HomeJamii

TAASISI YA JKCI YAFANYA UPASUAJI WA KUZIBUA MISHIPA YA MOYO ILIYOZIBA KWA ASILIMIA 100 NA KUSHINDWA KUPITISHA DAMU

Na Mwandishi Wetu.   Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Madaktari   Afrika kutoka nchini Marekani kwa ma...

MHE BITEKO AITAKA STAMICO KUITHIBITISHIA SERIKALI KWANINI IENDELEE KUWEPO
NAIBU WAZIRI BITEKO ATAMANI MADINI YACHANGIE ZAIDI PATO LA TAIFA
SERIKALI KUPITIA DAWASA KUJENGA MITAMBO MITATU YA KISASA YA KUCHAKATA MAJI TAKA JIJINI DAR ES SALAAM



Na Mwandishi Wetu.
 
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Madaktari  Afrika kutoka nchini Marekani kwa mara ya kwanza wamefanya upasuaji wa bila kufungua kifua (Catheterization Procedure) kwa mgonjwa na kuzibua mshipa wa Moyo uliokuwa  imeziba kwa zaidi ya miezi mitatu (kwa lugha ya kitaalamu Chronic Total Occlusion).

Upasuaji huo ambao unatumia mishipa ya damu ulichukuwa muda wa saa moja kwa  kuzibua mshipa mmoja wa damu ambao ulikuwa umeziba kwa asilimia 100 na   kushindwa kupeleka  damu upande wa kushoto wa moyo.

Kambi ya Madakari wa Afrika imeanza tarehe 23/1/2017 na inatarajiwa kumalizika tarehe 29/1/2017. Hadi sasa jumla ya  wagonjwa sita wameshapatiwa huduma za matibabu ya moyo ambayo ni kuzibua mishipa ya moyo iliyokuwa imeziba. Hali za wagonjwa zinaendelea vizuri na wanatarajiwa kuruhusiwa siku yoyote kuanzia kesho.

Tangu kuanza kwa mwaka huu wagonjwa 29  wameshafanyiwa upasuaji wa bila kufungua kifua kati ya wagonjwa hao 23 wamefanyiwa upasuaji katika kambi za ndani na wagonjwa sita wamefanyiwa upasuaji katika kambi ya Madaktari Afrika.

Taasisi inaendelea kuwaomba  Madaktari wote nchini wenye wagonjwa wao wa matatizo ya  moyo wawatume wagonjwa hao katika Taasisi ya Moyo  ili waweze kupatiwa matibabu. Kwa mawasiliano zaidi wawasiliane na Dkt. Peter Kisenge kwa namba 0713 236 502 na  022-2151379 ambaye atawaelekeza  utaratibu wa kuwatuma  wagonjwa hao.

Imetolewa na:


Kitengo cha Uhusiano na Masoko
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
24/01/2017
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: TAASISI YA JKCI YAFANYA UPASUAJI WA KUZIBUA MISHIPA YA MOYO ILIYOZIBA KWA ASILIMIA 100 NA KUSHINDWA KUPITISHA DAMU
TAASISI YA JKCI YAFANYA UPASUAJI WA KUZIBUA MISHIPA YA MOYO ILIYOZIBA KWA ASILIMIA 100 NA KUSHINDWA KUPITISHA DAMU
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/01/taasisi-ya-jkci-yafanya-upasuaji-wa.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/01/taasisi-ya-jkci-yafanya-upasuaji-wa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy