WANASHERIA OFISI YA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM WAJIUNGA NA PSPF
HomeJamii

WANASHERIA OFISI YA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM WAJIUNGA NA PSPF

  Afisa Uendeshaji wa PSPF, Hadji Hamisi Jamadari, akitoa ufafanuaiz kuhusu kazi zifanywazo na Mfuko huo, hususan uchangiaji wa...

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA MWAKILISHI MKAZI WA BENKI YA DUNIA, AENDESHA BARAZA LA MAWAZIRI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO
BOHARI YA DAWA (MSD) YAPONGEZWA KWA USAMBAZAJI WA DAWA NCHINI
ZIARA YA NAIBU WAZIRI MHANDISI MASAUNI NA WAZIRI BARANDAGIYE WA BURUNDI KATIKA KAMBI ZA WAKIMBIZI NDUTA NA MTENDELI MKOANI KIGOMA








 Afisa Uendeshaji wa PSPF, Hadji Hamisi Jamadari, akitoa ufafanuaiz kuhusu kazi zifanywazo na Mfuko huo, hususan uchangiaji wa hiari, (PSS), mwishoni mwa seina ya mafunzo ya siku mbili, kwa watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kitengo cha sheria, iliyomalizika leo Januari 4, 2017. Baada ya semina hiyo wanasheria hao zaidi ya 35 walijiunga na Mfuko huo kupitia mpangio huo wa PSS.




NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
WATUMISHI wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kitengo cha sheria, wamejiunga na Mfuko wa Pensheni wa PSPF baada ya kuhudhuria semina ya mafunzo ya siku mbili
iliyomalizika leo Januari 4, 2017.
Semina hiyo iliandaliwa na Mfuko huo kufuatia ombi la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makodna, kutaka wanasheria wa ofisi yake, wapewe semina ili kuwajengea
uwezo wa kutatua kero za wananchi ambao ni wanachama wa Mfuko huo watakaofika Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa kwa shida zinazohusiana na masuala ya Mafao na
Pensheni.
Katika semina hiyo iliyoanza Januari 3, 2017, wanasheria hao walipatiwa ufafanuzi wa kina kuhusu shughuli namajukumu yanayotekelezwa na PSPF. Meneja
wa PSPF huduma kwa wateja, Bi.Leila Magimbi, alitaja majukumu hayo kuwa ni pamoja na  kutambua na kusajili wanachama
wapya, kukusanyan michango na kutunza taarifa za michango ya wanachama, kuwekeza michango katika vitegauchumi mbalimbali na kulipa mafao.
Shughuli nyingine zinazotekelezwa na Mfuko huo ni kulipa mafao kwa wanaostahili kwa mujibu wa sheria, kutunza kumbukumbu za wanachama na wastaafu, kuangalia upya
ubora wa mafao na kufanya tathmini ya Mfuko na kuweka mikakati endelevu, aliongeza Bi. Magimbi.
Pia wanasheria hao walipata fursa ya kuelezwa aina za wanachama wa PSPF ambao ni Watumishi wa Umma, sekta binafsi ambao hawa watachangia katika mfumo wa uchangiaji wa lazima na watu wote walio katika sekta isiyo rasmi, ambao wao
watachangia katika Mfumo wa uchangiaji wa Hiari.
Aidha faina apatazo mwanachama wa PSPF, kwa mujibu wa Kaimu Meneja Mafao, Bw. Haji Moshi, ni pamoja na Fao la uzazi, mkopo wa elimu, mkopo kwa mwajiriwa mpya,
mikopo ya viwanja, mikopo ya nyumba, mkopo wa fedha taslimu, mikopo kwa wastaafu yenye masharti nafuu, mafao ya muda mrefu, fao la ulemavu, fao la mirathi, fao la kufukuzwa au kuachishwa kazi, na bima ya afya.
Akifunga semina hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, amewataka wanasheria hao kutumia busara wanapohudumia wananchi kwani kwa kufanya hivyo itawasaidia
kurahisisha utoaji huduma kwa wananchi kama ilivyokusudiwa.
“Huko mtakutana na watu wa aina mbalimbali, wengine wamesoma zaidi yenu, wengine hawakupata fursa ya kusoma kama nyinyi, kwa hivyo mnao wajibu wa kutunmia
busara katika kuhudumia wananchi wa kada tofauti tofauti.” Aliwaasa Bw. Mayingu.
Aidha mwakilishi wa wanasheria hao, Bi.Georgia Ephraim Kamina, amesema semina hiyo imekuwa na manufaa makubwa kwao, na kuishukuru PSPF kwa kuandaa semina hiyo na
kuuomba uongozi wa Mfuko, kujenga mahusiano ya kudumu baina ya Mfuko na wanasheria hao katika utendaji kazi wao wa kuhudumia wananchi.


Afisa Masoko Mwandamizi wa PSPF, Bw. Magira Werema, akifafanua masuala kadhaa yahusuyo shughuli za Mfuko na faida zake kwa wanachama.

 Afisa wa idara ya Pensehni ya Mafao wa PSPF, Bw.Andrew Dayson akitoa mada.

 Kaimu Meneja wa Uchangiaji wa Hiari (PSS), wa Mfuko huo, Bi.Sophia Mbilikira, akielezea faida za kuwa mwanachama kupitia uchangiaji wa hiari.
 Baadhi ya washiriki (wanasheria), wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa na wataalamu wa PSPF.

 Baada ya kuelewa "somo" hatimaye ilifika wakati wa wanasheria hao kujiunga na Mpango wa uchangiaji wa Hiari (PSS), na hapa wanajaza fomu.




 Obote Simon, akikabidhiwa kadi ya kujiunga na uanachama wa PSPF, kupitia mpango wa PSS, kutoka kwa Kaimu Meneja wa PSS, Bi. Sophia Mbilikira.

 Bw. Mahfoudh K. Mohammed (kushoto), akipokea kadi yake.

 Bw. Emmanuel S. Nyanza, (kushoto), akipokea kadi yake.

 Bw. Albert Nyange, (kushoto), akipokea kadi yake.

 Kongozi wa Wanasheria wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Georgia Sphraim Kamina, akizungumza
 Bi. Kissa, akiuliza swali kuhusu mikopo ya elimu.



 Meneja Masoko na Uhusiano wa PSPF, Bi. Costantina Martin, (kulia), akiwa amejiungana wanasemina wakati semina hiyo ikielekea ukingoni.




 Sehemu ya utunzaji nyaraka kwenye mfumo wa makabati yanayoendeshwa kielektroniki.



 Msaidizi maalum wa Mkuu wa Mkoa wa Dares Salaam, Bw. Daniel P. Jenga, (kushoto), akifurahia kuonyeshwa faili lake ndani ya dakika moja.

 Afisa wa PSPF akiwa kazini.

 Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu akitoa nasaha zake wakati wa kufunga semina hiyo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma na uendeshaji, Bi. Neema Muro.

 Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu akitoa nasaha zake mbele ya wanasemina hao wakati wa kufunga semina hiyo.

 Wanasemina wakitembelea kitengo cha kutunza kumbukumbu cha PSPF.



 Meneja Huduma kwa Wateja, PSPF, Bi. Leila Magimbi.


Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WANASHERIA OFISI YA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM WAJIUNGA NA PSPF
WANASHERIA OFISI YA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM WAJIUNGA NA PSPF
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiI8mQfiy3GVjqsEdlx1jpumY-AQRCmL__3UxujIEMeXN5OelNkuEmnjl3sHU44nV8u1wEAj2BFDCEm4o9Hmp_iJ4Vlji0pDWZU0x4JVEh9NmNinjNAy-LfpRhMAlSvEp1kNFFW3BEAAuU/s640/5R5A0287.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiI8mQfiy3GVjqsEdlx1jpumY-AQRCmL__3UxujIEMeXN5OelNkuEmnjl3sHU44nV8u1wEAj2BFDCEm4o9Hmp_iJ4Vlji0pDWZU0x4JVEh9NmNinjNAy-LfpRhMAlSvEp1kNFFW3BEAAuU/s72-c/5R5A0287.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/01/wanasheria-ofisi-ya-mkuu-wa-mkoa-wa-dar.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/01/wanasheria-ofisi-ya-mkuu-wa-mkoa-wa-dar.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy