MBUNGE wa Nzega mjini Hussein Bashe, amesema Katibu Mkuu wa CCM, ndiye atakayezungumzia nini kiliwatokea yeye na wenzake...
MBUNGE
wa Nzega mjini Hussein Bashe, amesema Katibu Mkuu wa CCM, ndiye
atakayezungumzia nini kiliwatokea yeye na wenzake, Joseph Kasheku almaarufu
kama Msukuma na Adam Malima, aliyewahi kuwa Mbunge wa Mkuranga.
Bashe
na wenzake inadaiwa kuwa walikamatwa na polisi Machi 11, 2017 wakituhumiwa
kupanga njama za kuvuruga Mkutano Mkuu Maalum wa chama hicho unafanyika baadaye
leo kwenye Kituo cha Mikutano ch Kimataifa cha Dodoma.
Akihojiwa
na Televisheni ya Azam, leo Bashe alikataa kabisa kueleza kwa undani kama
habari za kukamatwa kwake ni za kweli na kwanini walikamatwa. “Katibu Mkuu
atalizungumzia hili, mimi, Joseph Msukuma na Adam Malima, Katibu Mkuu
atalizungumza.” Alijibu Bashe.
Adam Malima
Joseph Kasheku Msukuma
COMMENTS