Katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tawi la Miembeni lililopo Kata ya Manzese,Fatuma Moham...
Katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) Tawi la Miembeni lililopo Kata ya Manzese,Fatuma Mohamed
(kulia) akishirikiana na wanachama wa chama hicho kufanya usafi katika maeneo
mbalimbali ya mtaa wao kwa ajili ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani jijini
Dar es Salaam. PICHA ZOTE NA ELISA SHUNDA
Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)Tawi la Miembeni lililopo Kata ya Manzese wakishirikiana na wafanyakazi wa hospitali ya Mtakatifu Monica kuweka taka kwenye sehemu ya kuwekea uchafu kama ishara ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani jijini Dar es Salaam.
Wanachama wa UWT Tawi la Mtaa wa Miembeni Kata ya Manzese wakiwa ndani ya Hospitali ya Mtakatifu Monica iliyopo Manzesed Darajani kwa ajili ya kufanya usafi kama ishara ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani.
Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tawi hilo la Miembeni Manzese,Hanifa Mkura,akiongoza wakinamama wanachama wa chama hicho kufagia katika mazingira ya jengo la Hospitali ya Mtakatifu Monica iliyopo Manzese Darajani.
usafi ukiendelea...
Picha ya pamoja wakinamama wa UWT Tawi la Manzese Miembeni na wafanyakazi wa Hospitali ya Mtakatifu Monica iliyopo Manzese Darajani baada ya kufanya usafi.
NA ELISA SHUNDA,DAR
WITO umetolewa kwa wanawake kuwa mfano wa kuigwa kwa
jamii inayowazunguka katika ufanyaji wa usafi katika mazingira wanayoishi ili
kujikinga na magonjwa ya milipuko na yanayosababishwa na mazingira ya uchafu
ukiwemo ugonjwa wa Kipundupindu,kuhara na Malaria.
Hayo yamesemwa na Katibu wa Umoja wa Wanawake wa Chama
Cha Mapinduzi (CCM) Tawi la Mtaa wa Miembeni lililopo Kata ya Manzese jijini
Dar es Salaam jana,Fatuma Mohamed wakati akizungumza na waandishi wa habari
ambapo waliadhimisha siku ya wanawake duniani kwa kufanya usafi katika maeneo ya mtaa wao ikiwemo eneo
la ofisi za chama za mtaa huo pamoja na Hospitali ya Mtakatifu Monica iliyopo
eneo la Manzese Darajani.
“Leo sisi wanachama wa chama cha mapinduzi (CCM) UWT tawi
la Manzese Miembeni tumejitokeza kufanya usafi katika mitaa ya eneo letu hili
la Miembeni,ofisi za chama chetu za tawi pamoja na Hospitali ya Mtakatifu
Monica ili kuonyesha mfano na kuwahamasisha wakinamama wenzetu kufanya usafi
kwa kujitolea wenyewe bila ya kushurutishwa ili kujiepusha na magonjwa
nyemelezi na milipuko kama ugonjwa wa kipundupindu,kuhara hata na Malaria
yanayotokana na wadudu wanaozaliana sehemu za mitaro isiyotembea na takataka
zinazokaa kwa muda mrefu hivyo tumejitolea leo kufanya usafi ili mtaa wetu uwe
mfano wa kuigwa na mitaa mingine”Alisema Mohamed
Aidha Mohamed alisema kuwa wanaendelea kuhamasisha
wananchi wa mtaa wao na kata ya Manzese kwa ujumla kufanya usafi katika
mazingira yanayowazunguka lakini pia ni wajibu kwa kila mtu kufanya usafi
katika eneo lake pamoja na kutosahau siku ya juma la mwisho wa mwezi
lililowekwa na Rais Dk.John Magufuli la kufanya usafi katika mazingira yao.
Kwa upande wake Katibu Mwenezi wa Tawi hilo,Hanifa Mkura
alisema kuwa ni kweli kuna baadhi ya wananchi hata wakinamama wamekuwa wagumu
wa kushiriki kufanya usafi katika mazingira yao kutokana na hali jinsi ilivyo
kuwa ngumu wanakuwa wanajikita kufanya biashara zao ili wajipatie kipato lakini
wao kama wakinamama watawashauri wapange siku katika wiki wafanye usafi kwenye
mazingira yao yanayowazunguka.
COMMENTS