SERIKALI YAZINDUA USAMBAZAJI WA VIFAA VYA HOSPITALI NCHINI
HomeJamii

SERIKALI YAZINDUA USAMBAZAJI WA VIFAA VYA HOSPITALI NCHINI

Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai , Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy na Mkuu wa wilaya ya Kongwa, ...

KAMATI YA BUNGE YA ARDHI,MALIASILI NA MAZINGIRA YAVUTIWA NA UBUNIFU WA SHUGHULI ZA KITALII HIFADHI YA TAIFA YA ZIWA MANYARA
JKCI YAFANYTIA UPASUAJI WATOTO 15 WENYE MATATIZO YA MOYO WAFANYIWA UPASUA WA BILA KUFUNGUA KIFUA
MCHUNGAJI JOYCE NKONE KUFANYA KONGAMANO LA WANAWAKE JAN 27, 2018 VCCT- MBEZI BEACH 'A', DAR
Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai , Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy na Mkuu wa wilaya ya Kongwa, Deogratius Ndejembi wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa mpango huo.

Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai akipokea vitanda hivyo kutoka kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy , kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kongwa, Deogratius Ndejembi. 


Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu na Mkuu wa wilaya ya Kongwa Deogratius Ndejembi wakikagua vitanda hivyo mara baada ya makabidhiano.






Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai akizungumza wakati wa uzinduzi wa ugawaji wa vitanda vya hospitali nchi nzima uliofanyika wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma leo katikati ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kongwa, Deogratius Ndejembi. 
 
……………………………………………………………………..
Serikali ya awamu ya tano nchini imezindua rasmi usambazaji wa vifaa vya hospitali kwa halmashauri zote nchini katika kutekeleza mkakati wa kuboresha huduma za afya nchini kwa kuhakikisha wananchoi wanapata huduma kwa kiwango stahiki 

Akizindua usambazaji huo leo wilayani hapa,Waziri wa Afya,maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy mwalimu alisema serikali imetekeleza ahadi iliyotoa kwa wananchi ambapo serikali inawekeza katika afya ya wananchi hivyo kuweza kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi wa viwanda 

Akizungumza kwenye hadhara ya wanachi wa Wilaya ya Kongwa,Waziri Ummy alisema serikali imefanya uwekezaji mkubwa kwa baadhi ya maeneo ikiwemo ya upatikanaji wa dawa ambapo bajeti ya dawa imeongezeka kutoka shilingi bilioni 31 mwaka 2015/16 hadi shilingi bilioni 251 mwaka 2016/17. 

“Hatua hii imeleta mapinduzi makubwa katika upatikanaji wa dawa,vifaa na vifaa tiba kwenye vituo vya Umma vya kutolea huduma za afya,hivyo wanaomba wananchi kuhakikisha mnafika kwnye vituo vya kutolea huduma za afya ili kupata matibabu sahihi” 

Aidha, Waziri Ummy alisema kufuatia ahadi ya Mhe. Rais ya kununua na kusambaza vitanda kwenye vituo vya Umma ,Wizara yake kwa bajeti ya mwaka 2016/17 ilitenga kiasi cha shilingi biliuoni 4 za kuwezesha kununua pamoja na kusambaza vifaa hivyo kwa halmashauri 184 nchini
Alivitaja vifaa vilivyonunuliwa na kuvikabidhi kwa Mhe. Job Ndungai (Mb), Mbunge wa Kongwa na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungazo wa Tanzania Mhe. John Ndugai ni pamoja na vitanda vya hospitali (20),vitanda vya kujifungulia wajawazito (5), magodoro (25) na mashuka (50). 

Vifaa vya Hospitali vitakavyopasambazwa kwenye Halimashauri zote 184 nchini ni pamoja na vitanda vya hHospitalini 3,680; vitanda vya kujifungulia akinamama wajawazito 920; magodoro 4,600; na mashuka 9,200. Thamani ya vifaa hivi ni shilingi bilioni 2,933, 125,600. Zoezi la kugawa vifaa hivi linatarajiwa kukamilika kabla ya Juni 30, 2107. 

Akipokea vifaa hivyo, Mhe. Ndugai ameishukuru Serikali kwa msaada wa vifaa vilivyotolewa kwa Hospitali na vituo vya Afya katika mkoa wa Dodoma ikiwemo Halmashauri Kongwa. Vifaa hivyo vitaboresha afya ya wananchi wa jimbo la Kongwa na maeneo mengine nchini na hivyo kusaidia kuwawezesha wananchi kukutumia mudao wao mwingi katika shughuli za kiuchumi.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: SERIKALI YAZINDUA USAMBAZAJI WA VIFAA VYA HOSPITALI NCHINI
SERIKALI YAZINDUA USAMBAZAJI WA VIFAA VYA HOSPITALI NCHINI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgGC0YUUi2IpSQbvwac5St7pg4xjDa3q_1R65pPFvh07fLh8RngpBpdOYQUI8Z-E1wb-vozyPH_4Njt4_KaeOkq13hMlHEVHqI57Q5aOKGul6lhQ1tpnMUJ4PbAD2IXSvduiOWvrAa0dzk/s640/ndu2.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgGC0YUUi2IpSQbvwac5St7pg4xjDa3q_1R65pPFvh07fLh8RngpBpdOYQUI8Z-E1wb-vozyPH_4Njt4_KaeOkq13hMlHEVHqI57Q5aOKGul6lhQ1tpnMUJ4PbAD2IXSvduiOWvrAa0dzk/s72-c/ndu2.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/04/serikali-yazindua-usambazaji-wa-vifaa.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/04/serikali-yazindua-usambazaji-wa-vifaa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy