Mrembo mwenye vipaji lukuki nchini, Jokate Mwegelo ameanzisha mpango maalum wa kufundisha somo la ujasiriamali kwa wanafunzi wa kid...

Mrembo
mwenye vipaji lukuki nchini, Jokate Mwegelo ameanzisha mpango maalum wa
kufundisha somo la ujasiriamali kwa wanafunzi wa kidato cha pili wa
shule ya sekondari ya Majani ya Chai iliyopo Vingunguti katika Manispaa
ya Ilala.
Jokate
ataanza mafunzo hayo maalum kwa wanafunzi wa kike kuanzia wiki ijayo na
lengo la mafunzo hayo ni kuwapa ufahamu wanafunzi hao na kuanzisha
biashara zao mara baada ya kumaliza elimu yao ya sekondari.
Alisema
kuwa mafunzo ya ujasiriamali kwa wanafunzi ni muhimu kwani
yanawawezesha kujiandaa vizuri kukabiliana na maisha mara baada ya
kuhitimu masomo yao ya sekondari na kushindwa kuendelea na masomo ya
ngazi ya juu.Kwa
mujibu wa Jokate, unaweza kusoma mpaka Chuo Kikuu ndani na nje ya nchi,
lakini bado utakabiliana na ugumu wa kupata ajira ambazo kwa sasa ni
haba.
“Kuna
wengine wamesomea taaluma fulani kwa ngazi ya Chuo Kikuu lakini mpaka
sasa hawana ajira na kukata tama katika maisha, pia unaweza kufanya kazi
tofauti na taaluma uliyosomea, lakini kwa ujasiriamali ni tofauti,
utajifunzi jinsi ya kupata mtaji, kukopa na kurejesha, kufanya biashara
gani na mbinu zake,”
“Mfano
halisi mimi mwenyewe, nimesomea mambo tofauti na kazi ninazozifanya ni
tofauti, ni mbunifu wa mitindo, mavazi, muigizaji wa filamu, mwanamuziki
na pia ni mfanyabiashara, haya yote sikusomea, ila najivunia kwani
ndiyo yanaendesha maisha yangu, wanafunzi wana vipawa tofauti, naamini
katika programu hii nitapata wengi na kupata mafanikio,” alisema Jokate.
Alisema
kuwa atakuwa anafundisha mafunzo hayo mara moja kwa wiki kuanzia wiki
ijayo. “Nimeamua kuanza rasmi siku ya wanawake duniani, maandalizi
yamekamilika na nawaomba wanafunzi wajiandae kwani mafunzo ni mazuri na
yatawajengea moyo wa kujiamini kwani si kila anayesoma anatakiwa
kuajiliwa,” alisema.
Jokate Mwegelo akicheza muziki na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Majani ya Chai ya Ilala wakati wa mahafari ya mwaka jana.
Jokate
Mwegelo akikabidhi zawadi kwa mmoja wa mwanafunzi wa shule ya sekondari
ya Majani ya Chai wakati wa maafali ya mwaka jana ya kidato cha nne.
COMMENTS