Na Jonas Kamaleki-MAELEZO. Zaidi ya vijana wapatao 1230 wametoa siri nzito kwa Maaskofu na ...
Na Jonas Kamaleki-MAELEZO.
Zaidi ya vijana wapatao 1230
wametoa siri nzito kwa Maaskofu na Mashekhe kutoka katika Kamati ya
Kitaifa ya Maadili , Amani na Haki za Binadamu kwa Jamii ya Madhehebu ya
Dini Nchini kufichua mtandao haramu wa watu wanaoendesha mauaji na
uhalifu mwingine kwenye mikoa 13, nchini kama njia muhimu ya
kumpongeza IGP mpya, Saimoni Sirro.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa
Kamati hiyo, Askofu William Mwamalanga, siri hiyo imetolewa jana na
vijana hao katika siku ya tatu mkutano wa kujenga maadili kwa vijana
unao fanyika Mbagala, jijini Dar es Salaam na kuwashirikisha vijana
wa madhehebu mbalimbali ya dini kutoka katika mikoa ya Pwani, Tanga,
Lindi, Morogoro,Dar es Salaam ambapo wameyataja maeneo ya Mkuranga,
Rufiji Kigamboni, Kibiti, Msata, Tanga mjini, Pemba na Unguja kuwa
maeneo hatari yanayowajengea vijana imani za kigaidi.
Aidha, Askofu Mwamalanga
alisema kuwa vijana 147 wa kiislamu wanaohudhuria mkutano huo
wamewataja baadhi ya watu ambao ni hatari na wamekuwa wakieneza
elimu ya mauaji kwenye misikiti mbali mbali nchini kwa kuiita Serikali
ya Awamu ya Tano jina la katili na kwamba elimu hiyo imesambazwa kwa
kasi katika mikoa ya Kagera, Tanga, Mwanza, Arusha, Pemba, Unguja, Dar
es Salaam, Lindi, Mtwara, Morogoro, Iringa, Singida, Dodoma, Pwani na
Kigoma huku vikosi vya vijana vikiandaliwa kufanya mauaji mara baada ya
mufungo mtukufu wa Ramadhani kama yale ambayo yamekuwa yakifanywa
Mukuranga, Kibiti na Rufiji.
Vijana hao wanamuomba IGP
Sirro kuwachukulia hatua kali maafisa wa jeshi hilo ambao wanatumia
jeshi kupandikiza Umngiki, na kwamba wana imani na IGP Sirro amabaye
kwa mujibu wa hao vijana hatamwangusha Rais Magufuli na watanzania kwa
ujumla.
Akifunga Mkutano huo
Askofu Mwamalanga amemtaja IGP Sirro kama polisi mahiri wa maadili na
jemadali mweledi wa mapambano hivyo amewataka vijana kote nchini
kumuunga mkono kwa kuwafichua polisi wote wanaoenzi uhalifu.
“Tusipofanya hivyo tutakuwa kama pipa zuri tunalo jaza maji wakati
tukijua chini limetoboka”,alisema Askofu Mwamalanga na kuongeza kuwa
raia wema ni asilimia 99.9 wahalifu ni 0.1 hii ina maana kuwa
ukiondoa polisi wahalifu ndani ya jeshi hilo wahalifu ni wachache mno
mitaani watayeyuka wenyewe.
Aidha, Askofu huyo
amewahimiza vijana na viongozi wa dini kushiriki kwenye mafunzo hayo
kote nchini ili wapewe ufahamu wa elimu ya maadili ya kweli ili wawe
walinzi wa taifa na kupenda amani na kuweka uchu wa kuchukia rushwa na
kujiwekea mitazamo ya kupenda kazi za baraka.
Kiongozi huyo wa dini amekemea
vikali nyumba za ibada kugeuzwa eneo la mafunzo ya uhalifu kwani ni
aibu kwa msikiti au kanisa kufanya mafunzo ya kigaidi ndani ya
nyumba za ibada kufanya hivyo ni ibada ya sanamu, watu wa jinsi hiyo
hawana uhusiano wowote na Mwenyenzi MUNGU ambaye kusudi lake ni kuondoa
uovu kwa mwanadamu.
Hivi karibuni yametokea mauaji
ya viongozi wa Chama Tawala maeneo ya Kibiti, Mukuranga na Rufiji na
kufanya wakazi wa maeneo hayo kuishi kwa wasiwasi na mashaka juu ya
maisha yao. Wakati akiipishwa kuwa IGP, Kamanda Simon Sirro alisema
kupambana na kuondoa uhalifu kwa kushirikiana na raia wema ni moja ya
vipaumbele vyake.
COMMENTS