Na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA. Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano imesema itajenga daraja la juu kwa aji...
Na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA.
Serikali
kupitia Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano imesema itajenga
daraja la juu kwa ajili ya kivuko cha waenda kwa miguu (Over head
Pedestrian Bridge) eneo la Kawe Bondeni.
Hayo
yamesemwa Bungeni leo na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe.Isack
Kamwelwe aliyekuwa akijibu swali la Mbunge wa Kawe Mhe.Halima Mdee kwa
Niaba ya Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano.
“Tatizo
la kivuko cha waenda kwa miguu eneo la Kawe Bondeni hadi Jeshini Kata
ya Mbezi Juu na Kawe Tayari limeshapatiwa ufumbuzi”, Aliongeza
Mhe. Kamwelwe.
Amesema kwa sasa Mkandarasi wa kujenga daraja hilo yupo kwenye hatua za maandalizi ya kuanza ujenzi katika eneo hilo muhimu.
Aidha
Serikali ina mpango wa kuweka taa za kuongozea magari katika Barabara
ya Mwenge-Tegeta ambapo Mkandarasi ameshapatikana wa kuweka taa hizo
katika makutano ya Afrikana na anatarajia kuanza kazi wakati wowote.
Mbali
na Hayo tatizo la Udogo wa mapokeo na matoleo ya maji ya mvua
yanayosababisha kero katika eneo la Makonde hadi Mbuyuni,Serikali
inakamilisha taratibu za kusaini mkataba wa ujenzi wa mtaro mkubwa eneo
la Mbezi Samaki ambao utatatua kero ya barabara kujaa maji nyakati za
mvua.
“Serikali
ya Awamu ya Tano ni makini sana na itahakikisha changamoto hizi
inazifanyia kazi ili wananchi waweze kutumia barabara zetu
vyema”Aliongeza Mhe.Kamwelwe.
COMMENTS