MAKONDA APOKEA MAGODORO 1,000 NA KUSEMA SASA HAKUNA MGONJWA KULALA CHINI MKOANI DAR ES SALAAM

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda amepokea Magodoro 1,000 yenye thamani ya Shillingi Million 100 kutoka kiwanda cha uten...





Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda amepokea Magodoro 1,000 yenye thamani ya Shillingi Million 100 kutoka kiwanda cha utengenezaji wa magodoro ya Dodoma asili kwa kushirikiana na wadau wanaopendezwa na kazi kubwa anayoifanya katika kutatua kero wananchi na kusema hakuna mgonjwa kulala chini mkoani Dar es Salaam.
Makonda amekabidhiwa magodoro hayo mjini Dodoma na uongozi wa kiwanda hicho mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Jordan Rugimbana.
Akizungumza baada ya makabidhiano hayo Makonda amesema, "Kwa kiasi hiki kikubwa cha magodoro tulichokabidhiwa napenda kusema, kuanzia sasa hakuna mgonjwa atakayelazwa chini kwenye mkoa wangu(Dar es Salaam)," Alisema Mhe. Makonda. Amesema kuwa Magodoro aliyopatiwa atayakabidhi kwenye Hospital zote za Mkoa wa Dar es Salaam kwakuwa baadhi zimekuwa na upungufu wa Magodoro hali inayofanya Wagonjwa kulala juu ya Vyuma vya kitanda na wengine kutandika Kanga na Nguo kwenye Sakafu. Amesema "idadi kubwa ya wananchi wamekuwa wakitoka mikoani kufuata huduma za Afya Dar es Salaam kutokana na wingi wa hospital za kisasa za umma na binafsi hivyo kusababisha hospital kuwa na wagonjwa wengi." Alisema.




Licha ya Changamoto hiyo Makonda amesema Sekta ya Afya jijini Dar es Salaam imeimarika kwa kiasi kikubwa ambapo lengo lake ni kuona Mkoa huo unakuwa kinara kwenye utoaji wa huduma Bora za Afya.
Ameshukuru Kiwanda hicho na Wadau waliomuunga Mkono na kuwasihi Wananchi kununua Magodoro ya Dodoma Asili yanayotengenezwa na Kiwanda cha Wazawa ili kukuza Uchumi wa Taifa.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Jordan Rugimbana amempongeza RC Makonda kwa kazi kubwa anayoifanya katika Sekta mbalimbali ikiwemo Maboresho ya Jeshi la Polis na kusema ataenda Dar es salaam kujifunza namna walivyofanikiwa kwenye Ulinzi na Usalama.

Nae Mkurugenzi wa Kiwanda cha Magodoro ya Dodoma Asili Bwana Haider Gulamali amesema wataendelea kutoa ushirikiano kwa RC Makonda kwakuwa kazi anayoifanya ni kubwa na inawagusa Wananchi wote hususani wanyonge.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MAKONDA APOKEA MAGODORO 1,000 NA KUSEMA SASA HAKUNA MGONJWA KULALA CHINI MKOANI DAR ES SALAAM
MAKONDA APOKEA MAGODORO 1,000 NA KUSEMA SASA HAKUNA MGONJWA KULALA CHINI MKOANI DAR ES SALAAM
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh3beWJbX5Wyk_UIZDgizmrqUZ9VDZCQkyzyXt9sMZwyVgs7eCzZYIOB2ADWkMiYOBuztr2xYMEnCadm1zYQgjmqBoGsHfQ2FA-6lxgODTRsglTQd0oCVoK6meJjJftgeCgeeJBRpI8xzg/s640/f396d6f4-771d-44bc-9f75-85c51ace5a89.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh3beWJbX5Wyk_UIZDgizmrqUZ9VDZCQkyzyXt9sMZwyVgs7eCzZYIOB2ADWkMiYOBuztr2xYMEnCadm1zYQgjmqBoGsHfQ2FA-6lxgODTRsglTQd0oCVoK6meJjJftgeCgeeJBRpI8xzg/s72-c/f396d6f4-771d-44bc-9f75-85c51ace5a89.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/09/makonda-apokea-magodoro-1000-na-kusema.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/09/makonda-apokea-magodoro-1000-na-kusema.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy