WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imeadhimia kupambana vilivyo dhidi ya biashara haramu ya dawa za kulevya na kuhakikisha ...
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imeadhimia kupambana vilivyo
dhidi ya biashara haramu ya dawa za kulevya na kuhakikisha inakuwa
historia nchini.
Pia
ametoa wito kwa wazazi wote nchini waendelee kufuatilia nyendo za watoto
ili wasijiingize kwenye mtego wa dawa za kulevya na wala wasisubiri
vijana wao waanze kutumia.
Ametoa
kauli hiyo leo (Alhamisi, Juni 29, 2017) kwenye maadhimisho ya Kitaifa
ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani, iliyoadhimishwa mjini
Dodoma.
Kufuatia
hali hiyo Waziri Mkuu amesema Serikali imejidhatiti kuhakikisha kuwa
uzalishaji, usambazaji na matumizi ya dawa za kulevya unadhibitiwa
kikamilifu nchini.
Amesema
katika kutimiza azma hiyo, ambayo pia inaelekezwa na Ilani ya Uchaguzi
ya CCM, Serikali ilifanya mabadiliko ya Sheria ya Dawa za Kulevya kwa
kuanzisha chombo cha kisheria cha kupambana na biashara hiyo, ambayo
imeongeza adhabu kwa wanaoshiriki.
Waziri
Mkuu amesema Serikali itaendelea kuimarisha chombo hicho kinachoongoza
mapambano ya dawa za kulevya ili kiendelee kufanya kazi kwa weledi na
kwa kutumia mbinu za kisayansi.
“Tunaponadi
uchumi wa viwanda lazima tuwe na nguvu kazi yenye siha njema kuweza
kushiriki kwenye kazi halali za kujenga Taifa letu na yeyote anayetaka
kudhohofisha nguvu kazi ya Taifa letu au kuhujumu jitihada za uchumi wa
viwanda atashughulikiwa bila huruma,” amesema.
Aidha,
kauli mbiu ya maadhimisho hayo kitaifa ni ‘Tuwasikilize na Kuwashauri
Vijana na Watoto ili Kuwaepusha na Dawa za kulevya.’
Waziri
Mkuu amesema kauli mbiu hiyo imetokana nan a takwimu za waathirika
wakubwa wa dawa za kulevya ambao ni vijana wenye umri kati ya miaka
15-35.
“Hili
ndilo kundi kubwa kwenye jamii jetu na ndilo tegemeo kubwa kwa ustawi wa
nchi yetu. Hili ndilo kundi litakalotoa askari wa kulinda Nchi yetu,
wanasiasa wa kuongoza Taifa letu na wataalamu mbalimbali wa kuisaidia
Tanzania,” amesema.
Awali
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Ajira na
Walemavu), Mheshimiwa Jenista Mhagama alisema matumizi ya dawa za
kulevya yamelisababishia Taifa madhara makubwa ya kiafya na kiuchumi
hivyo kila mwananchi ashiriki katika mapambano hayo.
Mapema
Waziri Mkuu aliweka jiwe la msingi la Kituo cha Kutoa Huduma ya Tiba
kwa Waathirika wa Dawa za Kulevya katika eneo la Itega mkoani Dodoma na
kuwashauri wakazi wa mkoa huo kutojihusisha na biashara hiyo.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA.
ALHAMISI, JUNI 29, 2017
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku
ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani kwenye uwanja wa Nyerere mjini
Dodoma Juni 29, 2017. 
Balozi wa Uingereza Nchini, Sarah Cooke akizungumza katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani kwenye uwanja wa Nyerere mjini Dodoma Juni 29, 2017

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama dawa mbalimbali za kulevya katika maonyesho yaliyokwenda sambamba na Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani kwenye uwanja wa Nyerere mjini Dodoma Juni 29, 2017

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la Msingi la Kituo cha Kutoa Huduma kwa Waathirika wa Dawa za Kulevya mjini Dodoma Juni 29, 2017. Kushoto ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na kulia ni Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers Sianga
Wasanii wa Kikundi cha Mchoyi cha Dodoma wakicheza ngoma ya kabila la Wagogo katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za ulevya Duniani kwenye uwanja wa Nyerere mjini Dodoma Juni 29, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuhutubia katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani kwenye uwanja wa Nyerere mjini Dodoma Juni 29, 2017
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Gaudensia Simwanza wakati alipotembelea banda la Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani kwenye uwanja wa Nyerere mjini Dodoma Juni 29, 2017.
Baadhi ya wananchi na Viongozi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani kwenye uwanja wa Nyerere mjini Dodoma Juni 29, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

COMMENTS