Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Fortunatus Kapinga, akizungumza wakati akimkaribisha Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika ...
Postamasta
Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Fortunatus Kapinga,
akizungumza wakati akimkaribisha Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika hilo, Dk.
Haruni Kondo (katikati), kuzungumza na waandishi wa habari, Makao Makuu
ya shirika, Dar es Salaam jana. Kulia ni Kaimu Katibu wa shirika hilo,
Zuhura Pinde. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com )
Mwenyekiti
wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania, Dk. Haruni Kondo (katikati),
akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, kuhusu uamuzi wa
bodi hiyo, kuwaondoa katika nafasi zao viongozi wanne waandamizi na
nafasi zao kuchukuliwa na wafanyakazi wengine kutokana na kile
alichokieleza kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo kwa ajili ya
kuliletea tija shirika hilo, lililotetereka kutokana na kile
kilichoelezwa kuwa ni hujuma kutoka kwa baadhi ya wafanyakazi wake.
Kushoto ni Postamasta Mkuu, Fortunatus Kapinga na kulia ni Kaimu Katibu
wa Shirika, Zuhura Pinde.
Mmoja wa wafanyakazi walioteuliwa na Bodi ya Shirika hilo kukaimu moja ya nafasi zilizowazi ya Meneja Mkuu Menejimenti ya Rasilimali za Shirika, Macrice Mbodo (kuli), akiwa katika mkutano huo. Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Usalama ya shirika hilo, George Mwamgabe.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania. Dk. Haruni Kondo, akizungumza na
waandishi wa habari, waki wa mkutano huo. Kushoto ni Postamasta Mkuu,
Fortunatus Kapinga.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania, Dk. Haruni Kondo (katikati),
akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, alipozungumza kuhusu uamuzi wa
bodi hiyo, kuwaondoa katika nafasi zao viongozi wanne waandamizi na
nafasi zao kuchukuliwa na wafanyakazi wengine kutokana na kile
alichokieleza kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo kwa ajili ya
kuliletea tija shirika hilo, lililotetereka kutokana na kile
kilichoelezwa kuwa ni hujuma kutoka kwa baadhi ya wafanyakazi wake.
Kushoto ni Postamasta Mkuu, Fortunatus Kapinga na kulia ni Kaimu Katibu
wa Shirika, Zuhura Pinde.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania, Dk. Haruni Kondo (kulia), akifafanua jambo katika mkutano huo.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania. Dk. Haruni Kondo, akisisitiza
jambo, wakati akizungumza na waandishi wa habari, jijini jana kuhusu
uamuzi ulifikiwa na bodi hiyo.
Baadhi ya viongozi wa Shirika la Posta Tanzania wakiwa katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania, Dk. Haruni Kondo (wa pili kulia), akizungumza katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania, Dk. Haruni Kondo, akijibu maswali ya waandishi wa habari katika mkutano huo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania, Dk. Haruni Kondo.
Baadhi
ya waandishi wa habari wakiwa kazini wakichukua taarifa hiyo, iliyokuwa
ikitolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania, Dk.
Haruni Kondo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania, Dk. Haruni Kondo (kulia), akimtambulisha kwa waandishi wa habari, Kaimu Meneja Mkuu Menejimenti ya Rasilimali za Shirika, Macrice Mbodo.
Kaimu Meneja Mkuu Menejimenti ya Rasilimali za Shirika, Macrice Mbodo, aliyetambulishwa kwa waandishi wa habari.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania, Dk. Haruni Kondo, akielezea
jambo, wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari katika mkutano huo.
Postamasta
Mkuu, Fortunatus Kapinga, akijibu maswali ya waandishi wa habari kuhusu
ni jinsi gani wanavyokabiliana na matatizo ya upitishwaji dawa za
kulevya kwa mfumo wa vifurushi kwenye shirika hilo.
Taarifa kamili ya bodi hiyo kama ilivyowasilishwa na Mwenyekiti wake, Dk. Haruni Kondo jijini Dar es Salaam jana.
SHIRIKA LA POSTA TANZANIA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI MKUTANO ULIFANYIKA KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO WA POSTA HOUSE
TAREHE 25 FEBRUARI, 2017
Kwa
kuzingatia maendeleo ya mageuzi makubwa yanayojitokeza katika sekta ya
mawasiliano, Shirika la Posta Tanzania kama mtoa huduma kwa umma (Public
Postal Operator), linawajibika kuhakikisha kuwa huduma za kisasa
zinazozingatia vigezo vya ubora, usalama, uadilifu katika utendaji na
uwajibikaji zinawafikia watu wengi zaidi katika maeneo yote ya nchi.
Kwa hivi sasa Bodi ya Wakurugenzi pamoja na Menejimenti imechukua hatua katika maeneo yafuatayo:-
1) KUPAMBANA NA UHALIFU WA MADAWA YA KULEVYA.
Shirika
la Posta Tanzania limechukua hatua kadhaa ili kuhakikisha linashiriki
na kuchangia kikamilifu jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano za
kupambana na uhalifu, ikiwa ni pamoja na usafirishaji, uuzaji na
utumiaji wa madawa ya kulevya, usafirishaji na utakatishaji wa fedha
haramu, ugaidi, udanganyifu katika utambulisho pamoja na uhalifu
mwingine wa kimtandao wa Kitaifa na Kimataifa.
Bodi
ya Wakurugenzi ya Shirika imedhamiria kuongeza msukumo na kasi ya
usimamizi ili kupambana na uhalifu huu ambao una madhara makubwa kwa
jamii.
Hatua
mojawapo zilizochukuliwa na Shirika ni kusimika mfumo wa kisasa wa
kudhibiti usalama na kurahisisha utambuzi wa vitu na matukio hatarishi
na haramu yanayopitishwa au kujitokeza kupitia mtandao wa Shirika.
Mfumo
huu uliogharimu zaidi ya shilingi milioni mia mbili (200) ambao
unajumuisha ufungaji wa kamera za kiusalama (CCTV) katika Posta Kuu ya
Dar es Salaam, tayari mzabuni aliyeusimika ameshakamilisha kazi yake na
ataukabidhi kwa Shirika wiki ijayo na utazinduliwa rasmi wakati wowote
kuanzia hapo.
Aidha,
tumesimika mifumo ya kisasa ya kiusalama ikiwa ni pamoja na mashini za
ukaguzi wa mizigo (baggage scanners) katika Ofisi zenye uwezekano wa
kuwa uchochoro wa uhalifu wa aina hii ikiwa ni pamoja na Ofisi za
Zanzibar, Kigoma, Dar es Salaam na Arusha.
Hatua
hii imechukuliwa kwa kuzingatia kuwa matukio ya uhalifu uliopangwa
(organized crimes) yamekuwa ni changamoto kubwa kwa Mashirika ya Posta
Duniani na hivyo tumedhamiria kuhakikisha kuwa, mtandao wa Shirika wa
Kitaifa sio uchochoro wa uhalifu huu.
Vitu
visivyoruhusiwa kusafirishwa katika mtandao wa Posta kwa mujibu wa
sheria ni pamoja na madawa ya kulevya, bidhaa za kemikali zenye sumu,
silaha za moto na milipuko, wanyama hai, nyara za Serikali, vifaa vya
mionzi, vyakula vinavyooza, betri za aina mbalimbali, vimiminika, fedha
haramu, utakatishaji wa fedha na vitu vyovyote hatarishi.
Katazo
la vitu hivi kusafirishwa katika mtandao wa Posta limezingatiwa katika
sheria na taratibu mbalimbali za Kitaifa ikiwa ni pamoja na sheria ya
Mawasiliano ya Elektroniki na Posta (EPOCA) ya mwaka 2010, Umoja wa
Posta Duniani (UPU), Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO) na
Shirika la Forodha Duniani (WCO).
Kwahiyo,
Shirika la Posta Tanzania kwa kushirikiana na vyombo vingine vya
usimamizi wa sheria, kwa hivi sasa limeimarisha uhakiki wa mifumo yake
na pia ukaguzi wa barua, vifurushi, vipeto na mizigo ili kujiridhisha
juu ya usalama na uzingatiaji wa sheria.
2) UANZISHWAJI WA JAMII CENTRE
Hatua nyingine iliyochukuliwa ni uanzishwaji wa kituo cha kisasa cha huduma ya Jamii Centre katika Posta Kuu ya Dar es Salaam iliyoko mtaa wa Azikiwe.
Maandalizi
ya Ofisi ikiwa ni kaunta za kutolea huduma, mifumo ya mawasiliano,
samani kwa wateja, mafunzo ya wahudumu na vifaa vya kazi tayari
vimefungwa ili vitumike na kituo kiko tayari kwa uzinduzi, wakati wowote
kuanzia sasa.
Kituo
kinatoa huduma jumuishi za kimtandao katika sehemu moja (One Stop
Community Centre) ili kuwapunguzia wananchi usumbufu wa kufuata huduma
hizo maeneo mbalimbali tofauti.
Huduma zinazotolewa ‘on-line’ kwa sasa ni pamoja na:-
Ø Malipo ya wastaafu (NSSF)
Ø Malipo ya gawio (dividends) za makampuni mbalimbali
Ø Malipo ya usajili wa Baraza la Mitihani
Ø Huduma za kibenki- CRDB
Ø Moneygram
Ø Maxmalipo (Road lincense), Luku, Ving’amuzi n.k
Ø Huduma mbalimbali za Posta.
Bodi
imeelekeza Menejimenti kuendelea na ushawishi kwa makampuni na taasisi
nyingine kama RITA, NHIF, NIDA, Mabenki n.k ili kujiunga na mfumo huu wa
kisasa. Hapo baadae zichukuliwe hatua za kufungua vituo vingine katika
miji/mikoa ya Zanzibar, Dodoma, Mbeya, Mwanza, Arusha na Morogoro kabla
kufikia mwisho wa 2017.
3) USIMAMIZI WA KADA ZA UONGOZI NA RASILIMALI WATU
Baada
ya Bodi kufanya tathmini yake juu ya utendaji wa Wafanyakazi wa
Shirika, imeelekeza Menejimenti ichukue hatua stahiki kwa kada zote za
Wafanyakazi kuanzia hapa Makao Makuu, Zanzibar, Mikoani, Wilayani hadi
Vijijini.
Bodi
inatambua kuwa ufanisi wa Shirika hili utatokana na utendaji wa
Rasilimali watu iliyopo. Kwa hivi sasa Shirika lina Wafanyakazi wenye
ajira ya kudumu wapatao 1,082 hadi kufikia Disemba 2016 lakini, baadhi
yao wanafanya kazi kwa mazoea na lazima sasa wabadilike.
Menejimenti
iendelee kusimamia uwajibikaji wa Viongozi na Watumishi wa kada zote
ndani ya Shirika ili kujenga nidhamu ya kazi, kujituma, kuheshimu kanuni
na taratibu, kuongeza ubunifu na kufanya kazi kwa ufanisi wenye tija
kwa Shirika.
Bodi
inatambua jitihada za Menejimenti za kuwa na mkakati wa kuimarisha
usimamizi na udhibiti wa nidhamu za Wafanyakazi hususani katika
kuwaongezea uwezo, kutokana na mafunzo wanayopewa kulingana na uhitaji
wa soko, utii, uaminifu na hamasa katika utendaji wa kazi.
Ili
kuthibitisha hilo, Wafanyakazi wanapoajiriwa wanakula viapo vya utii na
kutunza siri katika utendaji kazi wao na tunapenda kuendelea kuajiri
Wafanyakazi wenye uwezo na fuzu sahihi ili kuendana na mabadiliko ya
soko na Wafanyakazi waendelee kupewa mafunzo ya mara kwa mara ili
kuongeza ufanisi na dhana ya kumjali mteja.
Aidha,
kwa wakati huu kuna mwelekeo mzuri kwani Shirika limeanza kuwapima
Wafanyakazi kwa kutumia mfumo wazi wa kazi (OPRAS) kwa kuanzia mwaka huu
wa fedha 2016/2017, na itakapobainika kuwa wapo Wafanyakazi ambao
hawakufikia viwango vya utendaji lazima wawajibishwe.
Kwa
kuzingatia yote hayo, katika kikao chake cha jana tarehe 24/2/2017
Bodi ilipitia kwa makini utendaji, uwajibikaji na nidhamu na uwezo wa
watendaji wakuu katika Shirika hilo ambao wanatakiwa kuwa mfano bora wa
uongozi wa utendaji mzuri .
Imebainika
na kujiridhisha kuwa baadhi ya watendaji wakuu Makao Makuu ya Posta
wamekuwa kikwazo katika dhana ya uwajibikaji, weledi, na kujituma katika
kutekeleza wajibu na majukumu yao ili kulifanya Shirika la Posta kuwa
mfano bora wa Mashirika yenye ubora katika kutoa huduma.
Aidha,
kuna baadhi ya vitendo kwa baadhi ya watendaji vinadhihirisha tabia ya
umangimeza, urasimu, kufanya kazi kwa mazoea ubadhirifu na wizi.
Bodi imeamua kufanya mabadiliko ya uongozi wa juu wa Shirika la Posta kwa kutengua nafasi za watendaji wakuu:
1) Meneja Mkuu Menejimenti ya ya Rasilimali za Shirika Ndg. James M. Sando na kumteua Ndugu Macrice Mbodo kukaimu nafasi hiyo.
2) Meneja Mkuu uendeshaji wa Biashara Bi. Janeth Msofe na kumteua aliyekuwa Meneja Mkoa Shinyanga Ndugu. Hassan Mwang’ombe.
3) Imemsimamisha kazi Ndugu. Jasson Kalile aliyekuwa Meneja Msaidizi Mail and Logistic.
4) Imemsimamisha Kazi Ndugu Ambrose John aliyekuwa Senior Motor Transport Officer.
IMETOLEWA NA:-
MWENYEKITI
BODI YA WAKURUGENZI
SHIRIKA LA POSTA TANZANIA
DAR ES SALAAM
COMMENTS