa namna moja au nyingine kutokana na kuahirishwa ghafla kwa mnada huu.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
13/10/2017
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
MINISTRY OF MINERALS
Telegrams: “ENERGY” Kikuyu Road,
Telephone:+255-26-2322024 P. O. Box 422,
Facsimile: +255-26-2322282 40474 DODOMA
PRESS RELEASE
The Ministry of Minerals regrets to inform the general public that the Tanzanite auction which was scheduled to be held at Mererani Town in Manyara Region from 12th - 15th October, 2017 has been postponed until further notice.
This auction has been postponed due to the stakeholders request to give them enough time to allow them to have ample time for preparations and hence increase the number of auction participants. During this period, the Ministry and Manyara Region authorities will concentrate on improving necessary infrastructure to enable the auction to be conducted in a secure and conducive environment.
Please, accept the apologies of the Ministry of Minerals all the stakeholders of the gemstone industry especially the Tanzanite sub sector who have been affected in any way by this untimely postponement. The Ministry values your participation and cooperation in making this auction most successful in our region.
Issued by:
Government Communication Unit
13/10/2017
COMMENTS