Naibu Waziri wa Ujenzi, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Elias John Kwandikwa (kushoto) akifuatilia kwa makini majadilia...
Naibu Waziri wa Ujenzi, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Elias John Kwandikwa (kushoto) akifuatilia kwa makini majadiliano wakati wa kupokea maoni ya wadau mbele ya Kamati ya Bunge ya Miundombinu kuhusu Muswada wa Sheria ya Shirika la Mawasiliano Tanzania kwenye kikao kilichofanyika ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni, Dodoma. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Prof. Norman Sigalla King akifafanua jambo kwa wajumbe (hawapo pichani) wa Kamati hiyo
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania, Waziri Waziri Kindamba akifafanua jambo mbele ya Kamati ya Bunge ya Miundombinu kuhusu Muswada wa Sheria ya Shirika la Mawasiliano Tanzania kwenye kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni Dodoma
Naibu Katibu Mkuu wa Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Angelina Madete (aliyekaa) akifuatilia majadiliano ya wadau kuhusu Muswada wa Sheria ya Shirika la Mawasiliano Tanzania mbele ya Kamati ya Bunge ya Miundombinu kilichofanyika kwenye ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni Dodoma
COMMENTS