Mabingwa watetezi wa Ligi ya Vodacom Tanzanja Bara Yanga wamefanikiwa kutoka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Azam katika mchezo wa ligi k...
Mabingwa
watetezi wa Ligi ya Vodacom Tanzanja Bara Yanga wamefanikiwa kutoka na
ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Azam katika mchezo wa ligi kuu uliofanyika
katika dimba la Uwanja wa Taifa.
Mpira huo ulioanza majira ya sa 10 alasairi ulichezeshwa na Mwamuzi Jonesia Rukyaa akisaidiwa na John Kanyenye na Soud Lila ulikuwa na ushindani mkubwa huku Azam wakionekana kutawala sehemu ya kiungo.
Azam katika dakika 45 za kipindi cha kwanza walishindwa kutumia nafasi walizozipata kutokana na kutokuwa makini kwa safu yao ya ushambuliaji.
Kipindi cha pili kimeanza kwa kila upande kutafuta goli la kuongoza na katika dakika ya 71 mshambuliaji wa kimataifa kutoka Zambia Obrey Chirwa anaiandikia Yanga goli la kuongoza akitumia uzembe wa mabeki wa Azam kuurudisha mpira kwa golikipa Aishi Manula.
Yanga wanaamka na kuanza kulishambulia lango la Azam lakini nao wanakuwa makini na kusaka goli la kusawazisha na mpaka dakika 90 mwamuzi Jonesia anapuliza filimbi ya mwisho Yanga wanatoka kifua mbele kwa ushindi wa goli 1-0.
Baada ya matokeo hayo, Yanga wanafikisha alama 56 wakiwa mbele kwa alama moja dhidi ya mahasimu wao Simba wenye alama 55 ambao wanacheza na Kagera Sugar katika Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera.
Kikosi cha Yanga kilichoanza leo.
Kikosi cha Azam FC kilichoanza leo.
COMMENTS