Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Nuru Milao akichangia mada katika kikao Kazi cha Maafisa Mawasil...
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Nuru Milao akichangia mada katika kikao Kazi
cha Maafisa Mawasiliano Serikalini kinachoendelea katika ukumbi wa
Hazina mkoani Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Dkt Hassan
Abbas.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Dkt.Hassan Abbas akichangia mada katika kikao Kazi
cha Maafisa Mawasiliano Serikalini kinachoendelea katika ukumbi wa
Hazina mkoani Dodoma. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,
Utamaduni Sanaa na Michezo, Nuru Milao.
Mtendaji
Mkuu Wakala wa Serikali Mtandao Dkt. Jabiri Bakari akitoa mada juu ya
hali halisi ya uhuishaji wa Taarifa za Serikali kwenye Tovuti Kuu ya
Serikali na Taasisi za Serikali katika Kikao Kazi cha Maafisa
Mawasiliano Serikalini kinachoendelea katika ukumbi wa Hazina mkoani
Dodoma.
Mkurugenzi
Msaidizi Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Idara ya Habari (Maelezo), Zamaradi Kawawa akichangia mada katika kikao Kazi cha Maafisa
Mawasiliano Serikalini kinachoendelea katika ukumbi wa Hazina mkoani
Dodoma.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano TBC, Edna Rajabu akichangia mada katika kikao Kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikalini kinachoendelea katika ukumbi wa Hazina mkoani Dodoma.
Afisa
Habari Mwandamizi Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Margareth Chambili
akichangia mada katika kikao Kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikalini
kinachoendelea katika ukumbi wa Hazina mkoani Dodoma.
Afisa
Habari Mwandamizi wa Tanesco Neema Mbuja
akichangia mada katika kikao Kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikalini
kinachoendelea katika ukumbi wa Hazina mkoani Dodoma.
Mkuu wa Kitengo cha Intelejensia ya kidigitali kutoka Kampuni ya Push Observer Kanali Mstaafu Dkt Abas Katalla akichangia mada katika kikao Kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikalini kinachoendelea katika ukumbi wa Hazina mkoani Dodoma. (Picha na Benjamin Sawe-Maelezo).
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.
Maafisa
Mawasiliano Serikalini wametakiwa kutumia tovuti za ofisi na tovuti kuu
ya Serikali kwa kuweka taarifa mbalimbali zinazohusu huduma na bidhaa
zinazotolewa na taasisi hizo ili kuwawezesha wananchi kuzifahamu huduma
hizo kirahisi.
Rai
hiyo imetolewa leo Mkoani Dodoma na Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali
Mtandao (EGA), Dkt. Jabir Bakari alipokuwa akitoa semina juu ya
matumizi na umuhimu wa tovuti za Serikali katika kikao kazi cha Maafisa
Mawasiliano Serikalini kinachoendelea Mkoani humo.
Dkt. Bakari amesema dhana ya Serikali Mtandao ni kuhuisha
matumizi ya TEHAMA kwenye utoaji wa taarifa mbalimbali za Serikali kwa
wananchi hivyo ni muhimu kwa kila taasisi kuwa na tovuti zenye taarifa
za uhakika na zinazoendana na wakati ili kurahisisha upatikanaji wa huduma hizo.
“Wakala
kwa kushirikiana na TAMISEMI pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo tumetengeneza mfumo unaotumia muda mfupi kwa taasisi za
Serikali kutengeneza tovuti zao ili ifikapo Juni mwaka huu taasisi zote
ziwe na tovuti zao zitakazowarahisisha wananchi kufahamu huduma
kirahisi,”alisema Dkt.Bakari.
Mtendaji
Mkuu huyo ameongeza kuwa tovuti za taasisi zisitumike tu katika kutoa
taarifa za huduma na bidhaa zao bali zitumike kuelezea mambo mengine
muhimu yanayofanywa na taasisi hizo.
Akielezea
kuhusu tovuti kuu ya Serikali, Dkt. Bakari amesema ni muhimu
kuhakikisha taarifa muhimu na za kudumu za taasisi husika zinawekwa ili
kusaidia wananchi kufahamu kiundani kazi wanazozifanya.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Mawasiliano (TAGCO),
Bw.Innocent Mungy amesema mbali na kuweka taarifa katika tovuti za
Serikali, ni wajibu wa Maafisa Mawasiliano Serikalini kutumia mitandao
ya kijamii kufikisha taarifa muhimu kwa wananchi .
“Kutokana
na maendeleo ya teknolojia duniani hasa katika upande wa mawasiliano,
matumizi ya mitandao ya kijamii yamekuwa yakileta tija kwa taasisi za
Umma kwani yanasaidia Serikali kujibu haraka hoja zinazowasumbua
wananchi”alisema Mungy.
Pia
aliwataka Maafisa Mawasiliano kuwa wabunifu katika kutumia mitandao ya
kijamii kwani mitandao hiyo inatoa fursa ya kushirikiana, kutangaza
huduma na bidhaa za taasisi, kufahamu matatizo ya wananchi.
COMMENTS