MWELEKEO WA MVUA KWA KIPINDI CHA OKTOBA - DISEMBA 2014 NCHINI THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA MINISTRY OF TRANSPORT TAN...
MWELEKEO WA MVUA KWA KIPINDI CHA OKTOBA - DISEMBA 2014
NCHINI
THE UNITED REPUBLIC
OF TANZANIA
MINISTRY OF TRANSPORT
TANZANIA
METEOROLOGICAL AGENCY
|
Telex: 41442 HEWA
Telephone: 255 (0) 22
2460718
Telefax: 255 (0) 22 2460735 P.O. BOX 3056
E-mail: met@meteo.go.tz DAR ES SALAAM.
http//www.meteo.go.tz
Our ref: TMA/1622 4th
September 2014
PRESS RELEASE
CLIMATE OUTLOOK FOR TANZANIA OCTOBER – DECEMBER, 2014 RAINFALL SEASON
A: Introduction
This statement gives a review of rainfall
performance for March to May, 2014 and an outlook for October to December, 2014
short rain season (Vuli) in the
country.
Highlights for October –December, 2014
|
![https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhEcBlMY0PM_Otte6ra0uVIhXm74cEoAeXu84RRy_ptZC3D751ETK95xZ-GSm0TYNNpk2GKrLnOmGvqm0OSaNbGpQMu9uO-mbxc3GmzXuLBaTuvcRGEaFOCBsByLeKYs7_N2Yk_S5EeGKIW/s1600/1.jpg](file:///C:\Users\OKANDA\AppData\Local\Temp\msohtmlclip1\01\clip_image004.gif)
![http://engaresero.org/images/livestock.jpg](file:///C:\Users\OKANDA\AppData\Local\Temp\msohtmlclip1\01\clip_image006.gif)
![http://api.ning.com/files/4mbmBJabTg2Dp-NK-XftxATkJfMATwyRmLehO0NpX8emNPNV4k71kcIjIkxv5iMDsalVgZOfQIwlyOrLN2hcoZa09RG9*zGF/maf.jpeg](file:///C:\Users\OKANDA\AppData\Local\Temp\msohtmlclip1\01\clip_image008.gif)
![](file:///C:\Users\OKANDA\AppData\Local\Temp\msohtmlclip1\01\clip_image010.gif)
B: REVIEW OF RAINFALL PERFORMANCE
During the long rain season of
March to May (MAM) 2014, most
parts of the country experienced normal to above normal rainfall with pockets
of below normal rainfall over parts of Mwanza, Singida and Dodoma regions. The occurrence
of Tropical Cyclone ‘‘HELLEN’’ in Mozambique channel over South Western Indian
Ocean contributed to enhanced rainfall over Northern Coast areas.
Lake
Victoria Basin: Bukoba and Musoma stations received above normal
rainfall. Shinyanga station received normal rainfall while Mwanza station received
below normal rainfall.
North-Eastern
Highland: Station of Arusha, Lyamungo and Kilimanjaro
recorded above normal rainfall while Same and Moshi normal rainfall.
Northern
Coast and Unguja and Pemba Islands: Dar es Salaam, Morogoro and Pemba stations reported
above normal rainfall while Unguja (Zanzibar, Amani, Kizimbani), and Tanga statins
received normal rainfall.
South-Western
Highland: Mbeya, Mahenge and Tukuyu stations recorded above normal rainfall while
Sumbawanga station received normal rainfall.
Western: Station of Kigoma received above normal rainfall
while Tabora and Kibondo recorded normal rainfall.
Southern Coast: Kilwa station received above normal while
Mtwara received normal rainfall.
Central: Station of Hombolo recorded normal rainfall while
Singida and Dodoma below normal rainfall.
Southern
region: Songea station measured above
normal rainfall.
C: CLIMATE SYSTEMS OUTLOOK
During October to December, 2014 rainfall season, anomalous warming
over Western and South- Western Indian Ocean coupled with neutral SSTs over
Eastern Indian Ocean (Indonesia) are likely to enhance easterly to north easterly
wind flow. Expected cooling over Atlantic Ocean, is likely to support moist westerly
wind flow from Congo Basin. Slightly warming over Central Equatorial Pacific is
likely to persist during the October to December, 2014 rainfall season and
contribute to enhanced rainfall over bimodal areas. Moreover, warming across
much of the South-western Indian Ocean during the month of November and
December, 2014 is likely to trigger occurrence of tropical cyclones.
D: SEASONAL
RAINFALL OUTLOOK:
Expected climate systems for October to December, 2014 rainfall season
is likely to feature as follows:
(i) Short Rainfall Season (Vuli) over
Bimodal areas
The October to December, 2014 rainfall season (Vuli) is more
significant for the northeastern highlands, northern coast areas, Lake Victoria
Basin and northern Kigoma. The rains are expected to be normal to above normal
over the northern coast (Dar es Salaam, Northern Morogoro, Coast regions,
including Unguja and Pemba isles), Northeastern Highlands (Kilimanjaro, Arusha and
Manyara regions) and Lake Victoria Basin (Kagera, Geita, Mara, Mwanza, Simiyu, and
Shinyanga).
The onset of the short rainfall season (Vuli) is expected to commence
in September, 2014 over Lake Victoria Basin and gradually spreading to other
areas. However, early onset of the rains is likely over areas in the Northern coast
(Mainly over Dar es Salaam, Pwani and Tanga including Unguja and Pemba Isles).
Lake Victoria Basin: (Kagera,
Mara, Mwanza, Geita, Simiyu and Shinyanga regions):
Rains are expected to start during the first and second week of September,
2014 over Kagera, and northern Kigoma and then gradually spreading to Mwanza,
Geita, Shinyanga, Mara and Simiyu regions. The rains are expected to be above
normal over Kagera, Geita, Mwanza, Mara, Simiyu and northern Kigoma regions
while over Shinyanga region, rains are expected to be normal to above normal.
Northern coast areas and
hinterlands: (Dar es Salaam, Tanga, and Coast regions, extreme northern
Morogoro areas and Isles of Unguja and Pemba): Rains are expected to commence in the first week
of September. The rains are likely to be normal to above normal over most
areas.
North-eastern highlands:
(Kilimanjaro, Arusha and Manyara regions): Rains are expected to commence in the second to third week of
September, 2014 and are likely to be above normal over much of Kilimanjaro, Arusha
and northern part of Manyara regions. However, southern parts of Manyara region
are likely to experience normal to above normal rains.
(ii) Seasonal Rainfall (November to April) over Unimodal areas:
November to April rainfall season is more significant for the western,
central, southwestern highlands, southern region and southern coast. Rains are
likely to be normal to above normal over most areas during the months of
November to December 2014.
Western areas: (Tabora, Rukwa,
Katavi and Kigoma regions):
Rains are expected to start in the second week of November, 2014 The
rains are expected to be above normal over southern part of Kigoma, Rukwa and Katavi
regions while much parts of Tabora region rains are expected to be normal to
above normal.
Central (Singida and Dodoma
regions):
Rains will commence on the third week of November, 2014 and are
expected to be normal to above normal over much of Singida and Dodoma regions.
Southwestern highlands: (Mbeya,
Iringa, and Njombe regions and southern Morogoro areas):
Rains over these regions are expected to start during the first to
second week of November, 2014. The rains are expected to be normal to above
normal over most areas while the western parts of Mbeya region are expected to
experience above normal rains.
Southern region and Southern
Coast: (Ruvuma, Mtwara and Lindi regions):
Rains are expected to start during the first to second week of
November, 2014 and are expected to be normal to above normal over most areas.
However, pockets of below normal rains are expected over Ruvuma region.
![](file:///C:\Users\OKANDA\AppData\Local\Temp\msohtmlclip1\01\clip_image012.jpg)
![](file:///C:\Users\OKANDA\AppData\Local\Temp\msohtmlclip1\01\clip_image014.jpg)
Figure 1 – Rainfall Normal Maps – left: Average
rainfall for October to December; right: Outlook for the coming rainfall season
October-December 2014
It
should be noted that although events of heavy and short duration of rainfall
are likely to be more frequent in areas with above normal rains they are also common
even in normal to below normal rainfall conditions. Development of tropical cyclones over the
southwest Indian Ocean is likely to influence rainfall patterns in the country.
Areas in which rainfall is likely to be more influenced by Cyclones includes
Central, South-Western highlands, Western areas and Coastal areas.
E: LIKELY IMPACTS AND ADVISORY
Normal and above normal rainfall
conditions are expected over much of the country with exception of southern
region which is likely to feature normal to below normal rainfall. The
associated impacts on social-ecomic sectors and their respective advisories are
highlighted as follows:
Agriculture and food Security
Sufficient soil moisture levels are likely to favor normal cropping
season over much of the country except for southern sector of the country
(mainly Ruvuma region) where periods of reduced rainfall are expected mainly
during crop establishment. Excessive soil moisture levels associated with above
normal rainfall are likely to favor weeds and impede crop development, thus high
use of agricultural inputs is likely to raise production costs. Farmers are
advised to prepare their farms and acquire agricultural inputs early enough while
making appropriate land use management and right choice of crop varieties to
plant.
Pasture and Water for Livestock
and wildlife
Pasture and
water availability for livestock and wildlife over much of the country is
likely to be good. However, famers are encouraged to produce and stock animal
feeds for use during the dry season. Due to high likelihood of disease outbreak,
regular dipping and vaccination against pests and diseases are highly
recommended. Wildlife-human conflicts due to wildlife migration and
agricultural activities are likely to be minimal during the season.
Natural
Resources and Tourism
Natural resources management Authority
and Tourism Sector are encouraged to protect infrastacture such as roads and
bridges against damage from the expected torrential and above normal rains in the
National Parks and Game Reserve areas. Hunters, Photographic tourism visitors
and tour operators are advised to be aware of floods of rivers due to the
expected rainfall.
River flow discharges and water levels in dams are expected to improve
from their current levels over much of the country. In spite of the expected
normal and above normal rains, water should be used sparingly. Water harvesting
and storage practices are recommended.
Local Authorities
Water
drainage systems should be opened and cleaned to avoid water accumulation due
to surface runoff as floods cause destruction of infrastructures, loss of lives
and property.
Health sector
There
is a likelihood of water borne diseases outbreaks due to stagnant waters and uncontrolled
sewerages. Relevant Authorities and individuals are advised to take appropriate
health measures need to minimize the expected negative health impacts.
Disaster Management
The disaster management authorities and other stakeholders are advised
to take necessary measures such as good practice of environmental conservations
and ensure preparedness, response, and mitigation plan to reduce any negative
impacts that may result from the expected above normal rainfall.
Media
The media is advised to obtain, make regular follow-ups and disseminate
weather and climate information and warning as provided by Tanzania Meteorological
Agency (TMA). Moreover, Media is encouraged to seek and obtain inputs from
relevant sectors when preparing and relaying cross cutting issue on Weather and
Climate to the Public.
NB: The current status of seasonal forecasting allows for
prediction of spatial and temporal averages and may not fully account for
physical and dynamical factors that influence short term national climate
variability. Users of this outlook are,
therefore urged to make good use of daily, ten day and monthly updates issued
by the Tanzania Meteorological Agency.
Tanzania Meteorological Agency
will continue to monitor developments of the systems and issue updates.
Dr. Agnes L. Kijazi
DIRECTOR GENERAL
************************
JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA UCHUKUZI
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
|
Simu ya mdomo: 255 22 2460
735/2460 706-8
Nukushi: 255 22 2460 735/700 S.L.P.
3056
Tovuti: www.meteo.go.tz
Unapojibu
tafadhali nakili:
Kumb.
Na.: TMA/1622 4
Septemba, 2014
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MWELEKEO WA MVUA KWA KIPINDI CHA OKTOBA - DISEMBA 2014
NCHINI
A: UTANGULIZI
Taarifa hii inatoa tathmini ya mvua za masika
(Machi - Mei) 2014 na mwelekeo wa mifumo ya hali ya hewa na mvua kwa
kipindi cha mwezi Oktoba hadi Disemba, 2014(Vuli).
|
![https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhEcBlMY0PM_Otte6ra0uVIhXm74cEoAeXu84RRy_ptZC3D751ETK95xZ-GSm0TYNNpk2GKrLnOmGvqm0OSaNbGpQMu9uO-mbxc3GmzXuLBaTuvcRGEaFOCBsByLeKYs7_N2Yk_S5EeGKIW/s1600/1.jpg](file:///C:\Users\OKANDA\AppData\Local\Temp\msohtmlclip1\01\clip_image004.gif)
![http://engaresero.org/images/livestock.jpg](file:///C:\Users\OKANDA\AppData\Local\Temp\msohtmlclip1\01\clip_image006.gif)
![http://api.ning.com/files/4mbmBJabTg2Dp-NK-XftxATkJfMATwyRmLehO0NpX8emNPNV4k71kcIjIkxv5iMDsalVgZOfQIwlyOrLN2hcoZa09RG9*zGF/maf.jpeg](file:///C:\Users\OKANDA\AppData\Local\Temp\msohtmlclip1\01\clip_image008.gif)
![](file:///C:\Users\OKANDA\AppData\Local\Temp\msohtmlclip1\01\clip_image010.gif)
B: TATHMINI
YA MVUA KIPINDI CHA MACHI – MEI, 2014
Katika msimu uliopita wa mvua za Masika Machi hadi
Mei, 2014. Maeneo mengi ya nchi yalipata mvua za wastani hadi juu ya wastani
isipokuwa maeneo machache ya mikoa ya Mwanza, Singida na Dodoma ambayo yalipata
mvua za chini ya wastani. Matukio ya vimbunga hususan Kimbunga ‘Hellen’ kilichotokea
katika Rasi ya Msumbiji kusini magharibi mwa baharĆ ya Hindi kilisababisha
ongezeko la mvua katika eneo la Pwani ya kaskazini.
Maeneo
yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka:
Kanda ya Ziwa
Victoria: Viwango vya mvua vilivyopimwa katika vituo vya Bukoba na Musoma vilikuwa juu ya wastani. Kituo
cha Shinyanga kilipima mvua kiwango cha wastani wakati katika kituo cha Mwanza kiwango
cha mvua kilikuwa chini ya wastani.
Nyanda za juu
kaskazini mashariki: Vituo vya Arusha, Lyamungo na Kilimanjaro vilipima mvua
juu ya wastani ilihali vituo vya Moshi na Same kiwango cha mvua kilikuwa cha
wastani.
Pwani ya kaskazini
na visiwa vya Unguja na Pemba: Vituo vya Dar es Salaam, Morogoro na Pemba vilipima mvua za
juu ya wastani na vituo vya Zanzibar, Amani, Kizimbani pamoja na Tanga mvua zilikuwa
wastani.
Maeneo
yanayopata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka:
Nyanda
za juu kusini magharibi: Vituo vya Mbeya, Tukuyu, na Mahenge vilipima mvua
juu ya wastani na kituo cha Sumbawanga kiwango cha mvua kilikuwa cha wastani.
Kanda ya magharibi: Mvua juu ya wastani ilipimwa katika kituo cha Kigoma
ilihali vituo vya Kibondo na Tabora mvua zilikuwa ni za wastani.
Pwani ya kusini: Kituo cha Kilwa kilipima mvua juu ya wastani na vituo
vya Mtwara pamoja na Naliendele mvua
zilikuwa za wastani.
Kanda ya kati: Vituo vya Singida na Dodoma vilipima mvua
chini ya wastani na kituo cha Hombolo mvua za wastani.
Kanda
ya kusini: Kituo cha Songea kiwango cha mvua kilichopimwa kilikuwa juu ya wastani.
C: MIFUMO YA HALI YA HEWA
Katika kipindi cha miezi ya Oktoba hadi Disemba, 2014 hali ya joto la
bahari katika maeneo ya magharibi na kusini -magharibi mwa bahari ya Hindi inatarajiwa
kuwa juu ya wastani, upande wa mashariki mwa bahari ya Hindi hali ya joto la wastani inatarajiwa. Hali hii
inatarajiwa kusababisha upepo wenye unyevunyevu kutoka bahari ya Hindi kuelekea katika eneo la
Pwani ya Africa Mashariki. Aidha, hali
ya joto la chini ya wastani katika eneo la mashariki mwa bahari ya Atlantiki
(Pwani ya Angola) inatarajiwa kusababisha ongezeko la hewa yenye unyevunyevu
kutoka katika misitu ya Kongo kuelekea katika maeneo ya magharibi na kusini
Magharibi mwa nchi.
Hali ya joto la juu ya wastani katika eneo la Tropikali ya bahari ya
Pasifiki linatarajiwa kuendelea kwa kipindi cha miezi ya Oktoba hadi Disemba,
2014. Hali hiyo inatarajiwa kuchangia ongezeko la mvua katika baadhi ya maeneo
yanayopata misimu miwili ya mvua. Hali ya joto la juu ya wastani katika eneo la
kusini magharibi mwa Bahari ya Hindi linaashiria kuwepo kwa matukio ya vimbunga
katika msimu wa mvua za Vuli kuanzia mwezi Novemba, 2014.
D: MWELEKEO WA MVUA OKTOBA - DISEMBA 2014:
Kutokana na mwelekeo wa mifumo ya hali ya hewa inayotarajiwa, mvua za
kipindi cha Oktoba hadi Disemba, 2014 zinatarajiwa kuwa kama ifuatavyo:
(i)
Mvua za Vuli (kwa maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua)
Msimu wa mvua wa Oktoba hadi Disemba (Vuli) ni mahususi katika maeneo
ya nyanda za juu kaskazini mashariki, pwani ya kaskazini, kanda ya Ziwa Viktoria
na kaskazini mwa mkoa wa Kigoma.
Katika msimu huu mvua zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani
katika maeneo ya pwani ya kaskazini (mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Tanga,
kaskazini mwa mkoa wa Morogoro, pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba), nyanda
za juu kaskazini mashariki (mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara) pamoja na mikoa
ya Mwanza, Geita, Simiyu, Shinyanga na kaskazini mwa mkoa wa Kigoma.
Msimu wa mvua za Vuli
unatarajiwa kuanza mwezi Septemba, 2014 katika ukanda wa Ziwa Viktoria na
kusambaa katika maeneo mengine. Hata hivyo, mvua hizo zinatarajiwa kuanza
mapema katika maeneo ya ukanda wa pwani (Mkoa wa Tanga na kisiwa cha Pemba) na
katika baadhi ya maeneo ya nyanda za juu kaskazini Mashariki.
Kanda ya Ziwa Victoria: (Mikoa
ya Kagera, Mara, Mwanza, Geita, Simiyu na Shinyanga): Mvua zinatarajiwa kuanza katika wiki ya
kwanza na ya pili ya mwezi Septemba, 2014 katika mkoa wa Kagera na kaskazini
mwa mkoa wa Kigoma na kuendelea kusambaa katika mikoa ya Mwanza, Geita, Shinyanga, Simiyu na Mara. Mvua hizo zinatarajiwa
kuwa za juu ya wastani katika maeneo ya mikoa ya Kagera, Geita, Mara, Mwanza
pamoja na kaskazini mwa mkoa wa Kigoma. Maeneo mengi ya mkoa wa Shinyanga
yanatarajiwa kuwa na mvua za wastani hadi juu ya wastani.
Ukanda wa Pwani ya Kaskazini:
(Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani, Morogoro-kaskazini pamoja na Visiwa vya
Unguja na Pemba):
Mvua zinatarajiwa kuanza wiki ya kwanza ya mwezi Septemba, 2014 katika
maeneo ya mikoa ya Tanga, Dar es Salaam pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba na
kusambaa maeneo ya mkoa wa Morogoro. Mvua
hizi zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo mengi.
Nyanda za juu Kaskazini
Mashariki: (Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara):
Mvua katika maeneo haya zinatarajiwa kuanza wiki ya pili na ya tatu ya
mwezi Septemba, 2014 na zinatarajiwa kuwa juu ya wastani katika maeneo mengi ya
mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na kaskazini mwa mkoa wa Manyara. Hata hivyo,
kusini mwa mkoa wa Manyara, mvua zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya
wastani.
(ii) Mvua za Msimu (Novemba – Aprili) kwa maeneo yanayopata msimu mmoja wa
mvua.
Msimu wa mvua za Novemba hadi Aprili ni mahususi kwa maeneo ya
Magharibi mwa nchi, kanda ya kati, nyanda za juu kusini-magharibi, kusini
mwa nchi na pwani ya kusini. Katika kipindi cha Oktoba hadi Disemba, 2014
maeneo mengi yanatarajiwa kupata mvua za wastani hadi juu ya wastani.
Kanda ya Magharibi (Mikoa ya
Kigoma, Tabora, Katavi na Rukwa):
Mvua zinatarajiwa kuanza wiki ya pili ya mwezi Novemba, 2014. Mvua hizi
zinatarajiwa kuwa za juu ya wastani katika maeneo ya mikoa ya Rukwa, Katavi
pamoja na kusini mwa mkoa wa Kigoma. Hata hivyo, maeneo mengi ya mkoa wa Tabora
yanatarajiwa kuwa na mvua za wastani hadi juu ya wastani.
Kanda ya kati (Mikoa ya Singida
na Dodoma):
Mvua zinatarajiwa kuanza wiki ya tatu ya mwezi Novemba, 2014 na
zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani.
Nyanda za juu Kusini Magharibi:
(Mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe na kusini mwa Morogoro):
Mvua zinatarajiwa kuanza wiki ya kwanza na ya pili ya mwezi Novemba,
2014 na zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo mengi.
Maeneo ya magharibi mwa mkoa wa Mbeya, mvua zinatarajiwa kuwa juu ya wastani.
Maeneo ya kusini na pwani ya
kusini (mikoa ya Ruvuma, Lindi na Mtwara)
Mvua zinatarajiwa kuanza wiki ya kwanza na ya pili ya mwezi Novemba,
2014 na zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani isipokuwa maeneo mengi
ya mkoa wa Ruvuma, yanatarajiwa kuwa na mvua za wastani hadi chini ya wastani
katika baadhi ya maeneo.
![](file:///C:\Users\OKANDA\AppData\Local\Temp\msohtmlclip1\01\clip_image012.jpg)
![](file:///C:\Users\OKANDA\AppData\Local\Temp\msohtmlclip1\01\clip_image014.jpg)
Kielelezo: 1 – Ramani ikionesha Mvua – kushoto: Wastani wa mvua Mwezi Oktoba hadi Disemba;
Kulia: Mwelekeo wa Mvua katika msimu huu wa Oktoba hadi Disemba 2104.
Izingatiwe
kuwa pamoja na kuwapo kwa uwezekano wa matukio mengi ya mvua kubwa katika
maeneo yanayotarajiwa kupata mvua juu ya wastani, hali hiyo pia inaweza
kujitokeza katika maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za wastani hadi chini ya
wastani.
Matukio ya Vimbunga katika eneo
la kusini magharibi mwa Bahari ya Hindi yanatarajiwa kuchangia katika mwenendo
wa mvua nchini. Maeneo ambayo hali ya mvua inaweza kuathiriwa zaidi na vimbunga
ni pamoja na kanda ya kati, Nyanda za juu Kusini Magharibi, Magharibi mwa nchi
na maeneo ya ukanda wa Pwani.
E: ATHARI
NA USHAURI
Maeneo mengi ya nchi yanatarajiwa kupata mvua za wastani hadi juu ya
wastani isipokua baadhi ya maeneo ya kusini mwa nchi yanayotarajiwa kupata mvua
za wastani hadi chini ya wastani. Matarajio ya mvua hizo pamoja na ushauri kwa
baadhi ya sekta za kiuchumi na kijamii zimeainishwa kama ifuatavyo;
Kilimo na Usalama wa Chakula
Katika maeneo mengi ya nchi hali
ya unyevunyevu wa udongo inatarajiwa
kuwa ya kutosheleza shughuli za kilimo. Hata hivyo, kwa maeneo machache ya
kusini mwa nchi (hususan Mkoa wa Ruvuma) vipindi vya upungufu wa mvua
vinatarajiwa mwanzoni mwa msimu na hivyo kuathiri kiwango cha unyevunyevu wa
udongo. Hali ya unyevunyevu wa udongo kupita kiasi inayoambatana na vipindi vya
mvua kubwa inaweza kusababisha ongezeko
la magugu, matumizi makubwa ya pembejeo, hivyo kuongeza gharama za uzalishaji.
Wakulima wanashauriwa kuandaa mashamba
na pembejeo mapema pamoja na kuzingatia
ushauri wa wataalam wa kilimo kwa matumizi sahihi ya ardhi na mbegu.
