TIGO YAZINDUA DUKA KUBWA LA KISASA MJINI DODOMA

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Tanzania, Simon Karikari akikata utepe kuzindua duka jipya la kisasa lililofunguliwa mkoani Dodoma Agosti 1...


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Tanzania, Simon Karikari akikata utepe kuzindua duka jipya la kisasa lililofunguliwa mkoani Dodoma Agosti 1 2017. Wengine kutoka (kulia) ni Mkuu wa usimamizi na masuala ya kiserikali wa Tigo, Sylvia Balwire, Meneja usimamizi wa wateja wa Tigo Kanda Kaskazini, Vitalis Stephen na George Lugata mkurugenzi wa Tigo Kanda Kaskazini.


Meneja  usimamizi wa wateja wa Tigo Kanda Kaskazini, Vitalis Stephen akimuonesha Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Tanzania, Simon Karikari baadhi ya simu zinazouzwa kwenye duka jipya la kisasa lililozinduliwa mkoani Dodoma . Pembeni ni mkuu wa huduma kwa wateja wa Tigo Dodoma, Scolastica Kisori.


Mteja akipata huduma mara baada ya uzinduzi wa duka jipya la kisasa lililofunguliwa leo mkoani Dodoma,





Mteja akipata huduma mara baada ya uzinduzi wa duka jipya la kisasa lililofunguliwa mkoani Dodoma,
 Dodoma,  Agosti 1, 2017- Kampuni inayoongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali, Tigo Tanzania imeendelea kuishi kulingana na ahadi yake ya kuwapatia  wateja huduma wanazozifikia kwa urahisi zaidi kwa huduma za Tigo kwa kufungua duka la huduma kwa wateja ambalo ni jipya  lililofamnyiwa ukarabati  mkubwa   leo katikati ya jiji la Dodoma .
Akizungumza kwenye sherehe ya uzinduzi wa duka, Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Simon Karikari alisema duka iliyofanyiwa ukarabati ikiwa ni mkakati wa  upanuzi wa kampuni wa kuzileta bidhaa na huduma zake sehemu moja.
 Duka hilo jipya lililokarabatiwa miongoni mwa vitu vilivyomo ni pamoja na  sehemu ya watu mashuhuri (VIP) kwa ajili ya kuhudumia wateja ambao ni VIP na wale wanaohitaji huduma za ufuatiliaji wa  kasi, kaunta  zimeongezwa na eneo la  kufanyia majaribio  ambapo wateja wanaoingia wanaweza kufurahia uzoefu wa kwanza wa kujifunza jinsi ya kutumia bidhaa za Tigo kama vile simu za kisasa (smartphones) na bidhaa na huduma nyingine za mtindo wa maisha ya kidijitali kama vile  Tigo Pesa ambazo zinatolewa na kampuni. 
'Tigo imepania  kutumia  rasilimali zake zote ikatika  kuhakikisha kuwa wateja wetu wanapata huduma za daraja la juu  duniani, kuhakikisha ufanisi, wakati halisi wa majibu kwa maswali yao katika maduka yetu yote 52 ya huduma za wateja yaliyopo nchini, "alisema Karikari, na kuongeza  kuwa duka hilo  mpya Iimewekwa  vifaa vya kisasa, likihudumiwa na wafanyakazi waliopata mafunzo sawasawa na ambao ni wachapa kazi  ambao wako  tayari   kutoa huduma bora kwa idadi ya watu inayoongezeka kwa haraka jijini humo.
Akizungumza juu ya uendeshaji wake, Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini, George Lugata alisema kuwa duka hilo jipya la Tigo mpya litakuwa wazi siku zote saba za wiki.
"Kimkakati kuwepo kwa duka hilo eneo la katikati ya jiji kunafanya iwe rahisi kufikiwa na wakazi wa mji wa Dodoma, maeneo jirani  na watu wanaotembelea kitovu hicho cha nchi, " aliongeza Lugata.
Aliendelea kufafanua zaidi kuwa duka kubwa, la kisasa limekuwa pia linaenda bega kwa bega na mkakati wa Tigo kupeleka  huduma kwa  wateja kwa wakazi wa Dodoma kama mji ambao  unatarajia kuwa ‘ mlipuko’  wa idadi ya watu kufuatia uamuzi wa serikali kuhamishia shughuli zake za kiutawala  kutoka Dar es Salaam , na hivyo  kufanya mji wa Dodoma makao makuu ya nchi.
     
Duka lipo mkabala na mzunguko wa CDA kwenye sakafu ya chini ya Jengo la  CDA Barabara ya Uhindini katika Manispaa ya Dodoma,  na linatarajiwa kuhudumia  wateja zaidi ya 300 kwa siku.


COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: TIGO YAZINDUA DUKA KUBWA LA KISASA MJINI DODOMA
TIGO YAZINDUA DUKA KUBWA LA KISASA MJINI DODOMA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgThGfulOKISGgLXdOHgnqDY7X5HQAwGKDsHV2Bc1yJDwue_ArSbX7YlCSDCzmiFhkR3xVmTLWIkoF4AU75Ioakbod0NBVS6hxJp-WZ6RyYeE88y8c2NAfGiKLlYZtK9M0TJDVaWfF4F4Y/s640/Tigo%2527s+Head+of+Government+Relations+++and+Regulatory+Sylvia+Balwire%252C+Customer+Operations+Manager+North-+Vitalis+++Stephen%252C+Acting+MD+Simon+Karikari%252C+Zonal+Director+-+North+George+++Lugata.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgThGfulOKISGgLXdOHgnqDY7X5HQAwGKDsHV2Bc1yJDwue_ArSbX7YlCSDCzmiFhkR3xVmTLWIkoF4AU75Ioakbod0NBVS6hxJp-WZ6RyYeE88y8c2NAfGiKLlYZtK9M0TJDVaWfF4F4Y/s72-c/Tigo%2527s+Head+of+Government+Relations+++and+Regulatory+Sylvia+Balwire%252C+Customer+Operations+Manager+North-+Vitalis+++Stephen%252C+Acting+MD+Simon+Karikari%252C+Zonal+Director+-+North+George+++Lugata.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/08/tigo-yazindua-duka-kubwa-la-kisasa.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/tigo-yazindua-duka-kubwa-la-kisasa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy