Viongozi wa juu wa CHADEMA, wakiongozwa na Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, wakiwa kwenye kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho mjini ...
Viongozi wa juu wa CHADEMA, wakiongozwa
na Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, wakiwa kwenye kikao cha Kamati Kuu
ya chama hicho mjini Dodoma leo Mei 26, 2017. Kwa mujibu wa taarifa ya
chama hicho inayopatikana hapo chini, chama hicho kimeanza vikao nyeti
vya chama mjini humo leo Ijumaa na kesho Jumamosi, Baraza Kuu la chama
hicho litakutana mjini humo Jumamosi Mei 27. Katuka hatua nyingine,
Msemaji wa chama hicho Tumaini Makene amekanusha vikali taarifa
zinazodai kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Dkt.Vincent Mashinji
amejiuzulu wadhifa wake. Makene katika taarifa yake aliyoitoa mjini
Dodoma amesema."Tumeona tweetter moja inayotembea tena ya kiongozi mmoja
wa CCM na nimejibu nimesema kwamba taarifa hizi zinasambazwa na
viongozi wa CCM, Katibu Mkuu yupo mjini Dodoma tangu Jumanne kwa sababu
kuna kikao cha summit ya TDC, na jana alikuwa anaongoza kikao cha
Sekretariati ya chama kwa sababu yeye ndiye mwenyekiti wa kikao hicho na
leo yuko kwenye kikao cha Kamati Kuu ya chama ambayo inaandaa agenda za
kikao cha baraza kuu na Katibu Mkuu alikuwepo." Alisema Makene.
COMMENTS