Malisho na maji kwa ajili ya mifugo na wanyama pori
Hali ya malisho na upatikanaji wa maji
kwa ajili ya mifugo na wanyama pori inatarajiwa kuwa nzuri katika maeneo mengi
nchini. Hata hivyo, wafugaji
wanashauriwa kuzalisha malisho na kuyahifadhi kwa matumizi wakati wa kiangazi. Aidha,
wafugaji wanashauriwa kufuata maelekezo ya wataalam wa ugani katika maeneo yao hususan
matumizi ya maji na malisho na
kukabiliana na magonjwa ya mlipuko
yanayoweza kujitokeza. Kutokana na hali ya mvua inayotarajiwa, matukio ya migogoro
inayosababishwa na mifugo, wanyamapori
na shughuli za binadamu na kilimo hayatarajiwi kujitokeza kwa kiasi kikubwa.
Maliasili na
Utalii
Mamlaka za usimamizi wa shughuli za
utalii na hifadhi za wanyamapori zina shauriwa kuchukua hatua stahiki katika kuzuia
uharibifu wa miundombinu kama barabara
na madaraja ndani ya hifadhi dhidi ya adhari za mvua kubwa na za juu ya wastani
katika maeneo husika. Aidha, wawindaji,
wapiga picha za kitalii na makampuni ya kitalii yanashauriwa kuchukua tahadhari
ya uwepo wa mafuriko kutokana na mvua zinazotarajiwa.
Maji na Nishati
Mtiririko wa maji katika mito na vina vya maji katika mabwawa
vinatarajiwa kuongezeka katika maeneo mengi ya nchi kutokana na mvua za msimu
wa Vuli. Pamoja na matarajio ya
kuwepo kwa mvua za juu ya wastani inashauriwa kuwa maji yatumike kwa uangalifu
na kuzingatia taratibu za uvunaji, uhifadhi na matumizi endelevu ya rasilimali
maji.
Mamlaka za Miji
Inashauriwa kuchukua hatua za kuhakikisha kuwa mifumo na njia za
kupitisha maji zinafanyakazi katika kiwango cha kutosha kuhimili mvua
zinazotarajiwa ili kuepusha maji kutuama na kusababisha mafuriko na uharibifu
wa miundombinu, upotevu wa maisha na mali katika maeneo husika.
Sekta ya Afya
Ushauri unatolewa kwa jamii na sekta husika kuchukua hatua stahiki
katika kuzuia milipuko ya magonjwa
yanayosababishwa na kutuama kwa maji na
utiririshaji wa maji taka usiodhibitiwa katika maeneo yao.
Menejimenti ya Maafa
Mamlaka za maafa na wadau wengine wanashauriwa kuchukua hatua stahiki katika
utunzaji wa mazingira, upatikanaji wa maji safi na salama, na usambazaji wa
madawa, maji na chakula ikiwa ni hatua za kujiandaa na kukabiliana na majanga
yanayoweza kutokea kutokana na vipindi vya mvua kubwa na mvua za juu ya wastani
zinazotarajiwa.
Vyombo vya habari
Vyombo vya habari vinashauriwa kufuatilia, kupata na kusambaza taarifa
sahihi za mienendo ya hali ya hewa kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania
(TMA) na kutumia wataalam wa sekta husika katika kuandaa na kufikisha taarifa
za masuala mtambuka ya hali ya hewa kwa jamii. Aidha, jamii nayo inashauriwa
kufuatilia na kuzingatia taarifa sahihi za hali ya hewa na mirejeo yake kupitia
vyombo vya habari.
Angalizo: Mwelekeo wa mvua uliotolewa
hapa umezingatia zaidi kipindi cha msimu (miezi mitatu) na hali ya mvua katika
maeneo makubwa. Hivyo, viashiria vinavyochangia mwenendo wa mifumo ya mvua na
mabadiliko ya muda mfupi katika maeneo madogo utazingatiwa katika uchambuzi wa utabiri wa muda wa kati na
mfupi. Watumiaji wa taarifa za utabiri huu wanashauriwa pia kufuatilia tabiri za
saa 24, siku 10 pamoja na wa mwezi kama zinavyotolewa na Mamlaka ya hali ya
Hewa Tanzania.
Mamlaka
ya Hali ya Hewa Tanzania Itaendelea kufuatilia mwenendo wa mifumo ya hali ya
hewa na kutoa taarifa za mwelekeo wa mvua nchini.
Dkt. Agnes L. Kijazi
MKURUGENZI MKUU
COMMENTS