Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita akizungumza katika mkutano na wananchi wa mtaa wa Maweni wakati wa harambee ya kuchangish...
Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita akizungumza katika mkutano
na wananchi wa mtaa wa Maweni wakati wa harambee ya kuchangisha ujenzi
wa madarasa ya shule ya msingi ya Maweni iliyopo wilayani Kigamboni
jijini Dar es Salaam leo. Kushoto kwake ni Diwani wa Kata ya Mji
Mwema,Celestine Maufi (Chadema).
Diwani
wa Kata ya Mji Mwema,Celestine Maufi (Chadema) akizungumza katika
mkutano huo wa harambee ya uchangiaji wa ujenzi wa madarasa ya wanafunzi
wa shule hiyo. Kulia ni Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita.
NA CHRISTINA MWAGALA, Dar
MEYA wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita ameahidi kuchangia mifuko 100 ya Simenti pamoja na Mabati 100 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya msingi Maweni iliyopo Kata ya Mjimwema wilayani Kigamboni.
Shule hiyo ambayo inaupungufu mkubwa wa madarasa pamoja na uzio wa shule , inajumla ya wanafunzi 1300 ikiwemo na wale wenye ulemavu.
Akizungumza katika hafla hiyo ya chagizo kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa, Meya Isaya alisema kwamba hatua hiyo ni kwa jili ya kuzisaidia shule ambazo zinaupugufu wa madarasa ili kuwawezesha wanafunzi wasome katika mazingira salama.
Alisema kwamba wakati alipokuwa akiwania nafasi ya Udiwani Kwenye kata yake ya Vijibweni , na kisha kupata nafasi ya kuwa Meya wa jiji, moja ya vipaumbele vyake ilikuwa ni kuzisaidia shule ili kuondokana na changamoto ya wanafunzi kukaa.
“ Niseme tu kwamba jiji hili ambalo linarasilimali nyingi halafu wanafunzi wanakaa chini, sio jambo zuri, lazima watu ambao tumechaguliwa na wananchi ambao ndio wenye watoto wanasoma hapa, tutimize majukumu yetu” alisema Meya Isaya.
“ Kama kwenye Kata yako unaona kabisa wanafunzi wanakaa chini na wewe diwani upo, basi ujue huna sifa ya kuwa diwani na wananchi watakuwa na haki ya kukuondoa madarakani kwenye uchaguzi ujao.
Alifafanua kwamba” jambo la uchagiaji wa kusaidia wanafunzi wasikae chini sio la kisiasa bali ni katika sehemu ya kuwasaidia wananchi hivyo kuwataka wananchi kuondoa dhana ya kisiasa.
“ Hapa leo hii tukijenga madarasa kila motto anasoma akiwa amekaa kwenye madarasa mazuri, madawati ya kutosha, lakini watoto hao sio wa chadema, sio wa CCM wala CUF bali ni wananchi wote, nawaombeni sana kwenye suala la elimu tusilihusihwe na mambo ya siasa” alisema Meya Isaya.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Mjimwema, Celestine Maufi pamoja na mambo mengine alimpongeza Meya Isaya kwa kuunga mkono jitihada hizo zinazofanywa kwa ajili ya kujenga madarasa katika shule hiyo.
Hata hivyo Diwani huyo aliahidi kuchangia matofali 500 ,madawati 60 kwa ajili ya vyumba viwili vya madarasa .
Hata hivyo awali akisoma lisara kwa mgeni rasmi iliyoandaliwa na uongozi wa shule hiyo, Mwalimu Selemani alisema kwamba shule hiyo inakabiliwa na upungufu wa vyumba kadhaa vya madarasa ambapo vilivyopo havikidhi mahitaji ya wanafunzi waliopo.
Alifafanua kwamba kutokana na upungufu wa vyumba vya madarasa wananfunzi wenye ulemavu wamelazimika kusomea kwenye chumba cha darasa kimoja jambo ambalo linawapa shida walimu kwenye ufundishaji.
COMMENTS