BURIANI MWANAHABARI REVOCATUS BULIZYA
HomeJamii

BURIANI MWANAHABARI REVOCATUS BULIZYA

Marehemu Revocatus Bulizya enzi za uhai wake Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Mwanahabari Revocatus Bulizya wakati...

BALOZI WA CUBA NCHINI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA KAMISHNA JENERALI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI
RAIS DKT MAGUFULI MGENI RASMI KATIKA MAADHIMISHO YA MWAKA MPYA WA MAHAKAMA
PROF. KAMUZORA ATEMBELEA NA KUKAGUA KITUO CHA OPARESHENI NA MAWASILIANO YA DHARURA.



Marehemu Revocatus Bulizya enzi za uhai wake
Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Mwanahabari Revocatus Bulizya wakati ukiingizwa katika Kanisa la Katoliki Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya ibada ya kuuaga kabla ya kwenda kwenye mazishi yaliyofanyika Mwandege Kongowe Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam leo.

Mjane wa marehemu na mtoto wao (katikati), akisaidiwa na dada yake aliyewahi kuwa Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam toka mwaka 2010/2015, Shelymar Kweygia kuingia katika kanisa hilo kwa ajili ya ibada ya kuuaga mwili huo.





Jeneza likiingizwa kanisani.



Waombolezaji wakiwa katika ibada ya kuuaga mwili huo.
Wanahabari wa Sahara Media alikokuwa akifanya kazi marehemu katika Kituo cha Televisheni cha Star TV na ndugu jamaa wa marehemu wakiwa kwenye ibada hiyo. 
Wanahabari wakiandika wasifu wa marehemu Revocatus Bulizya.
Wanahabari Kibwana Dachi (kulia) na Ben Mwanantala 
wakiwa kwenye ibada hiyo.
Katekista wa Parokia ya Muhimbili akiongoza ibada hiyo.
Ni huzuni katika ibada hiyo.

Na Dotto Mwaibale

VILIO na majonzi vilitawala wakati wa ibada ya kuuaga mwili wa mwanahabari Revocatus Bulizya wa Kituo cha Televisheni cha Star TV wakati wa ibada ya kumuaga iliyofanyika Kanisa Katoliki la Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) Dar es Salaam leo asubuhi.

Ibada hiyo ilihudhuriwa na ndugu jamaa na marafiki wa marehemu pamoja na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali akiwepo aliyewahi kuwa Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam toka mwaka 2010/2015, Shelymar Kweygia ambaye ni ndugu ya mke wa Bulizya.

Akitoa mahubiri wakati wa ibada hiyo Katekista wa Paroko ya Kanisa Katoliki MNH, alisema ni wakati wa kila mmoja wetu kutafakari juu ya maisha yake ya kimungu.

Alisema hakuna njia ya kukutana na mungu bila ya kifo na ndio maana wakati wote tunatakiwa kujiandaa kwa sababu hatui ni lina tutatoweka duniani kama alivyotuacha ndugu yetu Revocatus Bulizya.

Recocatus Bulizya alizaliwa tarehe 29-10-1979 na kufariki dunia tarehe 2-5-2017 kwa kugongwa na pikipiki 'bodaboda' maeneo ya Pugu jijini Dar es Salaam wakati akirejea nyumbani kwake akiwa ameongoza na mke wake.

Mazishi ya marehemu yamefanyika Mwandege Kongowe Barabara ya Kilwa nje kidogo ya jijini Dar es Salaam na mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu.

(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com.simu namba 0712-727062)

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: BURIANI MWANAHABARI REVOCATUS BULIZYA
BURIANI MWANAHABARI REVOCATUS BULIZYA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjCASdR_BO8cn_cz9kpeToS2PTbJ5FZKl2H7RR1K0Osu5WuLn10PndjGNtgpRX3GFYU3pgvoiAVBQ0Nki8tqlvEC1sm5zwiVcKUcbagtluFihFTkJfxwP7_9yFUj6tMFzUxRXmuucAXKpRR/s640/1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjCASdR_BO8cn_cz9kpeToS2PTbJ5FZKl2H7RR1K0Osu5WuLn10PndjGNtgpRX3GFYU3pgvoiAVBQ0Nki8tqlvEC1sm5zwiVcKUcbagtluFihFTkJfxwP7_9yFUj6tMFzUxRXmuucAXKpRR/s72-c/1.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/05/buriani-mwanahabari-revocatus-bulizya.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/05/buriani-mwanahabari-revocatus-bulizya.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy