Na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA. Serikali kupitia Wizara ya Maji na Umwagiliaji imesema kuwa Serikali ya India imeahidi kutoa dola m...
Na Daudi Manongi-MAELEZO,
DODOMA.
Serikali kupitia
Wizara ya Maji na Umwagiliaji imesema kuwa Serikali ya India imeahidi kutoa
dola milioni 500 kwa ajili utekelezaji wa miradi ya maji katika miji 16 ya
Tanzania Bara na Zanzibar katika awamu ya tatu katika mwaka wa fedha 2017/18.
Hayo yamesemwa na
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe.Eng.Isack Kamwelwe akijibu Swali la
Mbunge wa Tumbatu Mhe.Juma Othman Hija leo Bungeni Mjini Dodoma.
“Katika bajeti ya
mwaka 2016/17 Wizara yangu ilitoa taarifa ya mchango mkubwa inaoupata kutoka
Serikali ya India ili kuboresha huduma ya Maji nchini kupitia mkopo wa masharti
nafuu kutoka Serikali hiyoa”,Aliongeza Mhe.Kamwelwe.
Aidha katika awamu ya tatu hatua inayoendelea kwa
sasa ni kufanya manunuzi ya Mhandisi Mshauri atayefanya mapitio ya usanifu wa
miradi na uandaaji wa makabrasha ya zabuni kwa ajili ya ujenzi ambapo kazi ya
ujenzi zinatarajiwa kuanza katika mwaka wa fedha 2017/18.
Amesema kuwa katika
awamu ya kwanza Serikali ilipata dola za kimarekani Milioni 178.125 ambapo kazi
zilizotekelezwa katika awamu hiyo ni upanuzi wa mradi mkubwa wa Ruvu Juu,Ujenzi
wa bomba kuu kutoka Mlandizi hadi Kimara,Pia Ujenzi wa mfumo wa usambazaji maji katika Jiji la Dar es Salaam pamoja na ujenzi
wa mradi Chalinze.
COMMENTS