JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA Simu ya Upepo: “ N G O M E ” Makao Makuu ya Jeshi, Simu ya Mdomo: 22150463 Sanduku...
JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
Simu ya Upepo: “N G O M E” Makao Makuu ya Jeshi,
Simu ya Mdomo: 22150463 Sanduku la Posta 9203,
Telex: 41051 Dar es Salaam,TANZANIA.
Fax: 2153426
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linasikitika kutangaza vifo vya Askari wake wawili Koplo Maselino Paschal Fabusi na Praiveti Venance Moses Chimboni, ambao walikuwa katika Ulinzi wa Amani nchini DRC.
Askari hao wamefariki baada ya kushambuliwa kwa kupigwa risasi na kundi la waasi tukio ambalo limetokea tarehe 09 Octoba 2017 umbali wa kilomita 24 mashariki mwa mji wa Beni. Majeshi yetu yamefanikiwa kuwarudisha nyuma waasi hao na kudhibiti eneo hilo.
Kufuatia shambulizi hilo Umoja wa Mataifa umeunda Bodi ya Uchunguzi kuchunguza tukio hilo. Aidha, Maafisa na Askari wa JWTZ wanaendelea kutekeleza majukumu yao katika Operesheni hiyo.
Umoja wa Mataifa unaandaa utaratibu wa kuleta miili ya marehemu nchini. Mtajulishwa taratibu za mapokezi, kuaga miili ya marehemu hao na mazishi.
Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi Amina.
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
10 Octoba, 2017
COMMENTS