JKCI KUENDELEA KUPOKEA MADKTARI KUTOKA CHINA.

HomeJamii

JKCI KUENDELEA KUPOKEA MADKTARI KUTOKA CHINA.

Na Agness Moshi na Bushiri Matenda-MAELEZO. Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) inatarajia kupokea madaktari wengine wanne kutoka ...

RAIS MAGUFULI AWASILISHA FOMU ZAKE ZA TAMKO LA RASILIMALI NA MADENI KWA VIONGOZI WA UMMA KATIKA OFISI ZA SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA
HALI YA USALAMA BARABARANI YAIMARIKA:KAMANDA MUSILIMU
MAVUNDE AJIBU KERO ZA WANANCHI WA HOMBOLO

Na Agness Moshi na Bushiri Matenda-MAELEZO.
Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) inatarajia kupokea madaktari wengine wanne kutoka China kwa ajili ya kuendelea kusaidiana na madaktari wazawa katika taasisi hiyo baada ya madaktari wengine wanne kutoka China kumaliza muda wao.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Dkt. Peter Kisenge katika hafla ya kuwaaga madaktari wanne kutoka China waliomaliza muda wao wa utumishi hapa nchini ambao walikua wakishirikiana naTaasisi hiyo kwa takribani miaka miwili.  
“Wanarudi nchini China baada ya kumaliza muda wao, Tunawashukuru kwa kushirikiana nasi kwa kipindi chote walichokua nasi tunaishukuru Serikali ya China kwa misaada mbalimbali wanayotupatia ikiwemo ujenzi wa jengo la Taasisi ya Moyo, madaktari,wataalam pamoja na vifaa tiba”, alisema Dkt. Kisenge.
Dkt. Kisenge aliongeza kuwa hivi karibuni Taasisi inatarajia kupokea madaktari wengine wanne kutoka China kwa ajili ya kuendelea kushirikiana nao   katika utoaji huduma ili kuweza kuifanya Taasisi hiyo ya kimataifa.
Naye Kiongozi wa timu ya Madaktari kutoka China kwa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Sun Long amesema kwa miaka miwili waliyofanya kazi na Taasisi hiyo wamefanikiwa kufanya oparesheni  takribani 373 jambo ambalo limesaidia kupunguza  gharama za matibabu na idadi ya wagonjwa wa Moyo kwenda kutibiwa nje ya Nchi kama vile India.
“Sasa hakuna haja ya kutumia fedha nyingi kwa ajili ya matibabu ya Moyo, Matibabu yote yanapatikana katika taasisi hii, hakuna Matata, Hapakazi Tu”, alisisitiza Dkt. Long.
Aidha, Dkt.Long amesema kuna haja ya nchi hizi mbili kuendelea kushirikiana ili kuendelea kusaidiana katika utoaji huduma ikiwa ni pamoja na kubadilishana wataalam ili kukuza uwezo katika utoaji huduma.
Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi wa jopo la madaktari waliomaliza muda wao Dkt. Gu Zhigiang ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kujitegemea katika matibabu ya magonjwa ya Moyo kwa wananchi wake na ameshukuru ushirikiano walioupata kutoka kwa taasisi hiyo kwa kipindi chote walichofanya kazi hapa nchini.
“Ninamshuru kila mmoja na ninafurahi kuhudumia Nchi hii nzuri, ninatumaini tutaendelea kushirikiana zaidi”, alisema Dkt. Gu Zhigiang.
Dkt. Gu Zhigiang ameongeza kuwa anatarajia kukua kwa ushirikiano baina ya nchi hizi mbili kwani tunaelekea kuadhimisha miaka 50 ya ushirikiano kati ya Serikali ya China na Tanzania.
 








Kiongozi wa timu ya Madaktari kutoka China kwa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Sun Long akibadilisha nmawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Profesa Mohamed Janabi baada ya kutembelea taasisi hiyo jijini Dar es Salaam leo.

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: JKCI KUENDELEA KUPOKEA MADKTARI KUTOKA CHINA.
JKCI KUENDELEA KUPOKEA MADKTARI KUTOKA CHINA.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEinFFZDaHoTUxcM_oANx9NhggwP8pCd1mcY_faf7ShwUwDnu-0hoFt8d_ED63URQaEMt2yugwwLLUo9sNJLDjS7q57WZ-pMZP4yNJ1XhDQBv1BG82WMPYS2gmN6kPJaht74dq-bMD7Dj0Y/s640/JKC1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEinFFZDaHoTUxcM_oANx9NhggwP8pCd1mcY_faf7ShwUwDnu-0hoFt8d_ED63URQaEMt2yugwwLLUo9sNJLDjS7q57WZ-pMZP4yNJ1XhDQBv1BG82WMPYS2gmN6kPJaht74dq-bMD7Dj0Y/s72-c/JKC1.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/08/jkci-kuendelea-kupokea-madktari-kutoka.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/jkci-kuendelea-kupokea-madktari-kutoka.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy