Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO Dkt. Hassan Abbasi akitangaza mkusanyiko huo kuwa mahafali ya 20 ya Chuo cha Uandishi wa...
Mkurugenzi
wa Idara ya Habari-MAELEZO Dkt. Hassan Abbasi akitangaza mkusanyiko huo
kuwa mahafali ya 20 ya Chuo cha Uandishi wa Habari Morogoro (MSJ) kulia
ni Mkuu wa Chuo cha Uandishi wa Habari Morogoro (MSJ) Bw. Augustino
Nongwe wakati wa mahafali ya 20 ya chuo leo Mjini Morogoro.

Baadhi ya wahitimu wakiwa katika mahafali hayo.

Mhitimu
katika Chuo cha Uandishi wa Habari Morogoro (MSJ) Elias Eliakim akisoma
risala kwa Mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO
Dkt. Hassan Abbasi ambapo mbali na mambo mengine aliomba viongozi wa
Serikali kuweka utaratibu wa kutembelea vyuo vya kati vya uandishi wa
habari ili kujenga hamasa kwa wanafunzi.

Mkurugenzi
wa Idara ya Habari-MAELEZO Dkt. Hassan Abbasi akiongea na wahitimu wa
Chuo cha Uandishi wa Habari Morogoro (MSJ) ambapo alisisitiza umuhimu wa
wanatasnia ya habari kuwa watendaji na sio waongeaji bila vitendo ikiwa
ni moja ya mkakati wa kuikuza tasnia hii na kuendana na Sheria mpya ya
Huduma za Habari wakati wa mahafali ya 20 ya chuo leo Mjini Morogoro.

Mkurugenzi
wa Idara ya Habari-MAELEZO Dkt. Hassan Abbasi akiwapa vyeti vya uhitimu
wa Diploma na cheti katika uandishi wa habari waliokuwa wanafunzi wa
Chuo cha Uandishi wa Habari Morogoro (MSJ)
Mkurugenzi
wa Idara ya Habari-MAELEZO Dkt. Hassan Abbasi akiwa katika picha ya
pamoja wahitimu,wafanyakazi wa Chuo cha Uandishi wa Habari Morogoro
(MSJ) wakati wa mahafali ya 20 ya chuo leo Mjini Morogoro.
PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO.
COMMENTS