Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama amesema kuwa Serikali im...
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu)
Mhe. Jenista Mhagama amesema kuwa Serikali imejipanga kusaidia
vijana kutambua na kuchangamkia fursa mbalimbali za ajira zilizopo
nchini ili kutatua changamoto ya ukosefu wa ajira na kutimiza adhma
ya kuleta maendeleo hususani kwa vijana.
Mhe.
Mhagama ameyasema hayo jana wakati akijibu hoja ya Mbunge wa Kinondoni
Mhe. Maulid Mtulia iliyohoji juu ya jitihada za Serikali katika kutatua
tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana wakati wa Mkutano wa Tano wa Bunge
unaoendelea Mkoani Dodoma.
Katika
Mkutano huo Mhe. Waziri alisisitiza kuwa Serikali ina mipango na
mikakati madhubuti inayokusudiwa yakusaidia vijana wa Kitanzania
ili kujiletea maendeleo yao wenyewe na kuondokana na umasikini.
“Serikali
ya Awamu ya Tano imeendelea kuweka mikakati ikiwemo uwanzishwaji wa
programu mbalimbali zitakazo saidia kutatua changamoto ya ajira kwa
vijana kwa kuangalia matokeo ya tafiti mbalimbali ambazo zimepelekea
kuwa na programu zinazolenga kukabili tatizo la ukosefu wa ajira kwa
vijana” Alisema Waziri
Alisisitiza
kuwa programu hizo ni pamoja na; kurasmisha ujuzi usio rasmi kuwa
rasmi, mfumo wa mafunzo kwa vitendo, mfumo wa uanangezi pamoja na kukuza
mafunzo kwa watanzania kulingana na soko lililopo kwa sasa.
Pamoja
na juhudi hizo zinazotarajiwa kuzaa matunda bado Waziri aliwatoa hofu
wananchi wote kwa kuwepo kwa fursa hizo za ajira zitakazo jali hali za
watu pasipo kuangalia makabila yao, rangi wala dini.
“Katika
kutatua changamoto ya ajira kwa vijana hatuta angalia kabila, rangi
wala dini ya mtu bali kutakuwa na haki na usawa”.Alisisitiza Waziri
Aliongezea
kuwa, Serikali pia inajitihada za kuvutia uwekezaji kwenye sekta
mbalimbali na urasimishaji wa sekta isiyo rasmi ili kupunguza kiwango
cha ukosefu wa ajira.
“Serikali
itatumia sekta zenye uwezo wa kutoa ajira kwa wingi ikiwemo zile za
Kilimo, majenzi, Mawasiliano na Utalii ili kuzitumia kuweka mazingira
mazuri kwa vijana kupata fursa za ajira”.
Mhe.
Mhagama alisisitizia bungeni kuwa kutokana na tafiti mbalimbali
zilizofanyika zitatumika kama chachu ya kuangalia maeneo yanayohitaji
kusaidia kwa haraka na kupunguza changamoto hiyo kwa vijana.
“Kwa
kuangalia tafiti ya Hali ya Ajira Nchini ya mwaka 2014 imeonesha kuwa
kiwango cha ukosefu wa ajira kimepungua kutoka asilimia 11.7 mwaka 2006
hadi asilimia 10.3 mwaka 2014 na ukosefu wa ajira kwa vijana umepungua kutoka asilimia 14.2 mwaka 2006 hadi asilimia 11.7 mwaka 2014”,alisema.
Hata
hivyo, Waziri Mhagama alieleza kuwa pamoja na jitihada hizo Serikali
bado ina wajibu wa kuongeza jitihada zaidi ili kuongeza kasi ya
upatikanaji wa ajira na kuboresha maisha ya vijana.
COMMENTS