Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Yamungu Kayandabila akiongea na watumishi wa wizara hiyo katika m...
Katibu
Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Yamungu
Kayandabila akiongea na watumishi wa wizara hiyo katika mkutano wa
Baraza la Wafanyakazi na kuwataka waongeze jitihada za makusanyo ya kodi
ya pango la ardhi.
Baadhi
ya Watumishi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Yamungu
Kayandabila wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi.
Baadhi
ya Watumishi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Yamungu
Kayandabila wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi.
Baadhi
ya Watumishi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Yamungu
Kayandabila wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi.
Katibu
Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Yamungu
Kayandabila katikati, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Dkt. Moses
Kusiruka kushoto na Mjumbe Baraza kuu la Wafanyakazi Serikalini (TUGHE)
kulia, wakiimba wimbo wa mshikamano kwa wafanyakazi.

ya Watumishi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakiimba
wimbo wa mshikamano kwa wafanyakazi wakati wa mkutano wa Baraza la
Wafanyakazi.
………………………………………………………
Na Hassan Mabuye, Kitengo cha Mawasiliano, Wizara ya Ardhi.
Serikali
imefanikiwa kukusanya jumla ya kiasi cha shilingi bilioni 76 cha
makusanyo ya kodi ya pango la ardhi hadi kufikia tarehe 13 Mei 2017
kiwango ambacho hakijawahi kufikiwa.
Akiongea
katika mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Yamungu Kayandabila
amesema kiwango cha makusanyo ya kodi ya ardhi hakijawahi kufukiwa
ukilinganisha na miaka ya nyuma ambapo kwa sasa Wizara ya Ardhi imeisha
kusanya kiasi cha shilingi bilioni 76 cha kodi ya pango la ardhi.
Juhudi
za kukusanya kodi ya pango la ardhi kwa viwanja vilivyopimwa
zinaendelea vizuri licha ya changamoto iliyopo hususan muamko wa
wananchi katika kulipa kodi, amesema Dkt. Kayandabila.
“Ni
matumaini yangu kuwa katika kipindi kilichobaki Wizara itafikia lengo la
kukusanya kiasi cha makusanyo ya kodi ya pango la ardhi kilichowekwa
kwa mwaka wa fedha 2016/2017 ambacho ni kiasi cha shilingi bilioni
111.7”. Amesema Dkt. Kayandabila.
Amesema,
Serikali kuanzia mwezi julai, 2017 kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi itaanza kukusanya kodi ya pango la ardhi kwenye
viwanja na mashamba yasiyopimwa. Lengo la utaratibu huu ni kuongeza wigo
wa mapato yatokanayo na kodi ya pango la ardhi.
Utaratibu
huu utawafanya wananchi wote wanaomiliki ardhi waweze kulipa kodi. Hata
hivyo, ni vema ieleweke kuwa uamuzi huu hauna lengo ya kupunguza juhudi
za Wizara katika kupanga, kupima na kumilikisha ardhi kwa wananchi,
isipokuwa utaratibu huu unajenga dhana ya uwajibikaji kwa wananchi wote
katika kulipa pango la ardhi kwenye maeneo yao.
Aidha,
serikali imeanza Ujenzi wa mfumo wa kielektronic wa kumbukumbu za Ardhi
(Integrated Land Management System) ambao umeanza kutekelezwa. Mfumo
huo ukikamilika utasaidia sana kuwa na kumbukumbu sahihi za wamiliki wa
ardhi na hivyo kurahisisha ukusanyaji wa kodi za Ardhi.
COMMENTS