TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA Kitalu Na. 8, Mtaa wa Luthuli S.L.P 2643, DAR ES SALAAM Simu: +255 22 2135747/8; 21371...
TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA
Kitalu Na. 8, Mtaa wa Luthuli
S.L.P 2643, DAR ES SALAAM
Simu: +255 22 2135747/8; 2137125; 2135222
Faksi: +255 22 2111281
Barua Pepe: chragg@chragg.go.tz
Tovuti: www.chragg.go.tz
|
Septemba 29,2017
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Salamu za pole kwa Jeshi la Polisi
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) inaungana na Watanzania kumpa pole Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Kamanda IGP, Simon Sirro kwa nyumba zaidi ya kumi (10) za Askari wa Jeshi la Polisi zilizopo kata ya Sekei, Mkoani Arusha kuteketea kwa moto.
Pia, Tume inatoa pole kwa familia zote za Askari wa Jeshi la Polisi walioathirika na tukio hilo la kusikitisha lililotokea usiku wa Septemba 27 kuamkia Septemba 28,2017, na inawaomba kuwa na subira katika wakati huu mgumu.
Tume inapenda kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuchukua hatua za haraka za kutoa kiasi cha Shilingi Milioni 260 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba mpya za askari walioathirika na tukio hilo.
Pia, inaupongeza uongozi wa Jeshi la Polisi kwa kuzisaidia familia zilizoathirika na kwa hatua za haraka inazochukua kuhakikisha familia hizo zinapata makazi mapya mapema.
Imetolewa na:
(SIGNED)
Mhe. Iddi Ramadhani Mapuri
Makamu Mwenyekiti
TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA
Septemba 29, 2017
COMMENTS