RC MAKONDA AOKOA BILLION 1.11 KUFUFUA MAGARI MENGINE YA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA YALIYOKUFA
HomeJamii

RC MAKONDA AOKOA BILLION 1.11 KUFUFUA MAGARI MENGINE YA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA YALIYOKUFA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo amekabidhi Mabasi 10 chakavu ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa kampuni ya Dar Coach kwa aj...

RAIS MAGUFULI AZINDUA KITUO CHA MAFUNZO MAALUM YA KIJESHI BAGAMOYO-PWANI
SSRA NA NIDA WANAENDELE NA ZOEZI LA UANDIKISHAJI WA VITAMBULISHO VYA TAIFA KWA WANACHAMA WA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII
DK. KIGWANGALLA AFANYA MAZUNGUMZO NA MUWAKILISHI WA BENKI YA DUNIA NCHINI KWA AJILI YA KUBORESHA MRADI WA REGROW


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo amekabidhi Mabasi 10 chakavu ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa kampuni ya Dar Coach kwa ajili kufufuliwa upya na kuwa ya kisasa.


Mabasi hayo 10 chakavu yanatoka kwenye Vyombo vya Ulinzi na Usalama ikiwemo Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ Magari 3, Jeshi la Polisi Magari 4 pamoja na Jeshi la Magereza Magari 3 ambapo yote kwa pamoja Matengenezo yake yameokoa kiasi cha Shilingi Billion 1,110,000,000 ya Serikali.


Makonda amesema kuwa Gari hizo zitatengenezwa na kukamilika ndani ya Siku 90 hadi 120 ambapo ameipongeza Kampuni ya Dar Coach kwa kujitolea kukarabati Magari hayo bila kutumia pesa ya Serikali. Aidha Makonda amesema Magari hayo yatafungwa Vifaa vya Kisasa ikiwemo Kiyoyozi (AC), Mfumo wa Chaji ya Simu kila Seat, Runinga, Radio, Viti vya kisasa, Vyoo vya Ndani, Bodi mpya pamoja na mwonekano mzima wa Gari ili ziwe za kisasa.


Amesema mpango wake wa kuendelea kuongezea nguvu Vyombo vya Ulinzi na Usalama hautokoma kwakuwa lengo lake ni kuwatumikia Wananchi na Askari wajivunie kufanyakazi chini ya Mkuu wa Mkoa mwenye kuwapenda na kuwajali.


Amemuagiza Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa kuhakikisha Ving'ora vya Jeshi la Polisi vinakuwa tofauti na kampuni za Ulinzi na Usalama, Magari ya Wagonjwa ili kupunguza Mkanganyiko kwa wananchi na kujengea heshima Jeshi la Polisi.


Makabidhiano hayo yameshuhudiwa na Viongozi wa Vyombo vya Ulinzi na usalama akiwemo Kamanda wa Polisi Dar es Salaam Lazaro Mambosasa, Mkurugenzi wa usafirishaji JWTZ Kanal RAajab Mwenyumbu, Mnadhimu wa Jeshi la Magereza ACP. Noel James ambapo wote kwa pamoja wamempongeza mkuu wa mkoa kwa hatua kubwa anayoifanya ya kuhakikisha wanafanya kazi katika mazingira mazuri.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akikaribishwa na viongozi wa jeshi wakati alipokwenda kukabidhi Mabasi 10 chakavu ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa kampuni ya Dar Coach kwa ajili kufufuliwa upya na kuwa ya kisasa.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akimkabidhi Mabasi 10 chakavu ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa Mkurugenzi wa kampuni ya Dar Coach kwa ajili kufufuliwa upya na kuwa ya kisasa wakishuhudiwa na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaviva,Kamanda wa Polisi Dar es Salaam Lazaro Mambosasa, Mkurugenzi wa usafirishaji JWTZ Kanal RAajab Mwenyumbu, Mnadhimu wa Jeshi la Magereza ACP. Noel James.



Mabasi 10 chakavu yakiwa yanatoka katika Chuo cha Polisi Kilwa Road kuelekea Mkuranga kwenye ofisi za Kampuni ya Dar Coach kwa ajili ya kufanyiwa marekebisho na kuwa ya kisasa zaidi. 

Mkuu wa Mkoa Paul Makonda akiwa ndani ya basi la Magereza. 





Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akiwa sambamba na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaviva, Kamanda wa Polisi Dar es Salaam Lazaro Mambosasa, Mkurugenzi wa usafirishaji JWTZ Kanal Raajab Mwenyumbu, Mnadhimu wa Jeshi la Magereza ACP. Noel James wakati wa kukagua mabasi 10 chakavu kabla ya kupelekewa kwenye gereji ya Dar Coach kwa ajili ya matengenezo. (Picha zote na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii)
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: RC MAKONDA AOKOA BILLION 1.11 KUFUFUA MAGARI MENGINE YA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA YALIYOKUFA
RC MAKONDA AOKOA BILLION 1.11 KUFUFUA MAGARI MENGINE YA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA YALIYOKUFA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEja3O_eL5y24GJ4ZqeF4dnEeZcYPD2fHfU-GRE6Gox8OFwP3K1d5tzdKEwrv3X4VeUxKh4EnrgEXSmEVxiLBZlvqNXqv0IwQ4h7sAKsOwPgp8JR_MZsb9KIXwE6tTwK-6DBsGfMWXyUQPo/s640/DSCF0467.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEja3O_eL5y24GJ4ZqeF4dnEeZcYPD2fHfU-GRE6Gox8OFwP3K1d5tzdKEwrv3X4VeUxKh4EnrgEXSmEVxiLBZlvqNXqv0IwQ4h7sAKsOwPgp8JR_MZsb9KIXwE6tTwK-6DBsGfMWXyUQPo/s72-c/DSCF0467.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/10/rc-makonda-aokoa-billion-111-kufufua.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/10/rc-makonda-aokoa-billion-111-kufufua.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy