RAIS DKT MAGUFULI MGENI RASMI KATIKA MAADHIMISHO YA MWAKA MPYA WA MAHAKAMA
HomeJamii

RAIS DKT MAGUFULI MGENI RASMI KATIKA MAADHIMISHO YA MWAKA MPYA WA MAHAKAMA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU Simu: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: press@ikulu.go.tz ...

WAZIRI JAFO-KUMSOMESHA MTOTO NI IBADA KUBWA SANA KATIKA MAISHA YETU YA KILA SIKU
SERIKALI KUBORESHA KIVUTIO CHA UTALII CHA ENEO LA BARABARA YA LAMI INAYOPITA JUU ZAIDI KUTOKA USAWA WA BAHARI
RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA MWAKILISHI MKAZI WA BENKI YA DUNIA, AENDESHA BARAZA LA MAWAZIRI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO




JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULUDescription: Description: Description: Description: Description: Coat of Arms
Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz               

Faksi: 255-22-2113425


OFISI YA RAIS,
     IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,   
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amesema Serikali inaunga mkono utekelezaji wa matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa Mahakama ili kuongeza ufanisi wa majukumu yake.
Mhe. Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo tarehe 01 Februari, 2018 wakati akihutubia katika siku ya sheria, maadhimisho ambayo yamefanyika katika Mtaa wa Chimala, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam, yakiwa na kauli mbiu “Matumizi ya Tehama katika utoaji wa haki kwa wakati na kuzingatia maadili”.
Pamoja na kuunga mkono matumizi ya TEHAMA kwa Mahakama, Mhe. Rais Magufuli ameipongeza Mahakama kwa kazi inayoifanya ikiwemo kupunguza mrundikano wa kesi na ameahidi kuwa Serikali ipo tayari kusikiliza ushauri wa Mahakama juu ya maslahi ya wafanyakazi utakaotolewa mwezi huu na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma.
Pia Mhe. Rais Magufuli amesema yupo tayari kufanya uteuzi wa Majaji wengine kadiri atakavyoshauriwa na Mahakama ili kukabiliana na changamoto ya upungufu mkubwa wa Majaji iliyosababisha ongezeko kubwa la mrundikano wa mashauri katika Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani.
Hata hivyo Mhe. Rais Magufuli ametoa wito kwa Mahakama kuendelea kurekebisha dosari ambazo zimekuwa zikiuchafua mhimili huo wa Dola ikiwemo Majaji na Mahakimu kujihusisha na vitendo vya upokeaji wa rushwa na ucheleweshaji wa kesi ambavyo vinasababisha hasara kubwa kwa Taifa.
“Nilikuuliza Mhe. Jaji Mkuu na mimi nasema kwa uwazi kabisa, katika vibali vingi vya kusafiri nje ya nchi ninavyoombwa na Majaji na ambavyo vyote huwa ninaruhusu, na vimenisaidia kufanya utafiti wangu, wengi huwa wanaomba kwenda likizo nje ya nchi, Afrika Kusini, Uingereza, nakadhalika, na wanaenda na familia zao, wanakaa huko kwa siku 28, na pale chini wanaandika kuwa watajigharamia, hili huwa ni swali ninalojiuliza sana, maana mshahara wa Jaji ninaujua.
“Na ukweli huwa nafuatilia anapokwenda kule anakaa hotel na nani amehusika kulipa hotel hiyo yenye gharama za juu, na kwa nini ni fulani fulani tu, Mhe. Jaji Mkuu majibu hujayapata na mimi sijayapata, sasa Mhe. Jaji Mkuu fuatilia hili” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Aidha, Mhe. Rais Magufuli amempongeza Mhe. Jaji Mkuu kwa hatua alizochukuwa kuwafukuza kazi watumishi 112 wa Mahakama wakiwemo Mahakimu 17 waliojihusisha na vitendo vya ukiukwaji wa maadili na amevishangaa vyombo vingine ambavyo hushirikiana na Mahakama kama vile Jeshi la Polisi, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Magereza na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kwa kutowawajibisha watumishi wake wanaokiuka maadili.
“Mwaka jana nililalamika, sasa mwaka huu sitalalamika, nitachukua hatua, tena mwezi huu wa pili hautaisha, pale ofisini kwangu napokea barua nyingi za malalamiko ya ucheleweshaji wa kesi, kila kesi upelelezi haujakamilika, ni lazima kuwe na utatuzi wa jambo hili, hivi sasa kuna kesi za Shilingi Bilioni 169.1 na Dola za Marekani Milioni 38.2 zinasubiri tu na nchi inakosa mapato” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.
Halikadhalika Mhe. Rais Magufuli amemtaka Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi, kukamilisha kanuni za sheria ya msaada wa kisheria (Legal Aid Act, No.1 of 2017) ambayo imepitishwa na Bunge na kusainiwa na Rais tangu miezi 9 iliyopita, ndani ya kipindi cha mwezi mmoja kuanzia sasa.
Mapema kabla ya hotuba ya Mhe. Rais Magufuli Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma alisema Mahakama imedhamiria kuanza matumizi ya TEHAMA katika shughuli zake na ametaka watumishi hasa Majaji na Mahakimu wajiandae kutumia teknolojia hiyo, na pia ameahidi kuwa Mahakama itaendelea kuchukua hatua dhidi ya vitendo vya ukiukwaji wa maadili na kusimamia uwajibikaji.
Nae Makamu wa Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) Mhe. Godwin Simba Ngwilimi amesema TLS inaunga mkono dhamira ya kutumia TEHAMA katika shughuli za Mahakama na amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa uongozi wake unaoakisi nia na matarajio ya Watanzania.


Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
01 Februari, 2018


(Juu na chini) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wakati wa maadhimisho ya mwaka mpya wa mahakama ama Siku uya Sheria kwenye uwanja wa Mahakama kuu Ocean Road jijini Dar es salaam leo.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiteta jambo na Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma baada ya kuhutubia katika maadhimisho ya mwaka mpya wa mahakama ama Siku uya Sheria kwenye uwanja wa Mahakama kuu Ocean Road jijini Dar es salaam leo.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Jaji Mkuu Profesa Ibrahim  Juma na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Othman Omar Makungu, , Naibu spika Dkt. Tulia Ackson, Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi na  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais  - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora -  Mhe George Mkuchika katika picha ya pamoja na viongozi wa dini na Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama baada ya kuhutubia wakati wa maadhimisho ya mwaka mpya wa mahakama ama Siku uya Sheria kwenye uwanja wa Mahakama kuu Ocean Road jijini Dar es salaam leo. 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Jaji Mkuu Profesa Ibrahim  Juma na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Othman Omar Makungu, , Naibu spika Dkt. Tulia Ackson, Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi na  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais  - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora -  Mhe George Mkuchika katika picha ya pamoja na Majaji  Wastaafu baada ya kuhutubia wakati wa maadhimisho ya mwaka mpya wa mahakama ama Siku uya Sheria kwenye uwanja wa Mahakama kuu Ocean Road jijini Dar es Salaam leo. 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Makamu wa Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) Mhe. Godwin Ngwilimi baada ya kuhutubia katika maadhimisho ya mwaka mpya wa mahakama kama Sikukuu ya Sheria kwenye uwanja wa Mahakama kuu Ocean Road jijini Dar es Salaam leo. (Picha na IKULU)









Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: RAIS DKT MAGUFULI MGENI RASMI KATIKA MAADHIMISHO YA MWAKA MPYA WA MAHAKAMA
RAIS DKT MAGUFULI MGENI RASMI KATIKA MAADHIMISHO YA MWAKA MPYA WA MAHAKAMA
https://i.ytimg.com/vi/bOWRdYg0jXY/hqdefault.jpg
https://i.ytimg.com/vi/bOWRdYg0jXY/default.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/02/rais-dkt-magufuli-mgeni-rasmi-katika.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/02/rais-dkt-magufuli-mgeni-rasmi-katika.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy