Mbunge wa Jimbo la Mtama, Mhe. Nape Nnauye akipita juu ya migongo ya baadhi ya akina Mama walioamua kulala chini ili kiongozi huyo apite...
Mbunge wa Jimbo la Mtama, Mhe. Nape Nnauye akipita juu ya migongo ya baadhi ya akina Mama walioamua kulala chini ili kiongozi huyo apite juu yao, ambapo imeelezwa kuwa imefanywa vile ikiwa ni sehemu ya heshima kubwa waliompa pamoja na upendo walionao kwa Mbunge wao kwa kusimamia ukweli. Kitendo hicho kilisababisha Mh. Nape ashindwe kujizuia na kuanza kutoa machozi.


Baadhi ya Wananchi na Wafuasi wa chama cha CCM wakiwa wamekusanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Kiwalala,Mtama mkoni Lindi wakimsubiri kumsikiliza Mbunge wao Mh,Nape Nnauye.

Mmoja wa akina mama akitokwa machozi mara baada ya kumuona Mh Nape

Baadhi ya Wasanii wa Filamu haba nchini wakiongozwa na Steve Nyerere walipanda jukwani kuzungumza machache na kuwashukuru wananchi kujitokeza kwa wingi kumuunga mkono Mbunge wao Mh.Nape Nnauye.

Baadhi ya Wananchi na Wafuasi wa chama cha CCM wakiwa wamekusanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Kiwalala,Mtama mkoani Lindi mapema leo wakimsubiri kumsikiliza Mbunge wao Mh,Nape Nnauye aliyewasili jimboni humo kuzungumza nao machache yakiwemo na mambo ya maendeleo ya jimbo lake

Sehemu ya Umati wa watu wakishangilia kwa pamoja mara baada ya Mh Nape kupanda jukwaani na kuianza kuimba nyimbo kwa pamoja huku wakicheza sambamba na shangwe za hapa na pale uwanjani hapo

Wananchi wakifuatilia mkutano huo wa hadhara

Sehemu ya Umati wa watu wakishangilia kwa pamoja mara baada ya Mbunge wa jimbo la Mtama,Mh Nape Nnauye kupanda jukwaani na kuanza kuimba na kucheza kwa pamoja huku miluzi,shangwe na vigele gele vikiwa vimetawala uwanjani hapo

Sehemu ya Umati wa watu wakishangilia kwa pamoja mara baada ya Mbunge wa jimbo la Mtama,Mh Nape Nnauye kupanda jukwaani na kuanza kuimba na kucheza kwa pamoja huku miluzi,shangwe na vigele gele vikiwa vimetawala kila kona uwanjani hapo

Sehemu ya Umati wa watu wakishangilia kwa pamoja mara baada ya Mbunge wa jimbo la Mtama,Mh Nape Nnauye kupanda jukwaani na kuanza kuimba na kucheza kwa pamoja huku miluzi,shangwe na vigele gele vikiwa vimetawala uwanjani hapo

Baadhi ya Wananchi wakimsikiliza Mbunge wao Mh Nape,alipowasili jimboni humo mapema leo kwa lengo la kuwashukuru kwa Kumchagua kuwa mwakilishi wao mzuri na pia kuzungumza mipango yao mbalimbali ya kuliletea maendeleo jimbo lake

Wananchi wakimsikiliza Mbunge wao Mh Nape Nnauye katika mkutano wa hadhara uliofanyika mapema loe jioni katika uwanja wa shule ya msingi Kiwalala,Mtama mkoani Lindi.

Mbunge wa jimbo la Mtama, Mh. Nape Nnauye akizungumza na Wananchi (hawapopo pichani) katika mkutano wa hadhara uliofanyika Aprili 8 2017 jimboni kwake, kwenye uwanja wa shule ya msingi Kiwakala, mkoani Lindi. Mh Nape aliwashukuru Wananchi wake kwa kumpigia kura za kutosha na hatimae akachaguliwa kuwa mwakilishi wao Bungeni. Pia alitumia fursa fursa ya mkutano huo kuwashukuru kwa mapokezi makubwa waliyompa na kumuonesha ni kiasi gani bado wanampenda na kumuhitaji kama kiongozi wao katika kuwaletea maendeleo.
''Kilichonitoa machozi ni heshima kubwa mlionipa akina Mama,Mlilala chini,makataka nipite juu yenu,si ambalo nililitegemea, Nawashukuru sana, Niwaahidi nitafanya kazi kwa nguvu zangu zote, kuwatumikieni, usiku na mchana, nitaikumbuka heshima hii mlionipa na sitoisahau", alisema Mh Nape huku sauti yake ikiendana na hisia ya kutoa chozi mbele ya umati mkubwa uliokuwepo uwanjani hapo.
Mh. Nape alizungumza mambo mbambali yakiwemo mambo mbalimbali ya kuiletea maendeo jimbo la Mtama,ikiwemo suala la Maji,Barabara,Elimu na Afya, kwa maeneo hayo kwa sasa atavisimamia kwa spidi kubwa kwa sababu kwa sasa amepata muda wa kutosha wa kuanza kuwahudumia wananchi wa jimbo lake na kuhakikisha anatimiza yale yote aliyokwisha waahidi wakati wa kampeni.Pia amewataka Wananchi hao kuungana na kitu kimoja na kuweka itikadi za kisiaza pembeni na kuhakikisha wanashirikiana katika kuhakikisha jimbo la Mtama linapiga hatua kimaendeleo.

Baadhi ya Wananchi na Wafuasi wa chama cha CCM wakiwa wamejitokeza kwa wingi kumsikiliza Mbunge wa jimbo lao, Mh Nape Nnauye.

Wananchi wakimsikiliza Mbunge wao alipokuwa akiwahutubia.

Diwani chama cha CUF kutoka kata ya Sudi, Ali Athumani Njale akimpa mkono wa pongezi na kumtia moyo Mbunge wa Jimbo la Mtama, Mh. Nape mara baada ya kumaliza kuwahutubia wananchi,katika mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo katika uwanja wa Kiwalala,Mtama mkoani Lindi, ambapo pia alimuachia ujumbe bahasha alioishika pichani.

Baada ya kumalizika mkutano wa kuwashukuru Wananchi wa jimbo la Mtama, ilifauata dua ya pamoja kutakiana heri na kusameheana yale yote mabaya yaliyotokea na kuanza kurasa mpya,ya kuhimizana kuishi kwa upendo na amani na kutoruhusu migingano isiyo tija kwa kila mmoja wao.

Gari aliyopanda Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye likisukumwa na Wananchi mara baada ya kumaliza mkutano wake, uliofanyika katika uwanja wa shule ya Msingi Makalala, Mtama, mkoani Lindi.

Gari aliyopanda Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye ikisukumwa na Wananchi, mara baada ya kumaliza mkutano wake, uliofanyika katika uwanja wa shule ya Msingi Makalala, Mtama, mkoani Lindi.

Gari aliyopanda Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye ikisukumwa na Wananchi, mara baada ya kumaliza mkutano wake, uliofanyika katika uwanja wa shule ya Msingi Makalala, Mtama, mkoani Lindi.

Baadhi ya Wananchi wakimsubiri Mbunge wao, Mh. Nape Nnauye ili wamasalimie na kusikia lolote kutoka kwake
COMMENTS