UDHIBITI WA UBORA WA MAZAO SULUHISHO LA USALAMA WA CHAKULA
HomeJamii

UDHIBITI WA UBORA WA MAZAO SULUHISHO LA USALAMA WA CHAKULA

Na Ismail Ngayonga MAELEZO DAR ES SALAAM 13.9.2017 USALAMA wa ubora wa chakula na ulinzi wa afya za walaji ni miongoni mwa  masu...

DAWASCO YARAHISISHA HUDUMA KWA WATEJA WA MAJI, SASA KUUNGANISHWA KWA NJIA YA SIMU
WAFANYAKAZI JUMIA WAFANYA MATEMBEZI YA HISANI KUCHANGIA FEDHA KUSAIDIA JAMII
MAKAMU WA RAIS MHESHIMIWA SAMIA SULUHU HASSAN AWASILI MKOANI LINDIMAKAMU WA RAIS, MAMA SAMIA AWASILI MKOANI LINDI; KUFUNGA MAONESHO YA NANE NANE KUSHO AGOSTI 8

Na Ismail Ngayonga
MAELEZO
DAR ES SALAAM
13.9.2017

USALAMA wa ubora wa chakula na ulinzi wa afya za walaji ni miongoni mwa  masuala ya kimsingi yaliyopewa kipaumbele katika ngazi za  Kitaifa na Kimataifa kwa kuwa magonjwa yatokanayo na  Chakula yanaelezwa kuwa ni chanzo cha vifo vingi Duniani.

Milipuko ya magonjwa kama vile kipindupindu  na  homa  ya matumbo pamoja na vifo vitokanavyo na magonjwa hayo ni mambo ambayo yamekuwa yakiripotiwa kuiathiri jamii yetu katika suala la Usalama wa Chakula. 



Masuala ya Usalama na Ubora wa Chakula yana uhusiano wa moja kwa moja na Akiba ya Chakula,  hii ni kutokana na ukweli kwamba iwapo Chakula kitabainika kutokuwa salama na bora, itakuwa na madhara ya moja kwa moja kwa Akiba ya Chakula ya Taifa.

Hapa Nchini, zipo Taasisi zinazohusika na masuala ya Usalama na Ubora wa Chakula ikiwemo Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) na Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, ambazo zilianzishwa kwa ajili ya majukumu ya Kisheria ya kutoa huduma za Udhibiti wa Ubora wa Chakula na bidhaa nyingine.

Pamoja na kutambua umuhimu wa Usalama na Ubora wa Chakula na mahusiano yake katika suala zima la Chakula Nchini, ziko tetesi kwamba kwa sasa bado Wakulima nchini ambao ndio wazalishaji wakubwa wa Chakula hawajui wala hawajanufaika vya kutosha na jitihada za Kitaifa na za Taasisi husika katika Usalama na Ubora wa Chakula.

Kwa kutambua hivyo, Serikali ilianzisha Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP) ili kuhakikisha kuwa Wakulima wanaelimishwa kuhusiana na masuala ya Usalama na Ubora wa Chakula ili kuwasaidia Wananchi.

Akiwasilisha Hotuba ya Makadirio ya Bajeti ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2017/18, Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi anasema Wizara hiyo kwa kushirikana na Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Shirika la Kilimo na Chakula la Umoja wa Mataifa (FAO) na Halmashauri za Wilaya imetoa mafunzo kwa Maafisa Ugani 180 katika Wilaya za Kondoa, Chemba, Mufindi, Kilolo, Kilombero, Mbalizi na Mpwapwa kuhusu athari na mbinu za kudhibiti sumu kuvu.

Anasema Serikali pia imetoa elimu kwa wadau 837 kuhusu mbinu za udhibiti wa sumu kuvu kupitia maonesho ya Wakulima (NaneNane). Wadau hao ni Wakulima, Maafisa Ugani, Watafiti, Wakufunzi, Wanafunzi na Wafanyabiashara wa mikoa 14 ya Dodoma, Singida, Simiyu, Manyara, Kilimanjaro, Arusha, Kagera, Mbeya, Iringa, Dar Es Salaam, Shinyanga, Morogoro, Lindi na Mtwara.

Kwa mujibu wa Tizeba anasema Wizara yake pia imeendelea kufanya majaribio kwenye mashamba 100 ya Wakulima kwenye Halmashauri nane za Masasi, Nanyumbu, Babati, Kilosa, Kilombero, Mpwapwa, Kongwa na Chamwino kwa ajili ya kutathmini viwango vya Aflasafe kwenye udhibiti wa sumu kuvu.

“Wizara kwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Shirika la Kilimo na Chakula Duniani (FAO) na Halmashauri za Mwanza, Misungwi, Singida, Mufindi, Kilolo, na Kilosa imeendelea kutoa mafunzo rejea kwa Wawezeshaji (ToT) na Wakulima juu ya Udhibiti Husishi wa Visumbufu vya mimea na mazao” anasema Dkt Tizeba.

Dkt. Tizeba anasema Serikali pia imeendelea kudhibiti nzi waharibifu wa matunda kwa kutoa mafunzo na usambazaji wa kivutia wadudu aina ya Methyl eugenol (ME), ambapo kiasi cha lita 105 ziligawiwa katika Mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Mtwara, Pwani, Morogoro, kwenye Vituo vya Utafiti vya Kilimo vya Naliendele, Kibaha na Mikocheni.

Waziri Tizeba anasema Serikali imeendelea na ukaguzi wa usafi wa mimea na mazao katika vituo vya ukaguzi vya Sehemu ya Afya ya Mimea vilivyoko katika viwanja vya ndege, bandari na mipakani, ambapo hadi kufikia Mwezi Machi mwaka huu tani 776,379.16 za mimea na mazao zilikaguliwa na kusafirishwa nje ya nchi.

Aidha Dkt. Tizeba anasema Jumla ya tani 597,837.33 za mimea/mazao zilikaguliwa na kuingizwa nchini, vyeti 8,736 vya usafi wa mimea kwa ajili ya kusafirisha mazao nje ya nchi na vibali 1,232 vya kuingiza mazao na mimea nchini vilitolewa, ambapo jukumu hilo limewezesha biashara ya mazao ya Kilimo kukidhi mashariti ya Soko la Kikanda na Kimataifa.

Kwa mujibu wa Waziri Tizeba anasema Serikali pia iliendesha zoezi la ifuatiliaji, ukusanyaji na uratibu wa takwimu/taarifa za athari za viuatilifu vyenye sumu kali kwa afya ya binadamu na mazingira ulifanyika kwa wakulima 100 wa Wilaya ya Kilolo - Iringa.

“Pia zoezi la ukaguzi wa maduka ya pembejeo za Kilimo ulifanyika, ambapo lita 14,671 za viuatilifu visivyo na ubora vilikamatwa na kuhifadhiwa ili kusubiri taratibu za uteketezaji, hatua zilizochuliwa ni pamoja na kufunga baadhi ya maduka ya wafanyabiashara waliohusika na kuuza viuatilifu vilivyo chini ya ubora na ambavyo havijasajiliwa.

Akifafanua zaidi Waziri Tizeba anasema Serikali itaendelea kutoa elimu kwa wakulima ili kubaini milipuko na jinsi ya kudhibiti na itaendelea kuimarisha vituo vya ukaguzi vya mipakani ili kudhibiti mazao yanayosafirishwa na yanayoingia nchini pamoja na kuimarisha kituo cha kudhibiti milipuko cha KILIMO ANGA ili kutoa huduma bora ya udhibiti wa milipuko ya visumbufu vya magonjwa ya mazao na mimea.

Pamoja na utoshelevu wa chakula uliopo nchini kwa sasa, ni vyema kwa taasisi binafsi na mashirika ya kimataifa yakaendelea kutoa elimu kwa wakulima uhifadhi wa chakula hicho ni jambo linalopaswa kupewa kipaumbele kwa kuzingatia kuwa kuwa wakulima wengi wanamwaga mazao ya chakula kama mahindi chini kwa ajili ya kuyaanika na baadaye kuyafadhiwa.

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: UDHIBITI WA UBORA WA MAZAO SULUHISHO LA USALAMA WA CHAKULA
UDHIBITI WA UBORA WA MAZAO SULUHISHO LA USALAMA WA CHAKULA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg5od4KG7GKUJc53wk_otcn-oJuQ9_NbI3mWDN4FcOihzo0nY4uw2uXQEgsGl4v92TBtgtLtKDx1vgTxaTqIa2ICIBILDoeBLkRwlbyqhhYHxt-NPhS9IvGUYo7Jogjy3fvUtnf1VhAU3Q/s640/CHAKULA.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg5od4KG7GKUJc53wk_otcn-oJuQ9_NbI3mWDN4FcOihzo0nY4uw2uXQEgsGl4v92TBtgtLtKDx1vgTxaTqIa2ICIBILDoeBLkRwlbyqhhYHxt-NPhS9IvGUYo7Jogjy3fvUtnf1VhAU3Q/s72-c/CHAKULA.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/09/udhibiti-wa-ubora-wa-mazao-suluhisho-la.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/09/udhibiti-wa-ubora-wa-mazao-suluhisho-la.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy