Na Ismail Ngayonga MAELEZO MAAFISA Habari na Mawasiliano katika sekretarieti za Mikoa na Wilaya nchini wametakiwa kujitokeza na k...
Na Ismail Ngayonga MAELEZO
MAAFISA Habari na Mawasiliano katika sekretarieti za Mikoa na Wilaya nchini wametakiwa kujitokeza na kuwajibika kikamilifu katika maeneo yao ya kazi ili waajiri wao kuweza kufahamu kwa ufasaha wajibu na majukumu yao ili waweze kuisadia Serikali na wananchi.
Rai hiyo, imetolewa leo Jijini Mwanza na Mkurugenzi wa Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas wakati alipokuwa akizugnumza na Maafisa Habari na TEHAMA katika mafunzo elekezi ya tovuti yanayofadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani (USAID) na kusimamiwa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na Wakala ya Serikali Mtandao (EGA).
Kwa Mujibu wa Dkt. Abbas alisema katika ulimwengu wa sasa suala la teknolojia ni jambo lisiloupekika, hivyo Serikali itaweka utaratibu maalum wa kuwapima Maafisa Habari ili kufahamu aina ya taarifa ziliwowekwa katika tovuti hizo zinavyoweza kumsaidia mwananchi..
“Zipo taarifa za miradi mbalimbali ambayo Serikali imeifanya, taarifa za bajeti za halmashauri na mikoa zote hizi mwananchi atnapenda kuzifahamu, hivyo ni wajibu wenu Maafisa Habari kuweka taarifa hizi” alisema Dkt. Abbas
Aidha aliongeza kuwa ni wajibu wa kila Afisa Habari aliyopo katika Mkoa na Halmashauri nchini aweze kujiwekea malengo ya utekelezaji ili aweze kujitafakari kwa kuwa kuwa kupitia malengo hayo ataweza kutatua changamoto mbalimbali zinazomkabili katika eneo lake la kazi.
Akifafanua zaidi Dkt Abbas alisema ili kufikia malengo hayo ni hawana budi Maafisa Habari kutengeneza mtandao wa mawasiliano baina yao ili kuwawezesha kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili katika maeneo yao ya kazi.
Dkt. Abbas alisema Serikali inatambua changamoto mbalimbali zinazowakabili maafisa Habari katika maeneo yo ya kazi, ambapo baadhi ya kazi yameanza kupatiwa ufumbuzi ikiwemo suala la miongozo ya iliyotolewa katika miaka ya nyuma kuhusu majukumu ya Maafisa Habari taasisi za Umma.
Kwa Upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Ofisi ya Rais- TAMISEMI, Rebbeca Kwandu alisema katika mafunzo hayo yaliyotolewa kwa Maafisa Habari na TEHAMA yatasaidia kujibu hoja mbalimbali za wananchi zilizokuwa zikiwasilshwa katika Halmashauri mbalimbali nchini.
“Afisa Habari atakuwa ndiye mhusika wa karibu zaidi kuhusu maudhui ya tovti hizi lakini Afisa TEHAMA yeye atawajibika kwa kiasi kikubwa na masuala ya kiufundi zaidi” alisema Kwandu.
Naye Afisa Habari wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, John Mlyambato alisema baadhi ya Mikoa nchini ikiwemo Mkoa wa Tabora hauna watumishi wa kada ya Maafisa Habari, hatua inayosababisha taarifa mbalimbali zisiweze kuwafikia wananchi pamja.
Aidha aliongeza kuwa katika baadhi ya halmashauri nchini wakuu wengi wa vitengo vingi vya habari katika halmashauri hizo wanakaimu vitengo hivyo, hivyo ni wajibu wa Serikali kuhakikisha kuwa watumishi wa kada hiyo wanaweza kupatikana.
COMMENTS