MULTCHOICE YATANGAZA NEEMA KWA WATEJA WA DStv
Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania Maharage Chande akitangaza punguzo kubwa la bei kwa vifurushi vyote vya DStv bei zitakazoanza kutumika rasi Septemba mosi 2017.
HomeJamii

MULTCHOICE YATANGAZA NEEMA KWA WATEJA WA DStv

Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania Maharage Chande akitangaza punguzo kubwa la bei kwa vifurushi vyote vya DStv bei zitakazoan...

RC MAKONDA AKABIDHIWA MAGARI 26 YA JESHI LA POLISI DAR ES SALAAM KWA AJILI YA KUYATENGENEZA
TANESCO YATAHADHARISHA WANAOOMBA AJIRA DHIDI YA MATAPELI
TAMKO LA SERIKALI JUU YA MATUMIZI YA PICHA ZA MARAIS WASTAAFU MAGAZETINI NA MITANDAONI KUHUSIANA NA SAKATA LA USAFIRISHAJI WA MCHANGA WA MADINI NJE YA NCHI



Balozi Maalum wa DStv Nancy Sumary akiongea wakati wa hafla hiyo Dar es Salaam Agosti 29 2017.


MultiChoice Yatangaza Neema kwa wateja wa DStv!
Yafyeka bei za vifurushi vyote! Wapenzi wa Kandanda ‘meno nje’
PANGA LA BEI LAFYEKA;  DStv Premium kwa 8.15%, DStv Compact Plus kwa 11.02%, DStv Compact kwa 16.11%, DStv Family kwa 9.09% and DStv Access (Bomba) kwa 4.88%

Dar es Salaam Jumanne Agosti 29,2017; Katika kuhakikisha kuwa wateja wake wote na watanzania kwa ujumla wanaendelea kufurahia huduma za DStv, kampuni ya Multichoice Tanzania imetangaza neema kubwa kwa wateja wake kwa kufyeka bei za vifurushi vyake vyote, huku pia ikiboresha maudhui na vipindi katika vifurushi vyake hususan vile vya bei ya chini!

Habari hiyo njema imetangazwa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania Maharage Chande, alipokuwa akiongea na waandishi wa habari katika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam ambapo amesema bei hizo mpya zitaanza kutumika rasmi Septemba mosi 2017.

“Kumjali na kumsikiliza mteja ni nguzo ya uendeshaji wa biashara yetu. Tumesikia maoni ya wateja wetu na wananchi kwa ujumla kutusihi tuangalie uwezekano wa kupunguza bei, tumechanganua kwa kina na tumeamua kutekeleza matakwa yao, leo hii tumepitisha panga kwenye bei za vifurushi vyetu vyote!” alisema Maharage.

Akifafanua kuhusu punguzo hilo, Maharage amesema  kumekuwa na punguzo la hadi asilimia 16, ambalo ni punguzo kubwa sana na litakalowapa ahueni kubwa watumiaji wa DStv. Amezitaja bei mpya kuwa ni;





Bei Mpya za vifurushi vya DStv:
Kifurushi
Bei ya sasa
Bei Mpya
% Ya Punguzo
Premium
TZS 184 000.00
TZS 169 000.00
8.15%
Compact Plus
TZS 122 500.00
TZS 109 000.00
11.02%
Compact
TZS 82 250.00
TZS 69 000.00
16.11%
Family
TZS 42 900.00
TZS 39 000.00
9.09%
Access (Bomba)
TZS 19.975.00
TZS 19 000.00
4.88%

Mara baada ya kutaja bei hizo Maharage aliwaambia waandishi wa habari; “Kwa lugha ya mtaani wanasema ‘Vuma Vimekaza’ – ikimaanisha hali ya kifedha imebana… Multichoice imelisikia hilo na kuamua kuwapa wateja wote wa DSrv ahueni kubwa! Sasa kwa wateja wetu wa DStv, ‘Vyuma vimeachia’”

Maharage amesisitiza kuwa Multichoice itaendelea kuwasikiliza wateja wake na kuhakikisha kuwa inatekeleza kile wanachohitaji wateja wake pale inapowezekana.

“Wateja wetu walituomba tuongeze maudhui ya kitanzania kwenye king’amuzi chetu, tukawasikia, tukaweka chanel maalum kabisa ya Maisha Magic Bongo ambayo ina asilimia 100 ya maudhui ya Kitanzania; wakatuomba tupunguze bei ya vifurushi, tukafanya hivyo mwishoni mwa mwaka jana, na leo tena kwa mara ya pili tumepunguza bei, wakatuomba tuongeze chanel kwenye vifurushi vya bei ndogo, tukafanya hivyo, tukaleta Laliga na Ligi kuu ya uingereza hadi kwenye kifurushi cha chini kabisa cha Bomba”.

“Kipekee kabisa Wananchi kupitia serikali wakatuomba tuongeze nguvu kwenye kuinua vipaji vya vijana wetu wa kitanzania, tukasikia, tukaitikia, tukaanza katika riadha ambapo tumemdhamini mwanariadha wetu Alphonce Simbu. Sote tunajua matokeo yake, sasa Tanzania inahofiwa kwenye ulingo wa riadha kimataifa! Haya yote tumefanya kwa sababu tunawasikiliza wateja wetu, tunawasikiliza wadau wetu, tunawasikiliza Watanzania” alisema Maharage.

Wakati habari hii ikiwa ni njema kwa watanzania wote, washabiki na wanazi wa kandanda wameonekana kufurahia Zaidi kwani kwa punguzo hilo kuwa wataweza kushuhudia ligi kuu ya uingereza PL pamaja na ligi nyingine kubwa ulimwenguni na makombe maarufu kama UEFA kwa bei nafuu zaidi.

Kwa maelezo Zaidi kuhusu bei mpya na vipindi mbalimbali katika vifurushi vya DStv tembelea; www.dstv.com.


Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MULTCHOICE YATANGAZA NEEMA KWA WATEJA WA DStv
MULTCHOICE YATANGAZA NEEMA KWA WATEJA WA DStv
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh7lqkZN8UwopaMrlfnPm2E0d-YSYDwceh_jPB6D4N_IxQ3PrRBZEhp_ytoxEfmV_BMug8Zm3n0UAYP-wVSvWHq7hmev1r3DwlkakNcZ38BSOQ5tL5V-yzxZbKG_2xkCD73XiwCJYSw7Ks/s640/1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh7lqkZN8UwopaMrlfnPm2E0d-YSYDwceh_jPB6D4N_IxQ3PrRBZEhp_ytoxEfmV_BMug8Zm3n0UAYP-wVSvWHq7hmev1r3DwlkakNcZ38BSOQ5tL5V-yzxZbKG_2xkCD73XiwCJYSw7Ks/s72-c/1.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/08/multchoice-yatangaza-neema-kwa-wateja.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/multchoice-yatangaza-neema-kwa-wateja.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy