DKT. MWIGULU AAGIZA WANAOPANGA MIPANGO YA MAANDAMANO WAKAMATWE

Na Ripota Wetu,Globu ya Jamii WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Mwigulu Nchemba amesema amemuagiza na kumuelekeza Mkuu wa Jeshi la Polis...



Na Ripota Wetu,Globu ya Jamii


WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Mwigulu Nchemba amesema amemuagiza na kumuelekeza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro kuwakamata watu wote ambao wamepanga njama za kutaka kuwauwa watanzania katika maandamano ambayo wameyapanga kuyafanya Aprili 26 mwaka huu.


Dk.Mwigulu ametoa maelekezo hayo wakati alipokuwa akitoa salamu zake kwa Rais Dk.John Magufuli aliyopo mkoani Singida katika ziara yake ya kikazi ambapo jana amezindua kiwanda cha Alizeti mkoani humo.Amesema lengo la maandamano hayo ni kutaka kuchafua taaswira ya nchi na tayari ameshatoa maelekezo kwa IGP Sirro.


"Njama hiyo tumeiona na mimi nimemuelekeza IGP Sirro kwamba hata kupanga njama ya kuua ni kosa, wachukue hatua kwa wale watu wanaopanga mipango ya aina hiyo na kuchafua taswira ya nchi yetu ama kwa mipango yao au ya wale wanaowatuma." Watu wanataka mikusanyiko ili wafyatue na kuuwa watu ili kuchafua taswira ya nchi yetu na tunayo mifano wa maeneo waliwahi kufanya jambo la aina hiyo na hatua zitachukuliwa", amesema Dk.Mwigulu.


Pamoja na hayo, Dk.Mwigulu ameendelea kwa kusema "Mhe. Rais ndio maana unaona vinyago vinyago vingi hivi kama hivi juzi alitokea kijana mdogo amesema ametekwa, eti ametekwa na akapata muda wa kutafuta pafyumu na nguo za kubadilishia kule atakapokuwa ametekwa. Unatowa wapi muda wa kujiandaa ?


"Watu wanatafuta njia za kuchafua taswira ya nchi yetu, na jambo hili Mhe. Rais kama ambavyo ulishatoa maelekezo, si jambo ambalo tutacheza nalo wala mjadala, hakuna sababu ya maandamano wala hakuna sehemu ya kuandamania na hakuna ruhusa ya kuandamana,"amesisitiza.Pia Dk.Mwigulu amesema endapo ikatokea hata watu wakaandamana ndani ya nyumba zao bado sheria itachukua mkondo wake dhidi ya watu hao.


"Ikitokea hata watu wakaandamana ndani ya nyumba wakazunguka kitanda na akatokea mtu akaumia, yule aliyeitisha waandamane pale atakuwa nala kuajibika kwasababu watu wanafanya mzaha na maisha na dira ya nchi yetu ambapo Rais umejitoa muhanga kwa ajili ya kutengeneza urithi wa watoto wa Tanzania",amesisitiza Dk. Mwigulu.


Kwa upande mwingine, amesema yeyote atakayethubutu kutaka kuharibu Taifa la Tanzania kwa kufanya vitendo vya uovu hawatoweza kumuacha salama.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: DKT. MWIGULU AAGIZA WANAOPANGA MIPANGO YA MAANDAMANO WAKAMATWE
DKT. MWIGULU AAGIZA WANAOPANGA MIPANGO YA MAANDAMANO WAKAMATWE
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiIQaOd4SMqbvAuPaTs9m0bZ-MBMtR6aasZJfPJN1VG4_xRx5wie11nAKRZGKbYyJw8vSeAjig9xgKJ0j3mu2fcJJi8UpHjYlvgy5uJn6v6GmCmLpYGl7Pf2wAbVoR6jSUJ9-xBR-90IV53/s400/Mwigulunchemba.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiIQaOd4SMqbvAuPaTs9m0bZ-MBMtR6aasZJfPJN1VG4_xRx5wie11nAKRZGKbYyJw8vSeAjig9xgKJ0j3mu2fcJJi8UpHjYlvgy5uJn6v6GmCmLpYGl7Pf2wAbVoR6jSUJ9-xBR-90IV53/s72-c/Mwigulunchemba.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/03/dkt-mwigulu-aagiza-wanaopanga-mipango.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/03/dkt-mwigulu-aagiza-wanaopanga-mipango.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy