Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi akizungumza na waandishi wa habari leo makao makuu ya o...
- Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi akizungumza na waandishi wa habari leo makao makuu ya ofisi hizo jijini Dar es Salaam akitoa utabiri wa msimu wa mvua za masika kuanzia mwezi Machi hadi Mei 2017.
- Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi akizungumza na waandishi wa habari leo makao makuu ya ofisi hizo jijini Dar es Salaam akitoa utabiri wa msimu wa mvua za masika kuanzia mwezi Machi hadi Mei 2017. Kushoto ni Meneja Kituo Kikuu cha Utabiri Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Samwel Mbuya pamoja na Mkurugenzi wa Utafiti wa TMA, Dk. Ladislaus Chang'a (kulia).
- Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi (kushoto na meza kuu) wakizungumza na waandishi wa habari leo makao makuu ya ofisi hizo jijini Dar es Salaam kutoa utabiri wa msimu wa mvua za masika kuanzia mwezi Machi hadi Mei 2017.
MKURUGENZI Mkuu
wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi leo ametoa
utabiri wa msimu wa mvua za masika kuanzia mwezi Machi hadi Mei 2017,
huku utabiri huo ukionesha uwezekano mkubwa wa mvua za wastani katika
maeneo mengi ya nchi. Dk. Kijazi ameongeza ya kuwa kutakuwa na
mtawanyiko hafifu wa mvua na vipindi virefu vya ukavu baadhi ya maeneo
katika kipindi cha msimu wa mvua wa Machi hadi Mei, 2017 hususan Nyanda
za Juu Kaskazini mashariki na Pwani ya Kaskazini.
Akizungumza
na wanahabari leo ofisi za TMA Dar es Salaam, Dk. Kijazi alisema maeneo
ya Nyanda za Juu Kaskazini-mashariki, Pwani ya Kaskazini na visiwa vya
unguja na Pemba ukanda wa ziwa Victoria pamoja na Kaskazini mwa Mkoa wa
Kigoma, kunatarajiwa kuwa na mvua za wastani hadi Juu ya Wastani.
Kwa
maeneo ya Pwani ya Kaskazini na Nyanda za Juu Kaskazini -Mashariki
yanatarajiwa kuwa na mvua za wastani hadi chini ya wastani, huku mvua
zinazoendelea kunyesha kwa sasa katika baadhi ya maeneo ya ukanda wa
Ziwa Victoria na Pwani ya Kaskazini zinatarajiwa kuungana na mvua za
msimu kabla ya kusambaa katika maeneo mengine wiki 1-2 ya mwezi Machi.
"..Vipindi
virefu vya ukavu vinatarajiwa kujitokeza baadhi ya maeneo ya Pwani ya
Kaskazini na nyanda za juu kaskazini mashariki. Matukio ya vimbunga
katika bahari ya Hindi yanatarajia kuchangia katika mwenendo wa msimu wa
mvua nchini.
- Baadhi ya wanahabari na maofisa wa TMA wakiwa katika mkutano na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi leo makao makuu ya ofisi hizo jijini Dar es Salaam alipokuwa akitoa utabiri wa msimu wa mvua za masika kuanzia mwezi Machi hadi Mei 2017.
- Meneja Kituo Kikuu cha Utabiri Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Samwel Mbuya (katikati) akifafanua jambo katika mkutano na waandishi wa habari leo makao makuu ya ofisi hizo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Kijazi pamoja na Mkurugenzi wa Utafiti wa TMA, Dk. Ladislaus Chang'a (kulia).
Kwa
upande wa Kanda ya Ziwa Victoria kwenye mikoa ya Kagera, Mara, Mwanza,
Geita, Simiyu pamoja na Shinyanga mvua zinazoendelea baadhi ya maeneo ya
Kagera na Mwanza zinatarajia kuungana na mvua za msimu na kusambaa
katika mikoa ya Geita, Mara, Simiyu na Shinyanga katika wiki ya 1-2 ya
mwezi Machi, 2017.
Mkurugenzi
huyo mkuu wa TMA, alisema maeneo ya Ukanda wa Pwani ya Kaskazini mikoa
ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani ya Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na
kaskazini mwa mkoa wa Morogoro mvua zinazoendelea kwa sasa (kwa
Dar/Pwani) zinatarajia kuungana na mvua za msimu na kusambaa katika
maeneo mengine ya Tanga, Visiwa vya Unguja na Pemba na kaskazini mwa
mkoa wa Morogoro wiki ya 1 na 2 ya mwezi Machi.
Alisema
kwa Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki inayojumuisha Mikoa ya
Kilimanjaro, Arusha na Manyara mvua katika maeneo haya zinatarajia
kuanza katika wiki 1-2 ya Mwezi Machi, 2017 huku zikiwa za wastani hadi
chini ya wastani. Pia vipindi virefu vya ukavu na mtawanyiko hafifu wa
mvua unatarajia katika baadhi ya maeneo.
Maeneo
yanayopata mvua za msimu mmoja, Magharibi mwa nchi, Kanda ya Kati,
Nyanda za Juu Kusini -Magharibi kusini mwa nchini na pwani ya Kusini;
kunatarajiwa kuwa na mvua za wastani katika maeneo mengi na juu ya
wastani katika maeneo ya mikoa ya Njombe, Songwe, Ruvuma, Mtwara na
Lindi pamoja na maeneo ya Morogoro Kusini Mahenge.
Kanda
ya Magharibi Mikoa ya Kigoma, Tabora, Katavi na Rukwa kwa ujumla
inataraji kuwa na mvua za wastani hadi juu ya wastani na zitaishia Mwezi
wa Aprili. Maeneo ya Kanda ya Kati mikoa ya Singida na Dodoma mvua za
msimu zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo
mengi huku zikitegemewa kuishia wiki ya 2-3 ya mwezi Aprili, 2017.
- Baadhi ya wanahabari na maofisa wa TMA wakiwa katika mkutano na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi leo makao makuu ya ofisi hizo jijini Dar es Salaam alipokuwa akitoa utabiri wa msimu wa mvua za masika kuanzia mwezi Machi hadi Mei 2017.
Maeneo
ya Nyanda za Juu Kusini Magharibi, mikoa ya Mbeya, Songwe, Irinda,
Njombe na Morogoro Kusini mvua zinatarajiwa kuisha wiki ya nne ya mwezi
Aprili, Huku maeneo ya Kusini na Pwani ya Kusini, mikoa ya Ruvuma, Lindi
na Mtwara mvua zinatarajiwa kuwa za juu ya wastani hadi wastani katika
maeneo mengi isipokuwa maeneo ya kaskazini mwa mkoa wa Lindi yatakuwa na
mvua za wastani hadi juu ya wastani.
Aidha
akitoa ushauri katika sekta ya afya, Dk. Kijazi alisema huenda kukawa
na uhaba wa maji salama kwa shughuli za binadamu ikiwemo usafi, hivyo
wananchi wanashauriwa kuchukua hatua stahiki ili kuzuia milipuko ya
magonjwa. Hata hivyo amewashauri wadau wa sekta ya afya pamoja na umma
kuchukua hatua kupunguza athari zinazoweza kujitokeza.
COMMENTS