WAZIRI MWIGULU AHIMIZA UADILIFU POLISI
HomeJamii

WAZIRI MWIGULU AHIMIZA UADILIFU POLISI

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba (kulia) pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu wakiongozwa na ...

TAASISI YA ELIMU YA WATU WAZIMA (TEWW) KUENDELEA KUWA KITOVU CHA KUTOA ELIMU BORA.
TAARIFA YA UMMA YA UTEUZI HIYOOO
RAIS DKT. MAGUFULI AWAPANDISHA VYEO MAAFISA MBALIMBALI WA JWTZ


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba (kulia) pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu wakiongozwa na askari wa kikosi cha bendera kuingia ukumbini kwa ajili ya ufunguzi wa kikao kazi cha mwaka kinachowahusisha maafisa wakuu wa jeshi la Polisi na makamanda wa mikoa na vikosi kinachofanyika mkoani Dodoma. (Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi)



Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba (kulia) akitoa hotuba ufunguzi wa kikao kazi cha mwaka kinachowahusisha maafisa wakuu wa jeshi la Polisi na makamanda wa mikoa na vikosi kinachofanyika mkoani Dodoma. 


 

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba (kulia) akiongea na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu wakati wa hafla ya ufunguzi wa kikao kazi cha maafisa wakuu wa jeshi la Polisi na makamanda wa mikoa na vikosi kinachofanyika mkoani Dodoma. 



Baadhi ya maofisa wakuu wa Jeshi la Polisi wakiimba wimbo wa maadili ya afisa wa polisi wakati wa hafla ya ufunguzi wa kikao kazi cha maafisa hao na makamanda wa mikoa na vikosi kinachofanyika mkoani Dodoma. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.

Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba amewataka maofisa na askari Polisi kote nchini kuendelea kufanya kazi kwa uadilifu ili kujenga taswira nzuri kwa wananchi wanaowahudumia jambo ambalo litaongeza imani na ushirikiano katika kukomesha vitendo vya uhalifu nchini.

Waziri Nchemba ameyasema hayo wakati alipokuwa akifungua kikao kazi cha Maofisa wakuu wa Jeshi la Polisi kutoka makao makuu, Makamanda wa Polisi wa Mikoa na vikosi kutoka bara na Zanzibar kinachoendelea mkoani Dodoma.

Alisema Pamoja na Jeshi hilo kufanya kazi nzuri bado linakabiliwa na changamoto ya baadhi ya askari na maofisa wasio waadilifu wanaofanya vitendo vya kuwabambikia wananchi kesi na wakati mwingine kuwabadilishia kesi ili kujenga mazingira ya kupatiwa rushwa jambo ambalo ni kinyume na maadili ya askari Polisi.

“Fanyeni kazi kwa weledi hasa kwa kuwasimamia waliopo chini yenu kwa kuwa wapo baadhi yao bado hawataki kubadilika na katika awamu hii lengo letu ni kutoa haki kwa maskini hivyo ninyi kama wasimamizi wa sheria mnapaswa kutenda haki mnapofanya kazi zenu na wale wasiotaka kubadilika hamna budi kuchukua hatua ” Alisema Nchemba.

Aidha alilitaka Jeshi hilo kuwachukulia hatua bodaboda wanaofanya makosa na wale wasiokuwa na makosa waachwe waendelee na majukumu yao ya kujipatia kipato na kuachana na dhana ya kuwa kila bodaboda ni mhalifu.
Kwa upande wake Inspekta Jenerali wa Polisi, IGP Ernest Mangu alisema kikao hicho kinafanyika kwa siku tatu kwa lengo la kufanya tathmini ya utendaji kazi kwa mwaka uliopita na kuweka mikakati kwa mwaka huu ili kuendeleza juhudi za kukabiliana na vitendo vya uhalifu hapa nchini.

Mangu alisema Jeshi hilo litaendelea na Oparesheni zake za kupambana na uhalifu zikiwemo za dawa za kulevya, uhalifu wa kutumia silaha na wizi wa mtandao kwa mikakati mipya ambayo itaibuliwa katika kikao kazi hicho ili kuhakikisha hakuna mhalifu anayetamba hapa nchini.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge mambo ya nje na usalama Balozi Adadi Rajabu alisema kamati hiyo itaendelea kuishawishi Serikali kuboresha maslahi na vitendea kazi vya Jeshi la Polisi ili Jeshi hilo liweze kufanya kazi zake kwa ufanisi.

Ufunguzi wa Kikao kazi hicho ulihudhriwa pia na Waziri Mkuu mstaafu Samweli Malechela, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana pamoja na baadhi ya wabunge na Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Dodoma.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAZIRI MWIGULU AHIMIZA UADILIFU POLISI
WAZIRI MWIGULU AHIMIZA UADILIFU POLISI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgBpXUSy-bHu2AVOSeQ4n-eOD8FEgcxnRXFLO2gMnzUAnBFi_X0DR9wKwLxFscSh6BGTQj4iClofJxjI6bEcEX_5SvjSMtSWelV8yZSIGcykhJ-TYeG2KXLYPFyGPy8554JmqTlN7jesWU/s640/1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgBpXUSy-bHu2AVOSeQ4n-eOD8FEgcxnRXFLO2gMnzUAnBFi_X0DR9wKwLxFscSh6BGTQj4iClofJxjI6bEcEX_5SvjSMtSWelV8yZSIGcykhJ-TYeG2KXLYPFyGPy8554JmqTlN7jesWU/s72-c/1.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/03/waziri-mwigulu-ahimiza-uadilifu-polisi.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/03/waziri-mwigulu-ahimiza-uadilifu-polisi.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy