JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU Simu: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: press@ikulu.go.tz To...
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Faksi: 255-22-2113425 |
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 26 Februari, 2017 amemteua Bw. Omary Rashid Nundu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL).
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Bw. Omary Rashid Nundu umeanza tarehe 24 Februari, 2017.
Bw. Omary Rashid Nundu anachukua nafasi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL Prof. Tolly Salvatory Augustine Mbwete.
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemuapisha Thobias Emir Andengenye kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Kamishna Jenerali Thobias Emir Andengenye anachukua nafasi ya Kamishna Jenerali Pius M. Nyambacha ambaye amestaafu.
Pia, Mhe. Rais Magufuli amewaapisha Mabalozi wanne walioteuliwa kuiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali kama ifuatavyo;
Mhe. Dkt. Pindi Hazara Chana ameapishwa kuwa Balozi wa Tanzania Nairobi, Kenya ambako anachukua nafasi ya Mhe. John Haule ambaye amestaafu.
Mhe. Silima Kombo Haji ameapishwa kuwa Balozi wa Tanzania Khartoum, Sudan ambako anakwenda kufungua Ubalozi.
Mhe. Abdallah Abas Kilima ameapishwa kuwa Balozi wa Tanzania Muscat, Oman ambako anachukua nafasi ya Mhe. Ali Ahamed Saleh ambaye amestaafu.
Mhe. Matilda Swila Masuka ameapishwa kuwa Balozi wa Tanzania Seoul, Korea Kusini ambako anakwenda kufungua Ubalozi mpya
Aidha Mhe. Rais Magufuli ameshuhudia Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Mabalozi wote wanne wakila kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa umma kilichoongozwa na Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji Mstaafu Harold Nsekela.
Hafla ya kuapishwa kwa viongozi hao imehudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
26 Februari, 2017.
![]() |
Omary Nundu. |
COMMENTS