MFUMO WA ‘DROPWALL’ KUSAIDIA TAKWIMU MASHULENI
HomeJamii

MFUMO WA ‘DROPWALL’ KUSAIDIA TAKWIMU MASHULENI

Meneja Ufuatiliaji na Tathimini mradi wa Data kwa Maendeleo ya Jamii wa Tume ya Sayansi na Teknolojia, Dk. Geofrey Chambua akiongea mbe...

MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BANDARI TPA YAKAMATA BOTI ILIYOTUMIKA KUIBA MAFUTA BAHARINI
DKT. SHEIN AWAAPISHA VIONGOZI MBALIMBALI MJINI ZANZIBAR
WASHINDI WA AFYABANDO KWENYE DROO YA PILI WAPATIKA LEO



Meneja Ufuatiliaji na Tathimini mradi wa Data kwa Maendeleo ya Jamii wa Tume ya Sayansi na Teknolojia, Dk. Geofrey Chambua akiongea mbele ya wanahabari jijini Dar es Salaam wakati wakimtambulisha mfumo mpya wa kieletroniki wa ‘Dopwall’. Pembeni ni Mkurugenzi Mkuu Kampuni ya Eagle Analytics, Rose Funja ambao ni wasimamizi wa mfumo huo.
Mkurugenzi Mkuu Kampuni ya Eagle Analytics, Rose Funja ambao ni wasimamizi wa mfumo huo akifafanua machache mbele ya wanahabari jijini Dar es Salaam jinsi mfumo huo unavyofanyakazi. Pembeni ni Meneja Ufuatiliaji na Tathimini mradi wa Data kwa Maendeleo ya Jamii wa Tume ya Sayansi na Teknolojia, Dk. Geofrey Chambua.

Na Mwandishi Wetu - Dar es Salaam.

MFUMO mpya wa kieletroniki wa ‘Dopwall’ umezinduliwa nchini na unatajwa kuwa utasaidia kupunguza mdondoko wa elimu kwa wananchi wa kike nchini.

Licha ya hali hiyo pia inatajwa kuwa mdondoko wa wanafunzi kwa shule bado ni tatizo nchini ambapo kwa kipindi cha mwaka 2015 wanafunzi 61,488 waliripotiwa kuacha masomo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam juzi Mkurugenzi Mkuu Kampuni ya Eagle Analytics, Rose Funja, alisema kuzinduliwa kwa mfumo huo kusaidia wazazi na walezi kujua hali ya maendeleo ya shule wanasoma watoto wao ikiwemo kuwa na uwezo wa kuhoji kupitia vikao vya wazazi na bodi za shule.

“Serikali kupitia wizara mbalimbali ikiwemo Serikali za Mitaa wameboresha ukusanyaji wa taarifa mbalimbali za kielimu ambazo ni msingi wa mapambano dhidi ya mdondoko wa wanafunzi. Pamoja na jitihada hizo matumizi ya taarifa kama hizo katika kuboresha utendaji wa kila siku wa watumishi wa umma na ufanyaji wa maamuzi hayatoshelezi au hakuna kabisa katika idara za serikali,” alisema Funja

Kwa upande wake Meneja Ufuatiliaji na Tathimini mradi wa Data kwa Maendeleo ya Jamii wa Tume ya Sayansi na Teknolojia, Dk. Geofrey Chambua, alisema mfumo wa kieletroniki wa ‘Dropwall’ unalenga kuongeza matumizi ya taarifa zinazokusanywa na wadau mbalimbali ikiwemo serikali.

“Ubunifu wa mfumo huu umedhaminiwa na mradi wa Data fot Local Impact (DLI) ikiwa ni moja kati ya miradi mitatu ya takwimu inayosimamiwa na MCC pamoja na PEPFAR. Udhamini wa dli uliwesha uchunguzi wa mdondoko mashuleni katika wilaya za Mbeya na Nzega chini ya mwongozo wa TAMISEMI.

“Kampuni ya Eagle Analytics inayotengeneza mfumo wa Dropwall ni kampuni changa. Mhandisi Rose na timu yake kupitia ubunifu wao wa kubaini uwezekano wa mwanafunzi kuacha masomoni mmoja wa washindi 12 wa shindano la ubunifu lililoratibiwa na DLI ikishirikiana na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) mwaka 2016,” alisema Dk. Chambua.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MFUMO WA ‘DROPWALL’ KUSAIDIA TAKWIMU MASHULENI
MFUMO WA ‘DROPWALL’ KUSAIDIA TAKWIMU MASHULENI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh2igeM7CphoHXo4t1q-EUEJeY7oAQ_OFYKh8pGpfGVmKMJ6dqeBxI2mHVQ4CLmHP7CQia2QhQOWpMeUWvOVd-ySSEmBSEDFZLsP-_bdzt9ILn8vWuA-Vl1er2DiA148F4u5h4O9ZBBAcU/s640/IMG_1070.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh2igeM7CphoHXo4t1q-EUEJeY7oAQ_OFYKh8pGpfGVmKMJ6dqeBxI2mHVQ4CLmHP7CQia2QhQOWpMeUWvOVd-ySSEmBSEDFZLsP-_bdzt9ILn8vWuA-Vl1er2DiA148F4u5h4O9ZBBAcU/s72-c/IMG_1070.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/10/mfumo-wa-dropwall-kusaidia-takwimu.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/10/mfumo-wa-dropwall-kusaidia-takwimu.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy