Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala (wa tano kushoto) akipokea karatasi yenye ...
Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis
Kigwangala (wa tano kushoto) akipokea karatasi yenye orodha ya Vifaa vya
kutolea huduma za Afya kutoka kwa Mbunge wa Kibaha Mjini, Silyvestry
Koka (kushoto kwake) wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa hivyo vyenye
thamani zaidi ya Sh. milioni 400 iliyofanyika kwenye Kituo cha Afya
Mkoani, mjini Kibaha, leo mchana. Kulia kwa Waziri ni MKuu wa Wilaya ya
Kibaha, Asumta Mshama. Picha Zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO).
Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis
Kigwangala, akikagua sehemu ya vifaa hivyo wakati akikabidhiwa na Mbunge
wa Kibaha Mjini, Silyvestry Koka (kulia kwake).

Mbunge
wa Kibaha mjini, Silyvestry Koka, akizungumza wakati wa hafla ya
kukabidhi Vifaa vya kutolea huduma za Afya, iliyofanyika kwenye Kituo
cha Afya cha Mkoani mjini Kibaha. Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Afya
Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala, Mkuu
wa Wilaya ya Kibaha Mjini, Asumta Mshama.
Akizungumza
katika hafla hiyo, Mbunge Koka, alisema kuwa alifanikiwa kupata msaada
wa vifaa hivyo kutoka kwa rafiki zake waishio nchini Marekani, wakati
alipokwenda katika shughuli zake za kibiashara, ambapo walimhakikishia
kupata vifaa hivyo kwa kuchangia gharama za usafirishaji hadi kuingia
nchini.
Baada
ya uhakika huo Koke alitumia gharama zake kuwasafirisha baadhi ya
wataalamu (Wazungu) kutoka nchini Marekani na kuja nchini hadi Mji wa
Kibaha kwa lengo la kukagua na kujiridhisha juu ya uhitaji wa vifaa
hivyo vya kutolea huduma za afya, ambapo alitumia jumla ya Sh. milioni
12.
Aidha
alisema kuwa vifaa hivyo vilichelewa kutokana na uhitaji kutoka mataifa
mengine yaliyokuwa yakipata matatizo na magonjwa ya mlipuko, na hivyo
kampuni hiyo ya Project Cure, kulazimika kughairisha kusafirisha kuja
nchini na kutoa kipaumbele kwa mataifa hayo yaliyokuwa yakipata matatizo
kwanza.
Mbali
na Mbunge kuchangia kiasi cha Sh. milioni 12, pia Halmashauri ya Mji wa
Kibaha pia ilichangia kiasi cha Sh milioni 32, zilizosaidia kusafirisha
vifaa hivyo kutoka nchini Marekani hadi kuwasili nchini. Vifaa hivyo
vilivyokabidhiwa hii leo vina thamani ya zaidi ya Sh. milioni 400.
Sehemu ya vifaa hivyo.
Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis
Kigwangala, Mbunge wa Kibaha Mjini, Silyvestry Koka, wakitoka kutembelea
katika Wodi ya Wazazi, katika Kituo cha Afya Mkoani, leo mchana wakati
alipofika kukabidhi Vifaa vya kutolea huduma za Afya vyenye thamani ya
zaidi ya Sh.milioni 400. 

NAIBU
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis
Kigwangala, (kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mfanyakazi wa Chumba
cha Maabala cha Kituo cha Afya Mkoani, Farida Chagulaga, wakati waziri
huyo alipotembelea chumba hicho na kukagua taratibu za ufanyaji kazi,
alipofika kwa ajili ya kukabidhi vifaa vya kutolea huduma za afya.
Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis
Kigwangala, (katikati) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mfanyakazi wa
Chumba cha Maabala cha Kituo cha Afya Mkoani, Farida Chagulaga, wakati
waziri huyo alipotembelea chumba hicho na kukagua taratibu za ufanyaji
kazi, alipofika kwa ajili ya kukabidhi vifaa vya kutolea huduma za afya.

Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis
Kigwangala (wa pili kushoto) Mbunge wa Kibaha Mjini, Silyvestry Koka
(kushoto kwake) Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Asumta Mshama (kushoto)
wakikabidhi karatasi ya orodha ya vifaa vya kuhudumia wagonjwa kwa
Madaktari wa Kituo cha Afya cha Mkoani mjini Kibaha, wakati wa hafla ya
makabidhiano ya vifaa hivyo vyenye thamani ya zaidi ya Sh. Milioni 400.
Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis
Kigwangala (wa tatu kulia) Mbunge wa Kibaha Mjini, Silyvestry Koka
(kulia kwake) Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Asumta Mshama (wa pili kulia) na
baadhi ya waganga wa Kituo cha Afya cha Mkoani Kibaha, wakikagua badhi
ya Vitanda vya wagonjwa, baada ya makabidhiano ya vifaa hivyo vya
kutolea huduma kwa wagonjwa vyenye thamani zaidi ya Sh. milioni 400.
Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye Kituo cha Afya Mkoani, mjini
Kibaha.
Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis
Kigwangala, akiimba wimbo maalumu kwa pamoja na Mkuu wa Wilaya Asumta
Mshama (kulia), Mbunge wa Kibaha mjini, Silyvestry Koka, alipokuwa
akizungumza na wananchi wa mji wa Kibaha, Wafanyakazi wa Kituo cha Afya
cha Mkoani (hawapo pichani) wakati wa hafla ya makabidhiano ya Vifaa vya
kutolea huduma za afya kituoni hapo
Dkt. Kigwangala, akizungumza wakati wa hafla hiyo.....
Baadhi ya wananchi wakimsangilia mgeni rasmi wakati akitoa hotuba yake katika hafla hiyo.
Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis
Kigwangala, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wananchi wa mji wa
Kibaha baada ya hafla hiyo.
Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis
Kigwangala, akiagana na baadhi ya wanachi waliohudhuria hafla hiyo.

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala, akiagana na Diwani Selina.
Wasanii wa Kikundi cha Malaika Dance, cha Kibaha wakitoa burudani katika hafla hiyo
COMMENTS