BALOZI WA CHINA AFIKA OFISINI KWA SPIKA NDUGAI KUMUAGA
HomeJamii

BALOZI WA CHINA AFIKA OFISINI KWA SPIKA NDUGAI KUMUAGA

Na Lawrence Raphaely - Bunge.   Balozi wa China nchini LU Youqing amefika Ofisini kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ...

DKT. MWIGULU AAGIZA WANAOPANGA MIPANGO YA MAANDAMANO WAKAMATWE
WANAWAKE WA BAM INTERNATIONAL WAPIGWA MSASA WALIPOADHIMISHA SIKUKUU YA KIMATAIFA YA MWANAMKE DUNIANI
ECOBANK TANZANIA KUFADHILI WANANFUNZI WA SHULE ZA SERIKALI


BALOZI WA CHINA AFIKA OFISINI KWA SPIKA NDUGAI KUMUAGA


Na Lawrence Raphaely - Bunge.
 

Balozi wa China nchini LU Youqing amefika Ofisini kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai  Jijini Dar es Salaam mapema leo kumuaga baada ya muda wake wa kukaa Tanzania kwisha.

Akizungumza na Spika Ndugai, Balozi huyo alisema kuwa muda wake wa kutumikia kama Balozi wa China hapa nchini umekwisha hivyo hana budi kuondoka ingawa angetamani kuendelea kubaki.Balozi huyo aliongeza kuwa amefurahi kuona kuwa katika kipindi chake chote akiwa hapa nchini uhusiano baina ya Tanzania na China umezidi kukua.

“Ninafuraha kubwa wakati ninaporejea China kuona kuwa uhusiano wetu wa kihistoria umezidi kukua na kwamba kuna ongezeko kubwa la uwekezaji wa China hapa Tanzania na pia tumesaidia katika utekelezaji wa miradi mingi,” alieleza Balozi huyo.

Balozi huyo ambaye amesema kuwa Tanzania ni nchi yake ya mwisho kuhudumu kama Balozi aliongeza kuwa kwa sasa anarejea nchini China na akiwa huko ataendelea kujitikita katika shughuli za kudumisha uhusiano baina ya Tanzania na China.

“Tanzania ndiyo nchi yangu ya mwisho  kuhudumu kama Balozi na nitakaporejea nyumbani (China) nitaendelea kufanya shughuli nyingine ambazo zinalenga kuimarisha uhusiano baina ya Tanzania na China,”  alisema Balozi Youqing.

Kutokana na hilo Balozi Youqing alisema kuwa ingawa  anarejea nchini China lakini yupo tayari kwa Tanzania kuendelea kumtumia kama Balozi wake katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali zitakozosaidia katika kudumisha ushirikiano baina wa nchi zote mbili.

“Nipo tayari kwa Tanzania kuendelea kunitumia kama Balozi wake aliyepo Nchini China, ninawakaribisha kwa mikono yote miwili tuendelee kufanya kazi kwa pamoja,” alisema Balozi huyo.

Kwa upande wake Spika Ndugai alimshukuru  Balozi huyo kwa kazi kubwa ambayo ameifanya akiwa hapa nchini na kumueleza kuwa daima Watanzania wataendelea kumkumbuka kwa kazi nzuri aliyoifanya.

“Mimi binafsi katika kipindi chako ukiwa kama Balozi nimeshuhudia ongezeko kubwa la watanzania wengi tena wa hali ya chini wakisaifiri kwenda China kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kibiashara,” alisema Spika Ndugai na kuonegeza kuwa; kupitia fursa hiyo Watanzania wengi wameweza kujiajiri kupitia biashara ya kununua bidhaa toka China na kuja kuuza hapa nchini.

Mhe Spika pia alimshukuru Balozi Youqing kwa uchakapakazi wake katika kuwezesha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kupitia wataalamu kutoka nchini China.

“Unaondoka lakini utakapojisikia kurudi, sisi kama Bunge na Serikali kwa ujumla tupo tayari kukupokea kwa mikono miwili na kuendelea kufanya kazi na wewe,” alisema Spika Ndugai.

Mbali na hayo Spika Ndugai pia alimuomba Balozi Youqing kuendelea kuwa Balozi wa Tanzania atakaporejea nchini China kwa kuendelea kufanya shughuli ambazo zitasaidia katika kuimarisha ushirikiano baina ya pande zote mbili.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai akizungumza na Balozi wa China nchini, Dkt. Lu Youqing  anayemaliza muda wake alipofika kumuaga  mapema leo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa masuala ya  Diplomasia na Vyombo ya Habari- Ubalozi wa China Bi. Wang Fang.
Balozi wa China nchini, Dkt. LU Youqing  anayemaliza muda wake akimueleza jambo Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai alipofika kumuaga  mapema leo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa masuala ya  Diplomasia na Vyombo ya Habari- Ubalozi wa China Bi. Wang Fang.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akimkabidhi zawadi  Balozi wa China nchini LU Youqing  anayemaliza muda wake alipofika kumuaga  mapema leo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
Balozi wa China nchini, Dkt. LU Youqing  anayemaliza muda wake akimkabidhi  zawadi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai alipofika kumuaga  mapema leo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu wa Spika Bw. Said Yakubu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai katika picha ya pamoja  na Balozi wa China nchini, Dkt. LU Youqing  anayemaliza muda wake alipofika kumuaga  mapema leo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai akiagana  na Balozi wa China nchini, Dkt. LU Youqing  anayemaliza muda wake mara baada ya kuzungumza nae  mapema leo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Bunge)
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: BALOZI WA CHINA AFIKA OFISINI KWA SPIKA NDUGAI KUMUAGA
BALOZI WA CHINA AFIKA OFISINI KWA SPIKA NDUGAI KUMUAGA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhtWTAVWclr6DZ1mjeTKbGXOj3st1XqyOV0rTOkwOdGWjDwPt0HCp7Ga8te8FVjcyWya45uPdaM3ZjdWs2enNS-Ui0BabZjfdFIAVjobmWIsvnMtvo67uRtMtiULBBwZsEL85_GhH0OYOpS/s640/PIC+1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhtWTAVWclr6DZ1mjeTKbGXOj3st1XqyOV0rTOkwOdGWjDwPt0HCp7Ga8te8FVjcyWya45uPdaM3ZjdWs2enNS-Ui0BabZjfdFIAVjobmWIsvnMtvo67uRtMtiULBBwZsEL85_GhH0OYOpS/s72-c/PIC+1.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/08/balozi-wa-china-afika-ofisini-kwa-spika.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/balozi-wa-china-afika-ofisini-kwa-spika.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy