NA K-VIS BLOG MVUA za masika zinazoendelea kunyesha hivi sasa, zimeleta madhara makubwa kwenye maeneo kadhaa ya jimbo la Chalinze mko...
NA K-VIS BLOG
MVUA za masika zinazoendelea kunyesha hivi sasa, zimeleta madhara makubwa kwenye maeneo kadhaa ya jimbo la Chalinze mkoani Pwani. Mbunge wa Jimbo hilo, Ridhiwani Kikwete, amesema maeneo yaliyoathirika sana na mafuriko hayo ni pamoja na Chalinze Mzee Bwawa la umwagiliaji la Msoga, ambalo kingo zake zimetoboka, na shule ya sekondari Imperial.
Alisema, zaidi ya Kaya 20 hazina mahala pa kuishi baada ya nyumba 9 kubomolewa na mafuriko hayo.
Aidha, alisema kuwa madhara mengine yaliosababishwa na mafuriko hayo ni kuharibika kwa mashamba, na kwa sasa wananchi hao wanahitaji msaada.
Ridhiwani ambaye alitembelea eneo hilo, ametoa pole kwa wakazi hao na kuwaomba kuwa vumilivu katika kipindi hiki.
Mbunge wa Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete, (mwenye nguo nyeupe) na baadhi ya wananchi wakitembelea moja ya maeneo yaliyoathirika na mafuriko ya mvua huko Chalizne Mzee.

Baadhi ya Nyumba katika eneo la Chalinze Mzee zikiwa zimearibika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akiangalia madhara yaliosababishwa na mafuriko katika jimbo hilo la Chalinze.

Wakazi wa chalinze wakiangalia nyumba zao zilizobomoka kutokana na mafuriko.

Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete (mwenye kanzu) akiwa na wananchi wa jimbo hilo wakikagua `Bwawa la Umwangiliaji la Msoga.

Sehemu ya bwawa la umwangiliaji la Msoga liloaribiwa na mafuriko na kupasua kingo za bwawa hilo.

Moja ya Nyumba iliyobomoka kutoka na mvua zinazoendelea kuonyesha katika eneo la Chalinze.

Moja ya Nyumba iliyobomoka kutoka na mvua zinazoendelea kuonyesha katika eneo la Chalinze.

Moja ya Nyumba iliyobomoka kutoka na mvua zinazoendelea kuonyesha katika eneo la Chalinze.

COMMENTS